Mbunge wa Jimbo la Siha, Godwin Aloyce Mollel(CHADEMA) ajivua wadhifa huo na kuhamia CCM

Mnyakatari

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,882
2,000
Naanza kwa ku-declare: SIUNGI MKONO GHARAMA ZITUMIKAZO KATIKA CHAGUZI ZA MARUDIO though sipingani na KATIBA ....

Jambo la kushangaza nguvu kubwa sana yatumika kuwashambulia hao waloyaachia majimbo yao kwa sababu ya kumuunga mkono Rais katika jitihada zake za kusimamia RASILIMALI za TAIFA .... sababu kubwa itolewayo ni UHARIBIFU WA PESA za wananchi kwa ajili ya UCHAGUZI wa MARUDIO ...

Swali Fikirishi: ... Hivi pesa itakayotumika kwa uchaguzi wa marudio jimbo aloliachia Mh. Nyalandu si PESA YA WANANCHI? ... mbona hatukuona POVU JINGI akikemewa Mh. Nyalandu kwa uamuzi wake huo? sana sana twaona akipongezwa kwa uamuzi huo na kuonekana shujaa ....

Akiachia mbunge toka SIDE A kwenda SIDE B twapiga VIGELEGELE na kuliza MAVUVUZELA huku tukimkaribisha kwa shangwe pasi na kutaja HASARA itakayolipata taifa kwa uchaguzi wa marudio ... but

Akiachia mbunge toka SIDE B kwenda SIDE A ni LAANA zamiminika mwanzo mwisho, avuliwa nguo na kufanywa kama HAYAWANI huku akitwishwa zigo zito la MSALITI na tukimlaani kwa kuliingiza taifa katika gharama za uchaguzi mwingine ....

THIS IS DOUBLE STANDARD and HYPOCRISY nothing else ... hebu tuwe WATANZANIA WAZALENDO

Kwanza unatakiwa uelewe kuwa sio kila mtu humu yumo kwenye hayo mavyama yenu unayoyaita side A na side B.Wengine ni watanzania tu na tunakosoa na kusifia bila kujali ujinga wa uchama.Sijui ni wapi umenisoma namsifia Nyalandu kujiunga chadema.Ndiyo maana nasema usifikiri kila mtu ni mshabiki humu na ukaishia kujadili vitu kwa level ya chini tu kishabiki.

Some of us think above partism.Kwahiyo hoja ni ninini sasa nikufafanulie.Kusababisha uchaguzi wa marudio kwa sababu ya kuunga mkono juhudi za ulinzi wa rasilimali huku ukisababisha matumizi ya rasilimali hizohizo unazodai unaungana kuzilinda.Hiki ndo kitu ambacho najaribu kuonyesha jinsi nisivyokubaliana nacho.Hakuna jina la mtu hapo wala hayupo huyo Nyalandu wako.Jifunze kujadili hoja itakusaidia kwenye mambo mengi.Kama Nyalandu nar alisema anahama huko alipotoka kwa sababu ya kuunga mkono juhudi za ulinzi wa rasilimali xa taifa huku akisababisha uchaguzi unaotumia rasilimali hizohizo nae ni kichaa tu.

Pia usielewe kuwa mimi sikubaliani na watu kuhama vyama.Vyama watu wahame lakini kwa sababu za kiitikadi zaidi na sio personalities.Sababu zingine zinazotolewa na wahama vyama ni za kizandiki sana na ni majuha na nyinyi wafia vyama tu ndo wataziamini kwa sababu hazina logic.

Kama ukiweza kujadili juu ya ushabiki wa kivyama na/au wa watu karibu ila kama utastick kwenye hiyo mentality yako ya side sijui A na B tafuta wenzio mbishane.Aksante...
 
