dimaa
JF-Expert Member
- Jul 30, 2016
- 4,143
- 5,609
Habari za mida wanaJF, ni matumaini yangu mmeamka salama.
Niingie kwenye mada moja kwa moja. Miezi kadhaa iliyopita nilikuwa katika wilaya ya Kondoa ambako mbunge wake ni Naibu Waziri wa Fedha, dakta Ashatu Kachwamba Kijaji.
Nitaongelea hasahasa katika kata ya Kwadelo inayokusanya vijiji vya Kirere cha ng'ombe, Kwadelo na Makirinya.
Hasa kabisa ni katika kijiji cha Kirere cha ng'ombe, hapa kuna tatizo kubwa sana la maji, umeme na barabara. Maji yapo ya mtaro(ntomoko), nashangaa sana sana mheshimiwa mbunge na diwani ndugu Kariati hili suala kwanini halikamiliki?Ni kero sana kwa wanakijiji.
Suala la umeme nguzo bado hazijachimbiwa katika hichi kijiji. Suala la barabara ndo kero kabisa kwa sababu kuna makorongo ambayo ni kitendo tu cha kuweka bajeti/mfuko wa jimbo ili kuboresha hii miundombinu. Sasa hivi hata basi inabidi zikwepe kwenye hiki kijiji kwa kuwa barabara ni mbovu.
Majuzi tu kuliibuka mgogoro wa ardhi( mipaka) kati ya Kwadelo na Mlongia, uliosababisha DC kupigwa mawe na wananchi kwa kuwa alikuwa akilazimisha kumpa mtu anayedaiwa kuwa mwekezaji anajulikana kwa jina la Msukuma. Uliletwa hapa Uzi kuhusiana na hili suala, na tulisikia mbunge mwenzako wa Chemba Bw. Juma Nkamia alivyopaza sauti kukemea hili suala lakini wewe Dr. Ashatu Kijaji kimya. Hata huruma hukuona kwa wananchi wako kupigwa na kuteswa na askari?
Angalia kwa umakini sana usije ukapoteza hili jimbo manake wanachi washaelimika sasa na watu wengi siku hizi washaelimika na elimu ya juu. Tunakuomba ujitafakari upya, nadhani hata wewe ni mdau mzuri sana wa JamiiForums. Lifanyie kazi hili suala ili tuijenge Kondoa yetu.
Karibuni sana kwa maoni ukiwemo mheshimiwa Dr. Ashatu Kijaji na Juma Nkamia.