Mbunge wa Mbeya alikuwa mkimbizi wa Kirundi, Je ni kweli?

Yawezekana ni kweli katika kutafuta maisha na alipopata pesa na ideas za kusaidia bongo kama malaria no more akajivua gamba na kurudi, sasa sijui inafanananje na elimu ya nyalandu, mama nagu, udokta wa JK, na ufisadi wa magamba

Hivi unajua tuna waziri foreigner?

better nusu shari kuliko shari kamili

Tunataka kujuwa ukweli wa wanaotuwakilisha bungeni. Kama ni shida ndizo zilizompeleka akawa mkimbizi atueleze au kama ni mkimbizi wa kweli wa kirundi tujuwe vilevile.
 
Sugu kweli amejilipua Uingereza na kweli alishinda kesi yake ya ukimbizi na makaratsi alipata ya kufanyia kazi, na ana pasipoti ya Uingereza ingiwa atumii jina la Mbilinyi.
Mwaka 2000 nimekutana nae Uingereza alikuwa anakaa Milton Keynes, karibia na duka DEBENHAMS, wanaopinga hawajui chochote kuhusu sugu
 
Halafu mbona we mjeshi umekomaa na sugu wivu ni mbaya,mbona mzee mkapa an asili ya msumbiji lakin aliongoza nchi vizur zaid ya handsome kikwete,obama hapend ubaguzi.
 
Sugu kweli amejilipua Uingereza na kweli alishinda kesi yake ya ukimbizi na makaratsi alipata ya kufanyia kazi, na ana pasipoti ya Uingereza ingiwa atumii jina la Mbilinyi.
Mwaka 2000 nimekutana nae Uingereza alikuwa anakaa Milton Keynes, karibia na duka DEBENHAMS, wanaopinga hawajui chochote kuhusu sugu

Hee sasa mkuu passport yake ya Uingereza inatumia jina gani? Hii ndiyo Tanzania usiyoijua; Mawaziri ni madokta wa kughushi, wabunge ni wakimbizi, duh tutafika kweli?
 
Halafu mbona we mjeshi umekomaa na sugu wivu ni mbaya,mbona mzee mkapa an asili ya msumbiji lakin aliongoza nchi vizur zaid ya handsome kikwete,obama hapend ubaguzi.

Mkuu mbona unaenda nje? Hata hilo jina Mbilinyi asili yake si Tanzania. Suala si asili kwa kuwa hata Wenje asili yake ni Kenya na ndugu zake wengi wako Kenya lakini yeye ni Mtanzania. Suala hapa ni kwamba watu wanasema Mr. II alijilipua yaani akakana uraia wa Tanzania na kujifanya ni mkimbizi toka Burundi ili apate kibarua huko ughaibuni. Kwa maana hiyo kama Mr. II hakuomba tena uraia wa Tanzania basi si Raia wa Tanzania ila ni Raia wa Burundi!! Suala si asili ila uraia. Unaweza ukawa na asili ya India lakini wewe ni Raia wa Tanzania. Nani anasema Prof. Shivji siyo Mtanzania?
 
Tuliona Jenerali Ulimwengu alivyotiwa kitahanani wakati wa Mkapa kuhusu uraia wake, nashaangaa hawa uhamiaji leo wanasikia au wanajuwa kuwa kuna Mbunge ambae ni mkimbizi wa Kirundi na ana passport ya kiingereza wanashindwa kumuhoji ukweli. Halafu utakuta mtu kama huyu anaingizwa bungeni, sehemu nyeti na anaingizwa kwenye kamati hata za ulinzi na kadhalika. wakati ukimpima "credibility" yake haimruhusu hata kusogelea jengo la bunge, iwe tu kwa kudanganya kwake huko Uingereza na kula viapo huko kuwa yeye ni Mrundi. Huo ni uongo tosha wa kumvuwa joho la Ubunge.

