Mbunge wa jimbo la Mbozi, Pasco Haonga: CCM imetenga fedha kununua viongozi wa upinzani

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,258
2,000

mbunge wa Jimbo la Mbozi, Pasco Haonga, ameibuka na kuzungumza Miongoni mwa aliyozungumza ni pamoja na madai kwamba Chama cha Mapinduzi kimetenge shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kile alichodai kuwa ni mpango wa kununua viongozi wa Chadema na Upinzani.

“Mimi Pascal Haonga bila kumumunya maneno, wananchi wangu wakiona siku nimehama CHADEMA na kwenda CCM nawaruhusu wakachome nyumba yangu. Sipo tayari kuwasaliti wananchi wangu ” Pascal Haonga
 
shiu yang

JF-Expert Member
Sep 16, 2016
3,294
2,000
hongera kama anaelewa maana halisi ya uongozi
kama kiongozi ananunuliwa au ananunua kiongozi mmoja kuhamia kwenda chama kingine atashindwaje kupokea rushwa,
maana hapo kwa kitendo hicho tayari ni rushwa.
kwa ufupi serikali ya JPM imeodha rushwa na mauaji.
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
170,188
2,000

mbunge wa Jimbo la Mbozi, Pasco Haonga, ameibuka na kuzungumza Miongoni mwa aliyozungumza ni pamoja na madai kwamba Chama cha Mapinduzi kimetenge shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kile alichodai kuwa ni mpango wa kununua viongozi wa Chadema na Upinzani.

“Mimi Pascal Haonga bila kumumunya maneno, wananchi wangu wakiona siku nimehama CHADEMA na kwenda CCM nawaruhusu wakachome nyumba yangu. Sipo tayari kuwasaliti wananchi wangu ” Pascal Haonga
Woga unawatoka wanafunguka sasa.. Safi sana
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,957
2,000
Mtoa rushwa na mpokea rushwa wote ni mafisadi yasiyostahili!

Sasa badala ya kuendelea kulalamika kwamba CCM wananunua wapinzani ni wakati wenu tuone mnakataa kununuliwa ili ionekane tofauti kati ya Wanunuzi/Watoa Rushwa CCM na CHADEMA wanaokataa rushwa!!!

Kama kweli mnanunuliwa na bado mkaendelea kununuliwa, basi hamna tofauti yoyote ile na CCM!!

Ikiwa leo mnaweza kununuliwa na watu kama akina Humphrey Polepole, mngeshindwa kununuliwa na multinational companies endapo CHADEMA mngepewa nchi kuongoza?!

What's the difference?!

Ndo maana kila wakati huwa nasema hii nchi imerogwa kwa ufisadi! CCM tangu kuzaliwa kwake hadi kesho ni mafisadi, upinzani na wenyewe hawana tofauti yoyote na hao CCM!

I hate to say this lakini ndo vile tu watu wanalazimika kuchagua upande but no one better side than the other!

Y'all corrupt!
 
Sijijui

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
7,893

ccm ndo baba na mama Wa uchafu wote unauona TZ mkuu,hao watu wengine unawaonea tu bure
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,957
2,000
ccm ndo baba na mama Wa uchafu wote unauona TZ mkuu,hao watu wengine unawaonea tu bure
Kwamba CCM ndio baba ndio mama wa uchafu wote... NAKUBALI! Na moja ya uchafu ndio huu ambao hivi sasa tunaambiwa wamegeuka kuwa WANUNUZI!

Kama ni kweli WANUNUZI basi wameshaona kuna WANUNULIKAJI outta there!

So, hatutarajii kuona watu wanakubali kuwa BIDHAA vinginevyo, hapatakuwa na tofauti kati ya Mnunuzi na Mnunuliwaji! Ni kama biashara ya Ukahaba!

Hata kama kwa dasturi zetu anayetupiwa lawama za ukahaba ni mwanamke peke yake, lakini Mwanamke na Mwanaume wote ni "Makahaba" tu!!!
 
