Mbunge wa Kahama Bw. James Lembeli atangaza kugombea Uenyekiti Mkoa wa Shinyanga

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Mbunge wa Kahama Bw. James Lembeli, akizungumza na wakazi wa Kata ya Igunda, wakati akitangaza nia ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Shinyanga jana, wakati wa uchaguzi wa Chama hicho mwaka huu. Mwenyekiti wa sasa ni Bw.Hamis Mgeja
 
Na kwanini anakwenda Igunga? Igunga si Tabora tena?
 
mdau ni igunda sio igunga soma sawasawa,naona kaona ampime ubavu mpambe wa Lowassa bwana Hamis Mgeja,utakua ni mpambano wa kukata na shoka kati ya mafisadi na wapambanaji wa ufisadi.
 
Utakuwa mchuano mkali sana,hawa jamaa hawaivi kabisa.Mgeja ni mfuasi wa mafisadi(hata yeye pia)na Lembeli camp ya 6.
 
Huyu LEMBELI hana nyumba Kahama,anakaa Guest,ni sawa na LA na Igunga,hana makazi ya kudumu anakuja kuchuma tu.
 
Huyu LEMBELI hana nyumba Kahama,anakaa Guest,ni sawa na LA na Igunga,hana makazi ya kudumu anakuja kuchuma tu.

Hakuna sifa ya kuwa nyumba ndipo uchaguliwe. Pia yeye ni mbunge wa Kahama alichaguliwaje pasipo kuwa na nyumba kama ingekuwa kigezo. Nyie wafuasi wa Mgeja msipotoshe, tena yeye anagombea uenyekiti wa mkoa
 
Hapo ni vita ya mafisadi na yeye.
Kila la kheri Mh Lembeli.
OTIS
 
Lembeli ni mpambanaji lakini kama ataingia NEC kajimaliza mwenyewe kisiasa, mafisadi watamnunua kwa gharama yoyote! na harakati zake zitaishia hapo.
 
Ndugu yangu nakubali kosa, sikusoma vizuri habari hiyo na ni finyu kwa Kichwa cha Habari.... KWAHIYO Haikuwa na sababu ya kusema Elimu ndio Dosari nimeishi nje ya Tanzania kwa Miaka 27 kutofautisha Igunda na Igunga ni kitu cha kawaida haina sababu ya kuwa wewe ni Elimu ya Darasa la Saba.

Lengo langu la kuweka hiyo Topic ilikuwa ni kuhusu Uongozi wa CCM sasa wanamawazo ya kugombania Madaraka Ndani ya Chama Chao na inasemekana uchaguzi ndani ya CCM sio Mwaka huu; Sasa Inakuaje anagombea Uenyekiti wa Mkoa na inaonyeshwa anaungwa Mkono na Vingunge Ndani ya CCM.

Mantiki ya habari yangu ilikuwa ni CCM na Vyeo Ndani ya CCM na Sio Mimi na Darasa la saba
 
nyie ndo mnamaliza Darasa la saba bila ya kujua kusoma na kuandika na bado sio mataahira! Wapi pameandikwa Igunga??

Ndugu yangu nakubali kosa, sikusoma vizuri habari hiyo na ni finyu kwa Kichwa cha Habari.... KWAHIYO Haikuwa na sababu ya kusema Elimu ndio Dosari nimeishi nje ya Tanzania kwa Miaka 27 kutofautisha Igunda na Igunga ni kitu cha kawaida haina sababu ya kuwa wewe ni Elimu ya Darasa la Saba.

Lengo langu la kuweka hiyo Topic ilikuwa ni kuhusu Uongozi wa CCM sasa wanamawazo ya kugombania Madaraka Ndani ya Chama Chao na inasemekana uchaguzi ndani ya CCM sio Mwaka huu; Sasa Inakuaje anagombea Uenyekiti wa Mkoa na inaonyeshwa anaungwa Mkono na Vingunge Ndani ya CCM.

Mantiki ya habari yangu ilikuwa ni CCM na Vyeo Ndani ya CCM na Sio Mimi na Darasa la saba
 
Mimi sioni tatizo la Lembeli kutangaza nia ya kugombea nafasi ya Uenyekiti mkoa ni haki yake kwa mujibu wa katiba ya CCM kwa hiyo anatimiza wajibu wake kikatiba jamani.
 
Mimi sioni tatizo la Lembeli kutangaza nia ya kugombea nafasi ya Uenyekiti mkoa ni haki yake kwa mujibu wa katiba ya CCM kwa hiyo anatimiza wajibu wake kikatiba jamani.[/QUOTE ]Lakini sio Mapema Mno kwa CCM kugombea cheo ndani ya Chama? nadhani simpaka itanganzwe ?
 
Back
Top Bottom