Mbunge wa Kahama Mjini (CCM), Jumanne Kishimba ataka waliolima Bangi waruhusiwe kuiuza

Naunga mkono hoja..
Bangi ihalalishwe.

Mbunge wa Kahama Mjini (CCM), Jumanne Kishimba amemuomba Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene kuwaruhusu wakulima wa bangi kuiuza katika kipindi cha miezi sita.

Amesema kwa sasa wapo wakulima wa bangi wanaoshindwa kuiuza kwa kuwa kilimo hicho hakiruhusiwi nchini, na kutaka ambao wamelima zao hilo kupewa msamaha wa miezi sita ili waweze kuuza kabla soko la zao hilo kuporomoka.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Februari 3, 2020 bungeni mjini Dodoma katika mjadala wa kamati za Bunge.

Mara kadhaa mbunge huyo amekuwa akiitaka Serikali kuruhusu kilimo hicho kwa kuwa bangi ina soko kubwa ndani na nje ya Tanzania.

Akizungumzia kauli ya mbunge huyo, Spika Job Ndugai ameitaka Serikali kuangalia jambo hilo kwa mapana kwani nchi ya Canada inapata fedha nyingi kupitia zao hilo.

Hoja ya mbunge huyo ikiwaibua mawaziri Angellah Kairuki (Uwekezaji) aliyesema kuna mwekezaji anayetaka kuwekeza katika madawa ya kutumia mbegu za pamba huku Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama akisema Tanzania haina sheria ya kuruhusu kilimo cha bangi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu mzee ni mpumbavu kabisa ! Nchi ina mijadala mizito ya Makonda na Mwamposa anaanza kuwatoa watu mchezoni ! Hovyo kabisa. Mwambie akavute hayo mabangi mwenyewe ! Na ukoo wake mzima !
Haoni mwenzake msiba baada ya kukosa soko la bangi msiba aliamua kuvuta mwenyewe na inampa mafanikio kila Siku anaota kazaliwa chato Lumumba haendi tena kulamba buku saba anatumia falsafa ya when things goes tough let tough goes with it
 
Mbunge wa Kahama Mjini (CCM), Jumanne Kishimba amemuomba Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene kuwaruhusu wakulima wa bangi kuiuza katika kipindi cha miezi sita.

Amesema kwa sasa wapo wakulima wa bangi wanaoshindwa kuiuza kwa kuwa kilimo hicho hakiruhusiwi nchini, na kutaka ambao wamelima zao hilo kupewa msamaha wa miezi sita ili waweze kuuza kabla soko la zao hilo kuporomoka.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Februari 3, 2020 bungeni mjini Dodoma katika mjadala wa kamati za Bunge.

Mara kadhaa mbunge huyo amekuwa akiitaka Serikali kuruhusu kilimo hicho kwa kuwa bangi ina soko kubwa ndani na nje ya Tanzania.

Akizungumzia kauli ya mbunge huyo, Spika Job Ndugai ameitaka Serikali kuangalia jambo hilo kwa mapana kwani nchi ya Canada inapata fedha nyingi kupitia zao hilo.

Hoja ya mbunge huyo ikiwaibua mawaziri Angellah Kairuki (Uwekezaji) aliyesema kuna mwekezaji anayetaka kuwekeza katika madawa ya kutumia mbegu za pamba huku Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama akisema Tanzania haina sheria ya kuruhusu kilimo cha bangi.
KUNA WAHESHIMIWA WENGINE WANALENGA KUFURAHISHA WAPIGA KURA WAO ... KAMA MIMI NINGEKUWA NINARUSIWA KUTOA USHAURI MAMLAKA ZA JUU ZA BUNGE ZINGEPASWA KUANDAA TIM YA WATU WAKIWEPO MAASKARI KUPITA KATA MOJA BAADA YA NYINGINE KTK JIMBO LA MTETEZI WA BANGI. KWA VYOVYOTE TUNGEPATA WANANCHI WENYE MATUMIZI NA MUHADARATI HUO. TUNGEWAKAMATA NA KUWAFIKISHA KTK VYOMBO VYA KISHERIA.

