Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia(CUF) ajivua uanachama na ubunge na kuhamia CCM

kilambalambila

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
8,897
2,000
Mimi Maulid Said Abdallah Mtulia Mbunge wa Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Civic United Front – (CUF) Chama cha Wananchi kwa hiari yangu nimeamua kujiuzulu uanachama wa CUF na kujiuzulu nafasi zake zote za uongozi nilizokuwa nashikilia.

Nimefanya uamuzi huu leo tarehe 02/12/2017 kwa utashi wangu na bila shinikizo la mtu yeyote.

BDA72C6C-0B71-4B22-8795-8F6A1F53DA19.jpeg

Sababu za kufanya hivi ni kutokana na uzoefu nilioupata kwa miaka miwili ya ubunge wangu ambapo nimebaini kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho ni chama tawala inafanya kazi kubwa ya kutekeleza Ilani na imefanya vizuri katika mambo mengi ambayo sisi upinzani tuliahidi kuyatekeleza.

Kwa kuwa nia yangu ni kuwatumikia wananchi, sioni sababu ya kuendelea kuwa upinzani na badala yake nimeona ni vema niungane na juhudi za Serikali kwa kumuunga mkono Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli katika kuwaletea wananchi maendeleo na kukabiliana na kero mbalimbali.

Nawashukuru wananchi wa Jimbo la Kinondoni kwa kunipa dhamana ya ubunge katika uchaguzi mkuu uliopita na nawaahidi kuwa nipo tayari kuendelea kushirikiana nanyi katika maendeleo nikiwa katika uwanja mwingine wa siasa ambao ni Chama Cha Mapinduzi.

Pia nawaomba wananchi na viongozi wengine ambao wanatambua mchango wa Rais Magufuli na Serikali yake kutosita kuungana nae katika kazi za kuitumikia nchini badala ya kuwa wapinzani.
======​

Maulid Said Mtulia mbunge wa bunge la Tanzania kupitia Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CUF amejiuzulu uanachama na ubunge kupitia chama hicho kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli.

Amesema mambo yote waliyoahidi tayari yanafanywa vizuri zaidi na CCM hivyo ni vigumu kuwa mpinzani.

Aidha ametanabaisha kuwa kwa sasa ili uwawakilishe wananchi vizuri inabidi uwe CCM kwani ndo kuna sera za kusaidia wananchi kwa sasa. Hivyo imekuwa ikimuwia vigumu kufanya kazi akiwa nje ya CCM
 

Attachments

  • 70300D53-4DA1-47E5-AC79-819D373BC724.jpeg
    File size
    118.8 KB
    Views
    255

mngony

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
3,835
2,000
Kwa Mujibu wa Taarifa ya Habari ya Azam 2 ya leo saa mbili usiku huu, Mbunge wa Kinondoni kupitia Chama Cha Wananchi (CUF)Maulid Mtolea amejivua uanachama wa CUF na kujinga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
 

Domck

Member
Dec 9, 2013
47
95
Mbunge wa kinondoni kupitia chama CUF amejiuzulu nafasi yake ya Ubunge. Chanzo cha habari TBC
 

kombo mzalendo

Senior Member
Dec 20, 2012
119
170
Aliyekua mbunge wa kinondoni said maulid(cuf )ajiuzuli nafas hio na nafasi zake zote ndani ya Chama hicho na kujifungua na ccm akidai kufurahishwa na utendaji wa rais
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom