Uchaguzi 2020 Mbunge wa Kigoma Mjini 2020

Makambako1

Member
Jan 17, 2020
25
38
Tumeingia Ule mwaka wa kuamua hatma ya Kata, jimbo na nchi yetu. Sisi Wana Kigoma mjini tumeamua kuachana na mazoea na siasa zetu za kuoneana huruma.

Kwakuzingatia matakwa ya kikatiba na kanuni zake...

Hivyo basi huyu ni aina ya mbunge tunaemtaka;

1. Asiwe muongeaji sana bali mtendaji. Ajitahidi kuahidi Yale anayoweza, ajiepushe na kudandia dandia tu trendings za kimbeambea huko mitandaoni, asiwe na ahadi 15 tu zitakazomshinda.

2. Afahamu changamoto zilizopo jimboni, hatutaki mbunge anayetegemea kupata changamoto za jimboni kupitia facebook na Instagram. Hatutegemei kuwa na mbunge anaezifahamu changamoto za mbaazi na korosho zaidi ya kufahamu changamoto za Migebuka, dagaaa na mawase. Hatutarajii kuwa na mbunge anaefahamu changamoto za barabara za jangwani na kimara kuliko kuzijua changamoto za barabara za burega na katonga. Mtu anaejua changamoto ya ndoa za viongozi wengine wa upinzani lakini hafahamu changamoto ndani ya ndoa zake.

3. Awe mbunge wa Wana Kigoma, sisi tutamtuma Bungeni na sio Twitter. Watu wa kigoma sasa wataka kuona mbunge anaesimama nao katika jua na mvua, usiku na mchana.

4. Aishi jimboni, tumeona mfano wa wabunge wengi tu wanaoishi jimboni kwao na kutatua changamoto kwa hali na Mali mfano mdogo tu, Mh Sugu pamoja na mavurugu yake huwezi sikia anaishi masaki na kuwazungumzia watu wa newala huko.

5. Awe bunifu na chapakazi. Tumekataa ulaghai, tumekataa misifi ya kijinga. Mbunge Awe ni jicho katika jamii yake, asaidie katika kuziendea na kuzifanyia kazi fursa kwa vitendo. Sidhani kama kuna mtu anaefikiria kuwa na mbunge ambae anachokisema ni tofauti na anachokifanya.

6. Itaendelea...

#CreatAwareness
#KataaPropaganda
#ChangeKigoma
#TimeIsNow
#Cwu2020
 
Sawa bwana tutawalete Mwita Waitara nadhani atawafaa wanakigoma ukizingatia atakuja akiwa na uhakika wa uwaziri mwakani.
 
Hayo maendeleo mnayoyalilia Leo,upinzani hapo kwenu ujiji umeingia lini.?.
Na hao wabunge mlokuwa nao zamani nao walikuwa wanauliza maswali au kusifu na kuabudu?
Kisa mpinzani,aliyekuambia mbona ndo alikuwa Hana lolote tofauti na huyu?..
 
Zitto aliwahi kusema ana uwezo wa kugombea majimbo 6 nchini na akachaguliwa,likiwemo Geita
Aende tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom