Mbunge wa Kisiwa cha Mafia atangaza Kutogombea tena 2015

HNIC

JF-Expert Member
Sep 6, 2011
1,898
2,195
SAM_0540.JPG


Katika hali isiyo ya kawaida Mbunge wa Kisiwa cha faia bwana Abdulkarim Shah ameamua kufanya ambayo hayajawahi kutokea kisiwani Mafia. Bwana Shah amesema kuwa anafuata maneno na vitendo vya baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa kutangaza kuwa ana NGATUTA na hatogombea tena ubunge kwa sababu za kiafya na anaona bora azipishe damu changa ambao wanaweza kukifikisha kisiwa cha mafia kuwa na maendeleo kama visiwa vya Taiwan.

Ndugu Shah amesema kuwa anashukuru Mnyaaaz Mungu kumjaalia na anategemea kutoa taarifa rasmi kupitia kwenye ukurasa wake wa Facebook, twitter, na whatsapp. Pia vile vile Shah anasema kuwa kashazifikisha hizo taarifa kwa katibu mkuu wa CCM taifa, Mwenye kiti wa CCM taifa ambao wamefurahishwa sana na uzalendo na siasa za ukomavu za kungatuka akama alivyofanya baba wa Taifa mwalimu Nyerere.

Amesisitiza kuwa yeye sasa hivi anataka afanye jitihada za kwenda kufanya ibada ya Umra na kushughulika na masuala ya uvuvi na pia kuendeleza biashara zake za trucks na bila kusahau kuweka familia yake sawa.

Mbunge Shah amesema kuwa atamuunga mkono mgombea yoyote yule na hasa ikiwa mgombea huyo ni Kijana Msomi na kadhalika. Ikumbukwe kuwa Ndugu Shah alikuwa anasakamwa sana na aliyekuwa mtoto wa jimbo hilo (Omari Kimbau) kuwa Shah alikuwa hajasoma na kaishia darasa la pili na hajui kusoma wala kuandika (sifa ambazo kwa kweli imeshindikana kuzithibitisha).

Omari Kimbao ambaye ana miliki Baa Mbali mbali za Pombe hapa Dar amekuwa naye anafanya kampeni za chini kwa chini na ametenga kiasi cha Bilioni 1 ili kuweza kuwanunua CCM wilaya, Mkoa na Taifa ili jina lake lipite na hatimaye kuupata ubunge wa Kisiwa cha Mafia.

Kama kawaida ya Jamiiforums tutaendelea kuwaletea habari kwa kadri muda unavy
 
kashasoma upepo wa ukawa akaona unavuma ndivyo sivyo, ccm watang'atuka wengi tu
 
yule mtoto wa kimbau amrafiki zake ni kina kinje lazima awe na pesa ya kutosha kuchukua jimbo!!! tuwahurumie wana mafia maana mbele ni giza bado litaendelea
 
Nimependa wasifu wa Kimbau! Anamiliki Baa Mbali mbali za Pombe hapa Dar.........
 
Omari Kimbau(au Shomari Kimbau) yule Drug dealer anayewahusishwa na kuwatumia boxers kwenye biashara hiyo ?
 


Omari Kimbao ambaye ana miliki Baa Mbali mbali za Pombe hapa Dar amekuwa naye anafanya kampeni za chini kwa chini na ametenga kiasi cha Bilioni 1 ili kuweza kuwanunua CCM wilaya, Mkoa na Taifa ili jina lake lipite na hatimaye kuupata ubunge wa Kisiwa cha Mafia.

Kama kawaida ya Jamiiforums tutaendelea kuwaletea habari kwa kadri muda unavy


Hivi hnii Biahsara inalipa sana eheeeeee!
 
Omari Kimbau muuza unga maarufu mwananyamala,pia wakishirikiana na Kinjikitile Ngwale
 
Back
Top Bottom