Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,102
- 4,228
Kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa kutujalia uzima na afya mpaka wakati huu.
Bila ya kuweka maneno mengine mengi nipende kuweka wazi juu ya uhalisia wa eneo la Chasimba hususani eneo lililopo nyuma ya Boko Basihaya eneo ambalo lina historia yake ambayo kwa sasa inapigwa danadana.
Eneo hilo lilikuwa likimilikiwa na wanakijiji lakini baadaye wanakijiji hao miaka ya 1996 walipewa fidia ya mazao kwa msingi kwamba eneo hilo litakuja kumilikiwa na kiwanda cha Twiga cement/Wazo hill na kuna wakati kiwanda kiliweka mpaka kwa kutengeneza njia inayotenganisha maeneo hayo na ya wanakijiji na juu ya hapo kiwanda kilipanda miti pembezoni mwa njia hiyo.
Kwa maana hiyo basi wanakijiji waliokuwa wakimiliki maeneo hayo wanazo kumbukumbu za nilichokiandika hapo na kwa msingi huo kwa kuwa walipewa maelekezo ya kutowekeza vitu vya kudumu katika maeneo hayo kwa kuwa siku yoyote kiwanda kinaweza kikayahitaji na wao walitii hilo.
Historia ya uvamizi ilianza miaka ya 2007 ambapo kuna Mzee mmoja wa kimakonde alihamia katika eneo moja wapo juu kabisa karibu na milima ya kiwanda na kisha kuanza kuuza maeneo kinyemela na baadaye wakaungana na kuanza kuwavamia wanakijiji wengine na kufanya uharibifu wa mazao waliyoyakuta katika maeneo hayo(nakumbuka hata mimi mwenyewe nilikimbizwa na mawe kama mwizi na wavamizi hao nikiwa katika harakati za kuondoa mifugo ambayo ilikuwa katika eneo walilovamia kwa kuwa walikuwa wakiharibu mabanda na kuiba mifugo hiyo ambayo nilikuwa mtunzaji.
Wavamizi hao wapo mpaka leo na wamepata utajiri wao kwa dhuluma ndani ya nchi hii ambayo tunaamini katika haki na usawa.Walichokifanya ni fedheha kwa wanakijiji waliodhulumiwa ni doa lisilofutika upesi nakumbuka hata Polisi kuna wakati walifika katika eneo hilo na kulikuwa na vurugu kwelikweli lakini polisi hawakufanikiwa kuzima vurugu hizo.
Kuna wakati wanakijiji waliodhulumiwa walikwenda mahakamani na kuliwekabshauri lao kwenye mikono ya sheria lakini mpaka leo hakuna jibu la wazi. Kama maeneo hayo ni ya Kiwanda kweli kama kiwanda lkilivyowajulisha hapo awali mbona leo kuna makazi ya watu waliouziwa na wavamizi?
Je hao waliovamiwa na wanajisikiaje ndani ya Nchi yao. Mh Mbunge wa Kawe Halima Mdee haki ni muhimu mno katika ujenzi wa jamii inayoheshimu utu na demokrasia haisaidii kulinyamazia suala ambalo lipo na limeshawaumiza wanajamii.