Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 116,441
- 215,235
Bado mpaka sasa hazijafahamika sababu hasa za kijana mdogo kama huyu kujizolea umaarufu mkubwa namna hii kiasi cha kuwabwaga wazee kadhaa ikiwa ni pamoja na viongozi waliopo madarakani , wakiwemo mawaziri wa sasa na wa zamani , Sugu ndio Dira na muongozo wa wateule wote kuanzia polisi , Wakurugenzi , wakuu wa wilaya na hata RC's wote wanaokuja Mbeya , Hii si karama ya kawaida !
Ukicheza na mtu huyu waweza kufaidika au kupata hasara , wako Viongozi waliopandishwa vyeo kwa kujaribu kupambana na Sugu , lakini wako walioshushwa vyeo ama kuhamishwa kwa sababu za huyu huyu Sugu pia , Bali jambo lililo wazi ni kwamba Wananchi wa Mbeya huyu Sugu ndio " RAIS WAO " na ukitaka kushushwa thamani ujaribu kupambana naye .