SAUTI YAKO
JF-Expert Member
- Jan 25, 2014
- 2,920
- 1,997
Mara ya mwisho kukuona ilikuwa kwenye kampeni, sababu kubwa ya uzi huu ni kutaka kujua sisi wakazi wa Kigogo lini tutaanza kuona miradi ya barabara za mitaani maana mitaa mingi jijini Dar ujenzi wa barabara za mitaani zinaendelea tena huku zikinakishiwa na mataa pembezoni, wote tumo ndani ya Jimbo la Kinondoni lakini barabara hizi ziko tu huko huko Kinondoni.
Kigogo ya sasa itapata thamani zaidi kama mtaipa nayo hizi barabara, tena tuna barabara ya kuchepuka ya muhimu inayopitia kule Kigogo sekondari unakuja kutokea hapa Kigogo njia panda lakini nani anayetukumbuka sisi watu wa huku!
Awamu iliyopita walau ilituletea hospitali.
Tafadhali Mheshimiwa ndani ya awamu yako tupambanie tupate hizi barabara.
Nakutakia vikao vyema huko Dodoma.