Mbunge wa Kigamboni(CCM), Mheshimiwa Dr Faustine Ndungulile:Sipingi Ujenzi wa Mji Mpya Kigamboni

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
[h=3][/h]




DSCN1199.JPG
galleryicon.png
Mheshimiwa Faustine Ndugulile na Fina Mango baada ya kipindi cha Makutano, Magic FM
DSCN1196.JPG
galleryicon.png
Mheshimiwa Ndugulile akisikiliza swali toka kwa Muendeshaji wa kipindi cha Makutano Fina Mango
DSCN1197.JPG
galleryicon.png
Mbunge wa Kigamboni akijibu moja ya maswali aliyoulizwa na wasikilizaji wa Kipindi cha Makutano.Picha na Makutano Show-
-
Mbunge wa Kigamboni, Mheshimiwa Faustine Ndungulile amesema kamwe hajawahi kupinga ujenzi wa mji wa Kigamboni bali alitaka serikali imhakikishie kuwa wananchi wanashirikishwa katika hatua ya maamuzi juu ya mradi wao. Mheshimiwa Ndugulile ameyasema hayo wakati akijibu swali kuhusu msimamo wake juu ya mradi huo katika kipindi cha Makutano, Magic FM.

Mradi huo ambao sasa ni miaka minne tangu uanze kuongelewa umezua mjadala mkubwa kwa wakazi wa Kigamboni, huku Mhe Ndugulile akitolewa kwenye moja ya vikao vya bunge la Jamhuri ya Muungano kutokana na msimamo wake juu ya mradi huo. Alisema tatizo la serikali imekuwa haitaki kufuata sheria inayotaka ushirikishwaji wa wananchi kila hatua katika sera ya mipango miji. Pia aliongezea kusema wananchi wanataka majibu kuhusu lini mradi utaanza, wapi utaanzia, nini hatma yao hasa kuhusu fidia. Alipoulizwa swali na mmoja wa wanakigamboni kuhusu mgogoro uliojitokeza baina yake na madiwani wa jimbo lake uliosababishwa na wao kutembelea moja vikao vya bunge kwa mualiko wa waziri wa ardhi na makazi Mhe Anna Tibaijuka, Ndugulile alijibu kuwa kwa sasa umeisha na kila mmoja ameshajua kosa lake.
chanzo;;haki ngowi.com
 
Huu mradi umekuwa wa siri mnoo kiasi ya kutia wasi wasi
Hebu jiulize kwani ni serikali isiweke bayana mipaka ya huo mjii wa kisasa ?
Mradi huo usiwe sababu ya watu kutofanya shughuli za ujenzi katika maeneo merngine !
Hivi kweli serikali ina uwezo wa kujenga mji mpya kabisa ? Ilishindwa nini Dodoma mpaka leo?
Hivi ukimpa mwekezaji ajenge eneo lote ni wana nchi wangapi watanzania wataweza kununbua nyumba humo?
Jee kweli kuna mwekezaji anayeweza kujenga mjii mzima na kusubiri wanunuzi ?
Mbona mipango mizima ya huu mradi ni giza ?
Kwanini serikali inakuwa bubu
Inachotakiwa kufanya serikali ni kuweka mindo mbinu and then kugawa maneo kwa wananchi kwa masharti maulum
Mfano sehemu A ni kwa resuidence low density
Sehemu B ni residence gorofa 5
Sehemu C ni Ofices hotels na nk
Sehemu ya michezo
Sehemu ya mashule
Wabanchi watamiliki wenyewe mji huo
Lakini ss tumezoea wafadhili.
Na huu ukimya ujue juna rushwa kubwa. Sana ina pangwa



Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom