Noti bandia
JF-Expert Member
- May 3, 2020
- 2,145
- 3,355
Hizo trilion 360 ndio zile za makinikia ama. Sijaelewa vizuri
Hizo zilitokana baada ya ripoti ya madini kubaini kwamba kampuni za madini kwa miaka yote zilizokuwepo nchini wakichimba madini walikuwa halipi stahiki ya nchi kwa thamani hiyo kupitia utoroshaji wa makinikia.
Baadae mazungumzo yalipokamilika mkuu wa kampuni kutoka Marekani bwana Thorn alikubaliana kutoa kishika uchumba cha dola bilioni 360
Sijui tafsiri hapo ni ipi ni mpaka mjumbe maalumu aliyeshirika aje afafanue kwa kina ili jukwaa waelewe hizo shilingi trilioni 360 ni zipi?
Inawezekana kwenye baraza walikuwa na mengi ambayo yalikuwa yanajiri ila umma ulifichwa kwa sababu maalumu lakini sasa ufukunyunyu utasababisha balaa kwenye mamlaka.
Hata wewe umekosea ukweli ni huuIlikuwa dollar milioni 400 na sio dollars bilioni
Hii ni kweliAmini usiamini huyo unakutwa kapangwa aongee hayo na spika anajua kabisa kabla. Usidhani huwa wanakurupuka. Hayo ni maigizo
Alikuwa busy na kuhamasisha wananchi kutembea na futi kwa ajili ya kupimia samakiMpina mnafiki tu, si alikuwa Waziri ktk serikali ya awamu ya 5, alikuwa wapi kushughulikia haya anayosema na kama waziri alikuwa na sauti na nafasi kubwa kuwezesha hizo fedha kupatikana na kuipa mbinu serikali wakati ule.
Majitu mengine hovyo sana, once you have given them good position in the government yako kimya tu hawatendi yale wanayojua vema kuisaidia serikali, yakitoka nje ya serikali, yanaanza kupiga kelele, tulishauriiii, tulishauriiiii..
Kwahiyo maana yako ni ipi? Hizo pesa hazipo, kwamba ameongea uongo..?Mpina yuko kwenye ndoto, nadhani hayuko sawa. Ana natural arrogance ya kisukuma, si alikuwa Waziri, kwanini hakuishauri serikali wakati alikuwa na nafasi nzuri mwaka mmoja tu hata haujapita, mnafiki sana huyu jamaa, appearance tu he looks arrogant.
Hao hawajui hela. Siyo kweli, trion 360 ni bajeti ya nchi kwa karibia miaka 10. Hela hiyo inaweza kuendesha bajeti ya nchi bila kutoza Kodi kwa miaka karibia 10. Impossible!!360 Trillion !
Hiyo ni nyingi sana aiseh!
Huyu Luhaga Mpina naye si Mwendazake alisemaga ni kichaa kichaa kama yeye! Hivi trilioni 360 anazijua ! Kusoma ukubwani na kwa kuungaunga ni shida sana!Nimefuatilia mijadala inayoendelea bungeni kuhusu Mpango wa Taifa wa Maendeleo nikamsikia Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina akizungumzia namna Serikali inavyoshindwa kukusanya fedha nyingi kutokana na kutokuwepo usimamizi madhubuti.
“Mhe. Mwenyekiti tulisema hapa wabunge tunazo Trilioni 360 zimeshikiliwa na Mahakama, uamuzi haujatoka nilitegemea kwenye mpango hapa isemwe kwamba hizo Trilioni 360 ziko wapi leo hapa Bunge zima linapiga makofi kwa Trilioni 1.3 tulizopewa na IMF fedha ndogo Trilioni 1.3 tunapiga makofi mpaka mikono inauma na kwakweli tunashukuru kwa hilo"
Mpina alisema asilimia 10 Trilioni 360 ni Trilioni 36 lakini bado hilo halijawauma, Bunge halijaumia, Serikali haijaumia lakini fedha zimeshikiliwa tu kinachosubiriwa ni maamuzi tu ya Mahakama.
“Kama tatizo ni hizo bodi zetu za rufaa za kodi zinashida ya wataalamu si tuajiri hata wataalamu wa kutoka nje kama tatizo ni wataalamu nini kinachosababisha mpango haujazungumza suala hilo?” amehoji
Ni vizuri Wabunge wangeungana kuzidai hizo fedha zingeleka ahueni kubwa na Maendeleo makubwa kwa Taifa letu.