Nashangaa sana labda iwe alitumwa na serikali ya Tanzania kwenda kuchunguza watu wanaojiruwa huko Uingereza. Kwani lolote linawezekana. Ikiwa huyu anawekwa bungeni na anawachwa kuwa katika mmoja wa mihimili ya hii nchi, kwanini?

Serikali itueleze, alitumwa huko Uingereza au ni yeye mwenyewe aliiidanganya serikali ya Uingereza kwa njaa zake?
 
Mkuu naona hii inamkamata pabaya Mr. II. Kama hakurekebisha mambo yake kama marafiki zangu wengi ambao nawajua kuwa waliji;ipua kama wakimbizi wa Burundi wakaishi huko ughaibuni wakarudi bila kuomba upya uraia wa Tanzania, basi tena Mr. II huenda akawa si Riziki kwenye Ubunge!!

Hamna kesi hapo, maana hakuwai kuukana Uraia wa Tanzania sehemu yoyote hile na hamna hasiye juwa yeye ni Mwenyeji wa Mbeya, Ni sawa na kusema mtu aliwai kuvuta bangi siku nyuma, kama hakukamatwa ni ngumu sana kujenga hoja katika Ushahidi maana unataka kusema atokee kichaa aseme ye si Mtanzania!? Ushahidi hauwezi kuwa huo hata siku moja, kama wangemshitaki kipindi hicho ambacho angeweza kupata ni kesi ya uongo kwa ajili ya kunufaika na nafasi za Wanyarwanda na si Kunyang'anywa Uraia.

Ushahidi wake wa Utanzania bado upo pale pale na haujawai kubadilishwa. Hapo yeye alitumia nafasi kutafuta maisha mbaya ni kama angelikuwa alibadili uraia na kuwa Mnyarwanda!

Kumbuka tena hii yake si official, there is no where in any court of law unofficial matters can edible evidence! Kama nakuumbuka vizuri wakati Nyerere Serikali ya Kenya ilimnyima Raila Passport kamakumdhibiti hasisafiri nje ya Africa Nyerere alimpa Passport ya Tanzania kwahiyo alipokuwa anasafiri huko nje alikuwa anaenda kama Mtanzania, wapo wa South Afrika wengi sana mimi mwenyewe nimesoma na mmoja na alikuwa anatumia passport ya Tanzania ambayo alienda kuibadili baada Mandela Kukamata nchni; hiyo inaweza kuwa mfano wa ambavyo CCM wamearibu nchni, mpaka vijana hawa jinsi ya kujiwezesha na kupambana na maisha yao ya kila siku.
 
Tuliona Jenerali Ulimwengu alivyotiwa kitahanani wakati wa Mkapa kuhusu uraia wake, nashaangaa hawa uhamiaji leo wanasikia au wanajuwa kuwa kuna Mbunge ambae ni mkimbizi wa Kirundi na ana passport ya kiingereza wanashindwa kumuhoji ukweli. Halafu utakuta mtu kama huyu anaingizwa bungeni, sehemu nyeti na anaingizwa kwenye kamati hata za ulinzi na kadhalika. wakati ukimpima "credibility" yake haimruhusu hata kusogelea jengo la bunge, iwe tu kwa kudanganya kwake huko Uingereza na kula viapo huko kuwa yeye ni Mrundi. Huo ni uongo tosha wa kumvuwa joho la Ubunge.Nashangaa sana labda iwe alitumwa na serikali ya Tanzania kwenda kuchunguza watu wanaojiruwa huko Uingereza. Kwani lolote linawezekana. Ikiwa huyu anawekwa bungeni na anawachwa kuwa katika mmoja wa mihimili ya hii nchi, kwanini? Serikali itueleze, alitumwa huko Uingereza au ni yeye mwenyewe aliiidanganya serikali ya Uingereza kwa njaa zake?
Sugu mwenyewe ndio aliidanganya Serikali ya Uingereza hayo mambo yanafanyika sana ata mimi ningetaka kujilipua ningefanya hivyo huko Uingereza wakati nipo huko ukifika pale MILTON KEYNES kuna Watanzania kibao pale kama kariakoo, wanashirikiana na wanasheria wa kinigeria unawapa pesa wanawafungulia kesi za kudai ukimbizi, pasipoti zenu mnazichoma moto, mimi nimekaa sana Berkshire Vanwall Road, Hili jambo badae litakuja kuichafua vibaya CDM
 
