Mbunge wa Kahama Mjini(CCM), Jumanne Kishimba ashauri Serikali kuanzisha chuo cha wizi

Huyu mzee anapoint nzuri sana. Jambo lingine ambalo lilipata kunisikitisha na ambalo linapoteza tena muda zaidi ni kwa yule mtu mwenye diploma anataka aongeze elimu awe na degree. Sasa jiulize mtu kasoma mpaka kafika form six bahati mbaya akapata division 2 or 3 ikambidi asomee diploma kwa miaka mitatu then akaamua asomee degree yaan anaanza tena moja na mtu ambaye ndio katoka form six fresh na anasoma naye tena miaka sawa ya degree as if hana utofauti naye kabisa. Kwanza lazma serekali na wataalamu walio vyuoni wajue masomo ya diploma kwenye coz fulani yanaendana kwa kiasi kikubwa na masomo ya degree kwa kwenye coz hiyohiyo why Sasa mtu aliyekwisha kusoma diploma asipunguziwe muda wa kusoma degree badala ya miaka minne iwe hata miaka miwili au miwili na nusu kiliko kusoma minne full sawa na form six fresh?
Wote wanao muunga mkono huyu Kishimba ukiwachunguza utakuta ni wale waliofeli au waliosoma kwa kuunga unga.
 
Wote wanao muunga mkono huyu Kishimba ukiwachunguza utakuta ni wale waliofeli au waliosoma kwa kuunga unga.
Kwahyo wewe ndio unaakili kuliko raisi wako aliyekubali maneno ya kishimba? Yaan elimu ya kujifunza kuchora panzi inamsaada gan kwa mtu anayekosa za serekali
 


Mbunge wa Kahama Mjini kupitia CCM Jumanne Kishimba, ameiomba Serikali ifungue chuo cha wizi kwa kuwa matukio ya wizi katika sekta za umma na Halmashauri nyingi umeshamiri kwa kiasi kikubwa na kwamba chuo hicho kitasaidia wale watu wanaoenda kuchunguza wezi, kuzijua mbinu zao na kuwabaini.

Hayo ameyabainisha leo Mei 28, 2020, Jijini Dodoma wakati wa mkutano wa 19, kikao cha 39, wakati wa uchangiaji wa hoja ya Kamati ya Kudumu ya Huduma za Serikali za Mitaa, na kueleza kuwa ni vyema chuo hicho kikawekwa japo kwa kutumia jina lingine ili kukomesha suala hilo.

"CAG na Waziri wa Fedha yuko hapa hawa vijana wanaoajiriwa lazima wanatoka shule inayofundisha maadili mema na uaminifu, sasa wanaenda kupambana na wizi wengine wamesoma Seminari, kwanini serikali haifikirii sasa kuanzisha chuo cha wizi, kwa maana mtu anapochaguliwa kwa sifa ya uaminifu kwenda kupambana na wezi anaenda kupambana nao namna gani? afadhali apite kwenye chuo hicho kwa miezi mitatu ili ajue akili ya wizi, hawa vijana wetu tutawamalizia magerezani na hali ya wizi ni mbaya sana" amesema Mbunge Kishimba.

Credit: EATV

Mwaka jana, Kishimba alitaka kilimo cha bangi kihalalishwe nchini Tanzania Mbunge Jumanne Kishimba (CCM) ataka kilimo cha bangi kuhalalishwa nchini Tanzania

Maoni Yangu
Kumbukeni huyo mbunge alishawahi kuomba Serikali iruhusu bangi itumike kihalali.

Daaaa hao ndiyo wabunge wetu ambao ni watunga sheria na wapitisha miswaada na mikataba mbali mbali.

Kama taifa bado tuna safari ndefu.

Wabunge wa CCM hao, saafi kabisa, kimjaacho mtu ndicho kimtokacho
 
Back
Top Bottom