Mbunge wa Jimbo la Siha Dr Mollel achangia ujenzi wa Shule Million Nne

Imma Saro

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
394
197
Wazazi wa shule ya sekondari Nuru iliyoko katika kijiji cha Ngaritati kata ya Makiwaru wilayani Siha mkoani Kilimanjaro, kwa pamoja wamepitisha azimio la kuchangia fedha kiasi cha shilingi elfu 50 kila mmoja kwa ajili ya huduma ya chakula kwa wanafunzi wote shuleni hapo shabaha ikiwa ni kuweka mazingira mazuri ya kujifunza kwa watoto wao.

Utaratibu wa kuchangia fedha kwa ajili ya huduma muhimu katika shule hii ikiwemo ile ya chakula ulianza kusuasua mara baada ya serikali kuanza kutoa elimu ya sekondari bure ,lakini kwa sasa imebainika fedha zinazotolewa hazitoshelezi hivyo wazazi wanakutana katika kikao cha dharula na kupitisha azimio kwa ustawi wa elimu ya watoto wao.

Akiwa katika ziara ya kutembelea shughuli mbalimbali za maendeleo katika jimbo lake, mbunge wa SIHA Dr.Godwini Mollel nae anaguswa na hatua iliyofikiwa na wazazi hawa ambapo katika kuwapunguzia mzigo wa uchangiaji nae anachangia milioni nne kwa ajili ya ujenzi wa bweni kwa ajili ya watoto wa kike, madirisha ishirini na nane na milingo mine kwa ajili ya jingo la bwalo na maabara ambalo ujenzi wake ulikuwa umesimama kutokana na kusekana kwa vitu hivyo

Mbunge huyo anaendelea na ziara jimboni kwake kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo barabara,maji na elimu.
 
Back
Top Bottom