Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,442
- 3,353
Mbunge wa Kahama Mjini (CCM), Jumanne Kishimba amemuomba Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene kuwaruhusu wakulima wa bangi kuiuza katika kipindi cha miezi sita.
Amesema kwa sasa wapo wakulima wa bangi wanaoshindwa kuiuza kwa kuwa kilimo hicho hakiruhusiwi nchini, na kutaka ambao wamelima zao hilo kupewa msamaha wa miezi sita ili waweze kuuza kabla soko la zao hilo kuporomoka.
Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Februari 3, 2020 bungeni mjini Dodoma katika mjadala wa kamati za Bunge.
Mara kadhaa mbunge huyo amekuwa akiitaka Serikali kuruhusu kilimo hicho kwa kuwa bangi ina soko kubwa ndani na nje ya Tanzania.
Akizungumzia kauli ya mbunge huyo, Spika Job Ndugai ameitaka Serikali kuangalia jambo hilo kwa mapana kwani nchi ya Canada inapata fedha nyingi kupitia zao hilo.
Hoja ya mbunge huyo ikiwaibua mawaziri Angellah Kairuki (Uwekezaji) aliyesema kuna mwekezaji anayetaka kuwekeza katika madawa ya kutumia mbegu za pamba huku Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama akisema Tanzania haina sheria ya kuruhusu kilimo cha bangi.