Mbunge wa Karagwe aomba Rais Magufuli alipopigia push up ujengwe uwanja wa kumbukumbu!

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,863


Katika hali isiyo ya kawaida mbunge wa Karagwe (CCM) Mh Inocent Bashungwa ameomba uwanja wa Kayanga mjini Karagwe ujengwe kama kumbukumbu ya kitendo cha mgombea Urais kupiga push up jukwaani

Akijibu ombi hilo waziri anayehusika na Habari, michezo, utamaduni na sanaa Nape amesema mchakato wa kuenzi kumbukumbu hiyo unaweza kuanza maana kitendo kile kilionyesha ni jinsi gani mgombea wao angetengeneza serikali ya kazi tu na kwamba mgombe mwingine ingekuwa kazi kwake kufanya hivyo.
 
Bora nife kuliko kuwa mshabiki na mwanachama wa ccm.Kama huyo ndiye mwakilishi wa wananchi,hali ikoje kwa wanachama na wafuasi wa hicho "CHAMA CHA MWENDOKASI"(CCM)?

Badala ya kujenga mnara/uwanja ambao watakuwa wakiuona watu wa huko ulipojengwa,nafikiri waweke hizo picha katika noti(fedha)zetu ili kila mmojawetu azione,katika moja ya noti hizo wasisahau kuandika nukuu ya mh.kuwa Saddam Hussein ni Rais wa Kuwait.

Hapa ndipo ccm walipotufikisha,watu wanaongea upuuzi hadi kwenye mihimili ya dola,huu ni ujinga wa kiwango cha PhD na katika dunia hii unapatikana hapa Tanzania pekee.
 
Itabidi ipitishwe sheria kuwa mbunge akitoa hoja za kipuuzi kama hizi basi anakatwa posho anayopokea kwa siku hiyo, na tabia ikijirudia zaidi inabidi afungiwe vikao vya kutosha kama wale kina Zito et al. labda wabunge watakuwa makini zaidi wanapofungua vinywa vyao.

Heri ukae kinywa watu walete tetesi kuwa wewe ni mjinga kuliko kufungua kinywa na kuhakiki kile kilichokuwa ni tetesi.
 
Back
Top Bottom