BANGI HAIKUBALIKI MUHESHIMIWAA. SI KUUZA, WALA KULA, WALA KUVUTA, WALA KULIMA, WALA WALA WALA WALA WALA......
 
Ndiyo maana wasomi mnadharaulika.

Mbunge Kishimba milionea mwekezaji wa kimataifa aliyeishia darasa la saba tu,ameweza kufanya utafiti yakininifu kabisa kuhusu zao la bangi.

Unakuja msomi kama wewe tena si ajabu una GPA zaidi ya 4,bila hata kufanya utafiti kidogo tu japo kwa Ku google,unakuja na hitimisho eti mmechoshwa?!

Huyu mzee sasa anatuchosha, mara "bangi iruhusiwe" tena anakuna na "waliolima waruhusiwe" Huyu jamaa inawezekana anauwekezaji huko

Tuonyeshe hayo mashamba kwanza, serikali inajuaje kama watu wanalima wakati ni haramu? Mwisho wa siku atakuja na walio na pembe za ndovu waruhusiwe kuuza! Kwanza huo ujasiri anautoa wapi kwamba kuna wakulima wa bangi Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ndio mpumbavu ila hujielewi tu!

Itakuongezea nini kujadili mwamposa au makonda?

Nchi itafaidikaje kujadili personalities na siyo issues kama Kishimba anavyofanya?

Unatamani nchi iwe na wapuuzi wambea kama wewe?
Huyu mzee ni mpumbavu kabisa ! Nchi ina mijadala mizito ya Makonda na Mwamposa anaanza kuwatoa watu mchezoni ! Hovyo kabisa. Mwambie akavute hayo mabangi mwenyewe ! Na ukoo wake mzima !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo maana wasomi mnadharaulika.

Mbunge Kishimba milionea mwekezaji wa kimataifa aliyeishia darasa la saba tu,ameweza kufanya utafiti yakininifu kabisa kuhusu zao la bangi.

Unakuja msomi kama wewe tena si ajabu una GPA zaidi ya 4,bila hata kufanya utafiti kidogo tu japo kwa Ku google,unakuja na hitimisho eti mmechoshwa?!

Sent using Jamii Forums mobile app
Basi awashauri wakulima bangi muandamane! Biashara haramu hata kilimo chake haramu sasa yeye na wewe mnafikiaje hatua ya kuomba kuuza kwa miezi site?

Mna tani ngapi kwanza mpaka mnahitaji miezi yote site
 
Wakulima wa Bangi wawe na leseni maalumu!ambayo wataruhusiwa kuiuza nje ya nchi nakupata fedha za kigeni!ndani ya nchi isiuzwe bali nje ya nchi zinazotumia!!!MBONA ANNA MAKINDA ANASEMA BANGI YA NJOMBE SIO KALI!MAANA YAKE NA YEYE AMEILA NA KUIVUTA!!HATA JPM ILI AROPOKE VIZURI NADHANI ANAKULA JANI KWANZA!!!
 
KUNA WAHESHIMIWA WENGINE WANALENGA KUFURAHISHA WAPIGA KURA WAO ... KAMA MIMI NINGEKUWA NINARUSIWA KUTOA USHAURI MAMLAKA ZA JUU ZA BUNGE ZINGEPASWA KUANDAA TIM YA WATU WAKIWEPO MAASKARI KUPITA KATA MOJA BAADA YA NYINGINE KTK JIMBO LA MTETEZI WA BANGI. KWA VYOVYOTE TUNGEPATA WANANCHI WENYE MATUMIZI NA MUHADARATI HUO. TUNGEWAKAMATA NA KUWAFIKISHA KTK VYOMBO VYA KISHERIA.

BANGI HAIKUBALIKI MUHESHIMIWAA. SI KUUZA, WALA KULA, WALA KUVUTA, WALA KULIMA, WALA WALA WALA WALA WALA......
We umekariri hakuna kitu kibaya kama kushikiwa akili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom