Mbunge wa Kahama Mjini ashauri Vyuo Vikuu kuwajibika kutafuta ajira kabla ya kusajili Wanafunzi

Huyu ni comedian tu na anataka siku zote kuwadharau waliosoma kwa vile yeye ni Darasa la 7. Bado watu hawajasahau namna alivyofanya uharamia wa biashara ndani ya Lake Victoria. Amebeba Sana magendo, amekwepa sana Kodi, ameua sana maafisa wa Serikali.

Na mara ya mwisho kwenye miaka ya mwanzo mwa 2000 alihusika kuwamwagia watumishi wa TRA tindikali. Kisha alipokuwa wanted akakimbilia Zimbabwe.

Kishimba hata madawa ya kulevya ameuaza Sana kwa kubeba kwenye magari yake kati ya SA, Zimbabwe na Tanzania.

Asidharau elimu kwa vile ametajirika kwa njia OVU
Unajua kuna watu, wamewasikia tayari wapi bungeni Hawa watu wakina msuk na kishimba lkn ni maharamia, mafisadi wakubwa pengine Bila hao wasomi kuwasaidia kwenye biashara zao wasingekuwa hapo walipo, wasomi wenyewe wamewafikisha bungeni kwa kuwasoma washindi wa matokeo ya uchaguzi kumbe walishindwa, mtu anao kubali hoja zao ni mjinga kama wao lkn kama umesoma unawapotezea tu
 
Ili kukabiliana na changamoto ya ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu hapa nchini,Mbunge wa Kahama Mjini, Jumanne Kishimba ameshauri vyuo vikuu kuwajibika kutafuta ajira kabla ya kusajili wanafunzi.

Amesema wazazi wengi hasa vijijini wanatumia wamechoshwa na mfumo wa elimu jinsi unavyofilisi mali zao tofauti na matarajio yao.

"Leo hii tunaongeza umasikini baadala ya kuongeza elimu, wananchi hawataki tena kusikia mambo ya shule, vijijini Mheshimiwa Spika ukifika ukiuliza ng'ombe wa hapa wameenda wapi, utaambiwa ng'ombe wamemalizwa na shule" Jumanne Kishimba

kuhusu changamoto ya ajira kwa wahitimu ameshauri vyuo kuwatembelea waajiri na kuuliza nafasi zilizopo ili kusajili idadi wanafunzi kulingna na ajira zilizopo.

"Leo hii nikizungumza kuhusu masuala ya vyuo vikuu naonekana kama chizi, lakini Mheshimiwa Spika, Makampuni yote duniani yanafanya biashara na vyuo vikuu, hapa Tanzania sijaona chuo kinachotembelea waajiri" Jumanne Kishimba

"Mhe. Spika hii inaweza kusaidia kwa sababu inawezakana hata ile elimu wanaotoa Vyuoni si ile inayohitajika kwa waajiri na tufike mahala baadala ya kusoma Degree kwa miaka mitatu wasome kwa miezi nane inatosha ili mtu aendelee na maisha mengine huku umri ukiwa unaruhusu " Jumanne Kishimba

Kishimba ametoa ushauri huo wakati akichangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2021/2022, jijini Dodoma.

Nini maoni yako?

He has a point...Vyuo vikuu vikiacha ukiritimba na kuwajibika kutengeneza ajira ni kazi rahisi sana...Tatizo vyuo vikuu vyetu havipo integrated na mifumo ya governance na wala ile sector binafsi yet wao ndiyo walitakiwa kuwa washauri wa kwanza kwa nchi...Mambo ya kuteuana na kudhani aliyeteuliwa ndiye anapaswa kushauri yanatupoteza sana...Watu hao wachache ambao kwa nafasi zao wanaona wanaweza kutoa ushauri ni udanganyifu wa hali ya juu...Vyuo vikuu viliwekwa ili viweze kutoa elimu na mwelekeo wa nchi kuanzia serikali hadi raia wa kawaida...University ina mission tatu 1. Academics ambayo inahusu knowledge 2. Consultancy ambayo ndiyo ushauri 3. Outreach ndiyo kueneza hiyo knowledge na ushauri katika ngazi ya utendaji...Unashangaa hata kule kwenye baraza la wafanyabiashara hakuna ma professor wanaolishauri...Huyo Professor apeleke sasa ushauri wake wapi na vipi?

Mifumo yetu inatuangusha sana na kusababisha lawama zirudi kwa watu waliofungwa gerezani na mifumo mibaya inayo endekeza competitions for survival badala ya ku produce to meet the basics and in surplus
 
We jamaa una machungu sana kuona mwamba ni tajiri ila wewe na degree yako unalipwa laki 4!

Jamaa ana hoja hilo ndilo la msingi sasa concetrate kwenye kupangua hoja! Hio elimu yako bila pesa ni ushuzi tu kwenye jamii maana hamna kitu utafanya bila hela. Binafsi nigerudishwa utotoni sasa nikaambiwa kuchagua kutafta hela na kusoma ningekimbilia kutafta hela maana elimu ya la 7 inatosha sana kujitambua, hio degree haina maana kama huna hela ni sawa na sifa ya kupendeza tu!
wewe umesoma English medium ila uka fail form four.
 
Sasa huu ulioandika wewe sindio ushuzi wa dengu kabisa!

Wewe toa suggestion kama hoja unayosimamia mbadala ya Kishimba maana degree za uchumi zipo tunaziona zinauza juisi za miwa tu wakati tulitarajia ziende BOT zikashauri mambo ya kiuchumi! Nafasi hizo hamna.

Je, mtu anahitaji degree kukamua juisi ya miwa? Amepoteza miaka takribani 17 kuja kukamua juisi ya miwa ambapo angeweza kuanza hio kazi miaka 10 nyuma! Ni muda kiasi gani amepoteza katika maisha yake kwa miaka 10 nzima!
Una hoja ya maana..kishimba pia ana hoja Ila tatizo linakuja pale mtu anapo anapoongea ukweli,tena kuwasema wasomi
Huwa wanakushukia Kama mwewe
 
Nilicheka Sana aliposema wanaosomea taaluma km ya udaktari ni Sawa Tu wakisoma chuo miaka mitatu maana anachokisomea anafanya practical kwenye hospitali,Hilo wwnanchi hatuna tatizo nalo,sasa wenzangu na mie mfano mtu anasomea procurement sijui wenyewe mnaita manunuzi unasomaje chuo miaka mitatu..unanunua nn miaka yote hiyo km siyo kupoteza muda tu..yaani unasomaje miaka mitatu manunuzi alafu unarudi nyumbani unamwambia mzazi nimesomea manunuzi Nani sasa atakuajiri kwenye Duka,miezi name inatosha degree

Huyu Mwamba na msukuma wananifurahisha sn
Huu ni ukweli
 
Mwenyewe na mkubali.....alihoji.majuzi Kama Kampuni za Simu.Zina mkopesha Pesa mtu zisiye mufahamu hata kwa sura,kwanini Serikali inasumbua raia wake kupata mikopo ,mfn.Bodi ya mikopo ya elimu,mabenki nk?!Si bora kuacha kusoma sasa?!!!!
Bado kuna mtu atakwambia eti hujasoma,sasa wewe uliesoma umetusaidia nini cha maana?
 
Elimu inahitaji marekebisho makubwa sana@ haliwezekani mtu ana bachelor ya economics, lakini bado mia tano ya vocha inampiga chenga mpaka apige mzinga kwa mdogo wake aliyemaliza la Saba tu.
Fani ya economics inahusika vipi kutafuta jero?
 
Back
Top Bottom