Mkuu hapa si suala la ukabila hapa ni suala la uraia. Hiyo post sikuisoma wakati huo. Lakini huenda kuna ukweli ndani yake kwa kuwa kuna kaka yake ambaye naye nasikia alijilipua huko ughaibuni na akawa anaishi kama mkimbizi huko Uholanzi kwa sasa nasikia yupo hapa nchini. Kuna wakati nilimsikia akiwa katika mambo ya akina Aunt Ezekiel!! Kwa mwendo huo huenda ikawa Mr II naye alijilipua. Akanushe habari hii.Watanzania wengi sana walishajilipua kama wakimbizi wa Burundi na baada ya muda wanarudi lakini wanasahau kuuhuisha uraia wao. Kama Mr. II alifanya hivyo basi tena!!Kuna watu wanasema ukitaka kuonekana wewe ni mchafu ama msafi kiasi gani basi ingia kwenye siasa!! Siasa itakuumbua
tunaulizia uraia wa sugu wakati yuko mjengoni?kwa hiyo vyombo vyetu vya usalama sio makini!Ok kama hatuongele ukabila sasa nauliza tena kwani Rostam ni raia wa nchi ipi?
 
Rostam ni Mbulushi kwa asili na ni Raia wa Tanzania kwa kuzaliwa yeye na wazee wake na hajawahi kuwa mkimbizi. Wacha.
sijawahi kusikia hili kabila la kibulushi hapa tanzania labda limeanzishwa na familia ya Rostamu,
 
Hii hoja ni umbea! kwa sababu zifuatazo;
... hakuna evidence (Hapa ktk jukwaa) za either Mbilinyi kupewa ukimbizi wala vielelezo vya yeye kuikana Tanzania. Hivyo mtoa hoja tuletee hata evidence mfano copy ya passport au vitambulisho vyake vyenye vya UK kuonesha ukimbizi.
.... kuna mchangia hoja kasema jina Mbilinyi sio la Tanzania na hivyo kasupport hoja, ukweli ni kuwa Mbilinyi ni jina lenye asili ya Tanzania toka Wilaya ya Makete au Njombe kama sikosei. Yeye Mr. II kapata ubunge Mbeya kwasababu ya uhuru wetu wa kugombea uongozi mahali popote Tanzania ukiwa tu Mtanzania na unakubalika sehemu husika.
 
Mkuu MTM, hayo ndiyo mambo ya kujadili hapa. Kama kuna waziri foreigner atajwe tumjadili. Udaktari wa baadhi ya watu ni kichefuchefu na sijui kuna mtu wa kuwatetea. Ila udaktari wa JK ni sawa kabisa kwa kuwa ni wa heshima. Mimi nadhani wanatakiwa wachukuliwe hatua za kisheria. Kuna jamaa mmoja anaitwa msemakweli aliwaanika wengine wakasema wanmshitaki. Sijui nini kinaendelea. Kosa ni kosa tu uwe Magamba au Ngozi!! Kama magamba wana waziri foreigner ni kosa na asemwe na kama CHADEMA wana Mbunge Mrundi asemwe! Hii nchi ni yetu sote na hawa watu wanatutawala sote.
MTM lete habari

Katika kundi aliloandika Msemakweli Dialo peke yake ndiye aliyemshitaki,wengine walikaa kimya pengine kuashiria ukweli katika kufoji ma-PHD,sijui kesi imefikia wapi
 
Mimi nadhani huna akili na bila shaka wewe ni jobless, je wewe ni "muchengetwa" kamuulize nduguyo Rostam Aziz na huyo Rugemalila mutahaba ambaye ni mganda. Kafie mbali
 
Back
Top Bottom