Mbunge wa Kisese, Luhaga Mpina aitaka Serikali itaje zilipo Tsh. Trilioni 360

Huyu Luhaga Mpina naye si Mwendazake alisemaga ni kichaa kichaa kama yeye! Hivi trilioni 360 anazijua ! Kusoma ukubwani na kwa kuungaunga ni shida sana!
Ameunga unga mkuu huyu mzee kweli?
Ila nae anazingua T sio billion
Nadhani ulimi uliteleza hakumaanisha achokuwa anaongea
 
Mpina yuko kwenye ndoto, nadhani hayuko sawa. Ana natural arrogance ya kisukuma, si alikuwa Waziri, kwanini hakuishauri serikali wakati alikuwa na nafasi nzuri mwaka mmoja tu hata haujapita, mnafiki sana huyu jamaa, appearance tu he looks arrogant.
JF of GT's haiko kwa ajili ya kushambuliana, tueleze kuhusu hizo fedha jinsi unavyozijua.
 
Atakachoambulia ndugu Mpina ni kuambiwa mtetea legacy! Watanzania baadhi yetu hatujui tunachokitaka ama bila kujua ama kwa makusudi mbali na uelewa na nafasi tulizonazo.
====
Tunaomba ufafanuzi hizo tri 360 tunamdai nani?
Tatizo ni kuwa na wabunge wasio na sifa. Wanaoteka nafasi kwa njia haramu wakiwa na nia zao binafsi. Ninaona akili ndogo kuongoza akili kubwa, ni zaidi ya maudhi.
 
Suala la "Transfer Pricing" lipo halali kabisa kisheria. Kwa kuwa moja wapo ya fursa zilizopo za "tax avoidance" na kwa vyovyote vile haliwezi kuhesabika kuwa ni "tax evasion". Ni njia ya kihasibu katika kufanya "manipulation" ili kutafuta unafuu wa kodi endapo "parent & subsidiaries companies" zipo katika nchi tofauti zenye mifumo tofauti ya kikodi.

Kampuni mama inaweza kuhamisha bidhaa ama huduma zake kutoka nchi moja kwenda katika kampuni tanzu. Kampuni mama ya Coca Cola iliyopo USA ambayo ndiyo yenye "patent right" katika bidhaa zake ina haki kusafirisha "concentrate" za bidhaa zake kuja kuzalishwa na kampuni tanzu ya Coca Cola iliyopo Tanzania ili kuthibiti ubora. Kampuni mama husafirisha wataalamu wake kutoka USA kwa malipo ya viwango vya juu na kuja kufanya kazi hapa Tanzania, huku kampuni tanzu ikiwajibika kulipa gharama zao kupitia akaunti zake za benki zilizopo USA.

Katika eneo kama hilo ndipo "manipulation" hufanyika, ambapo anaweza kuja mtaalamu mmoja tu, mathalani Quality Controller, lakini akaambatana na watu wengine kama 10 wasiokuwa na sifa zake, ambao wote watahesabika kuwa ni wataalamu wenye sifa sawa na kulipiwa gharama sawa ili kupunguza faida katika kampuni tanzu na fedha hizo kupelekwa katika akaunti za kampuni mama.
 
Nimejifunza kitu. Asante!
 
Wabunge wangapi wanaelewa alichokuwa anazungumza Luhaga ?
Wana Bodi hili suala la Tranfer Pricing alilogusia Mh. Luhaga Mpina Bungeni limekaaje.

Nimemsikia Mpina akizungumzia suala la ‘transfer pricing’ ambalo wabunge walishauri Serikali wakati wa Bunge la Bajeti mwaka huu kwamba kuna makampuni ya kimataifa 504 yenye miamala zaidi ya Trilioni 105 kwa mwaka na uwezo wa TRA kuyakagua makampuni hayo ni asilimia 1, TRA haina wataalamu, haina fedha na haiwezi kukagua miamala hiyo ya TP na hivyo Serikali haiwezi kupata kodi katika maeneo hayo fedha nyingi za watanzania zinapotea.

“Mhe. Mwenyekiti haya yote kwetu sisi mipango yetu hatuoni kama ni shida lakini tukiletewa hata bilioni 5 tunafurahi kweli kweli lakini fedha zetu zimeshikiliwa na watu hatupati hasira katika hili”

Sasa nini hatma ya Taifa letu katika suala hili la la Makampuni hayo 504 ambayo tunapoteza Trilioni 105 kwa mwaka.
 
Sasa huyo kichaa aliwahi kutoa ushauri huo kwa kichaa mwenzake au alikuwa anaogopa kumwaga ugali wake wakati huo akiwa mezani anakula?
 
Back
Top Bottom