Miss Madeko

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
4,150
2,000
Huyu ni masai namfahamu mpaka nyumbani kwao mkuu na yeye ananifahamu vizuri sana kwa jina mpaka home kwetu.
mimi ndio nakwambia huyo ni Mwarusha na sio mmasai wewe kuna tofauti ya usingizi na kifo kati ya mmasai na mwarusha elewa hivyo.
 
busy bees

JF-Expert Member
Aug 26, 2016
2,250
2,000
Kwanza unatakiwa uelewe kuwa sio kila mtu humu yumo kwenye hayo mavyama yenu unayoyaita side A na side B.Wengine ni watanzania tu na tunakosoa na kusifia bila kujali ujinga wa uchama.Sijui ni wapi umenisoma namsifia Nyalandu kujiunga chadema.Ndiyo maana nasema usifikiri kila mtu ni mshabiki humu na ukaishia kujadili vitu kwa level ya chini tu kishabiki.

Some of us think above partism.Kwahiyo hoja ni ninini sasa nikufafanulie.Kusababisha uchaguzi wa marudio kwa sababu ya kuunga mkono juhudi za ulinzi wa rasilimali huku ukisababisha matumizi ya rasilimali hizohizo unazodai unaungana kuzilinda.Hiki ndo kitu ambacho najaribu kuonyesha jinsi nisivyokubaliana nacho.Hakuna jina la mtu hapo wala hayupo huyo Nyalandu wako.Jifunze kujadili hoja itakusaidia kwenye mambo mengi.Kama Nyalandu nar alisema anahama huko alipotoka kwa sababu ya kuunga mkono juhudi za ulinzi wa rasilimali xa taifa huku akisababisha uchaguzi unaotumia rasilimali hizohizo nae ni kichaa tu.

Pia usielewe kuwa mimi sikubaliani na watu kuhama vyama.Vyama watu wahame lakini kwa sababu za kiitikadi zaidi na sio personalities.Sababu zingine zinazotolewa na wahama vyama ni za kizandiki sana na ni majuha na nyinyi wafia vyama tu ndo wataziamini kwa sababu hazina logic.

Kama ukiweza kujadili juu ya ushabiki wa kivyama na/au wa watu karibu ila kama utastick kwenye hiyo mentality yako ya side sijui A na B tafuta wenzio mbishane.Aksante...
Nina imani yangu hukunielewa vyema katika hoja yangu .... hata hivyo nakushukuru kwa kadri ya kuniona nilo kama PUNGUANI ... MFIA VYAMA .... huwa siyajui MATUSI na hivyo sitakutukana .... I remain humble .... by the way thank you sir
 
Mnyakatari

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,882
2,000
Nina imani yangu hukunielewa vyema katika hoja yangu .... hata hivyo nakushukuru kwa kadri ya kuniona nilo kama PUNGUANI ... MFIA VYAMA .... huwa siyajui MATUSI na hivyo sitakutukana .... I remain humble .... by the way thank you sir
Hakuna sehemu uliyotukanwa.Kama unaona ipo bonyeza kitufe cha report abuse uwaambie mods wamipige ban.

Otherwise nachukulia hii kama namna yako nyingine ya kukwepa mjadala wa hoja
 
Allybalowab

JF-Expert Member
Aug 8, 2017
481
250
Mbunge wa Jimbo la Siha kwa tiketi ya CHADEMA, Godwin Ole Mollel ajiuzulu nafasi hiyo pamoja na uanachama wa CHADEMA kuanzia leo Disemba 14, 2017.

Mwanasiasa huyo amesema kuwa ameshindwa kuukataa ukweli huu kuwa hivi sasa uongozi wa nchi yetu chini ya Chama cha Mapinduzi (CCM) umedhihirisha wazi kupigania rasilimali za nchi na kwa kuwa niliomba ridhaa ya Ubunge kwa ahadi ya kupigania rasilimali za nchi nimejikuta sina namna nyingine zaidi ya kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiuzulu Ubunge wangu ili niungane na CCM katika jukumu hili muhimu kwa Taifa.

Nimefanikiwa kuipata barua yake ya kujiuzulu na kujivua uanachama wa CHADEMA;

Video

Watu wengine hawajitambui kuwa kunawatu walipata shida kumuweka hapo waje nakigoma manispaa ina madiwani wengi ni act wazalendo waone kama watapata hata mmoja hiki ndio kitovu cha upinzani upinzani wakweli upo kigoma wengine njaaa sana
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom