Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 6,315
- 8,214
Ili kukabiliana na changamoto ya ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu hapa nchini,Mbunge wa Kahama Mjini, Jumanne Kishimba ameshauri vyuo vikuu kuwajibika kutafuta ajira kabla ya kusajili wanafunzi.
Amesema wazazi wengi hasa vijijini wanatumia wamechoshwa na mfumo wa elimu jinsi unavyofilisi mali zao tofauti na matarajio yao.
"Leo hii tunaongeza umasikini baadala ya kuongeza elimu, wananchi hawataki tena kusikia mambo ya shule, vijijini Mheshimiwa Spika ukifika ukiuliza ng'ombe wa hapa wameenda wapi, utaambiwa ng'ombe wamemalizwa na shule" Jumanne Kishimba
kuhusu changamoto ya ajira kwa wahitimu ameshauri vyuo kuwatembelea waajiri na kuuliza nafasi zilizopo ili kusajili idadi wanafunzi kulingna na ajira zilizopo.
"Leo hii nikizungumza kuhusu masuala ya vyuo vikuu naonekana kama chizi, lakini Mheshimiwa Spika, Makampuni yote duniani yanafanya biashara na vyuo vikuu, hapa Tanzania sijaona chuo kinachotembelea waajiri" Jumanne Kishimba
"Mhe. Spika hii inaweza kusaidia kwa sababu inawezakana hata ile elimu wanaotoa Vyuoni si ile inayohitajika kwa waajiri na tufike mahala baadala ya kusoma Degree kwa miaka mitatu wasome kwa miezi nane inatosha ili mtu aendelee na maisha mengine huku umri ukiwa unaruhusu " Jumanne Kishimba
Kishimba ametoa ushauri huo wakati akichangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2021/2022, jijini Dodoma.
Nini maoni yako?