Tairi bovu

JF-Expert Member
Sep 28, 2017
3,067
2,000
habari isiyokukufurahisha
Sheria za kulinda uhuru habari na maoni zipo kulinda zile habar ambazo hupendi kuzisikia .unazopenda hazilindwi kwakuwa tayat zinakufurahisha. Habar ni jambo lisilo la kawaida kwa tafsir ya kawaida. Hii ni habar kwakuwa sio lengo la kawaida kwa chama cha siasa tena kipo madarakani kinajibisha na kununua viongozi wa upinzani badala ya kutimiza ahadi. Lakini kwakuwa mwenyekiti mzee wa frastrations sio mwanasiasa ngoja kina chakubanga wampige
 
Zakaria Lang'o

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
2,596
2,000
Mtoa rushwa na mpokea rushwa wote ni mafisadi yasiyostahili!

Sasa badala ya kuendelea kulalamika kwamba CCM wananunua wapinzani ni wakati wenu tuone mnakataa kununuliwa ili ionekane tofauti kati ya Wanunuzi/Watoa Rushwa CCM na CHADEMA wanaokataa rushwa!!!

Kama kweli mnanunuliwa na bado mkaendelea kununuliwa, basi hamna tofauti yoyote ile na CCM!!

Ikiwa leo mnaweza kununuliwa na watu kama akina Humphrey Polepole, mngeshindwa kununuliwa na multinational companies endapo CHADEMA mngepewa nchi kuongoza?!

What's the difference?!

Ndo maana kila wakati huwa nasema hii nchi imerogwa kwa ufisadi! CCM tangu kuzaliwa kwake hadi kesho ni mafisadi, upinzani na wenyewe hawana tofauti yoyote na hao CCM!

I hate to say this lakini ndo vile tu watu wanalazimika kuchagua upande but no one better side than the other!

Y'all corrupt!
Acha tabia za kukata tamaa, maana ukitaka kuyaharibu maisha yako na jamii yako, jenga tabia ya kukata tamaa.
Yuda alinunuliwa na Makuhani naye akamsaliti Yesu, je, leo tunawalaumu wanafunzi wote wa Yesu? Ukristo umeenea kila mahali leo kwa sababu, licha ya msaliti, mashujaa hawakukata tamaa!!! Walisonga mbele.
 
Nimekata tamaa kivipi?

Hoja ni kwamba Mtoa rushwa na mpokea rushwa wote ni mafisadi. Kama viongozi wa CHADEMA wanakubali kununuliwa; sasa wana tofauti gani na CCM?

Leo hii tunavyoishambulia serikali ya CCM kutufikisha hapa tulipo kwa sababu ya rushwa; si kwamba wao ndio wanatoa rushwa bali wanapokea kama ambavyo leo hii wanavyopokea viongozi wa CHADEMA.

Mwana-CHADEMA anayeitaka CHADEMA imara angekuwa more concerned na wala rushwa/walio tayari kununuliwa ndani ya CHADEMA kuliko kuwa too more concerned na wanunuzi walio nje ya CHADEMA ambao you've no control over them.
 
Hicho unachokisema ndio 'strategy' ya mnunuzi, kwamba wananchi wasiuamini upinzani kwa sababu wanaweza kununulika kama ambavyo wao CCM wamekuwa wakinunuliwa na mafisadi. Kwa kuamini hivyo wengi wasiotumia bongo zao sawa sawa wataishia kukata tamaa na hivyo kuitaka CCM iendelee maana hata hao wengine wameoza vilevile.
Binafsi naamini wanaonunuliwa kwa fedha au kwa ushawishi wa vyeo si vyama bali watu binafsi ambao kwa utashi wao wanakubali kusaliti dhamana zao kwa umma.
Tabia hii haikuanza leo, ilianzishwa na Mkapa, Magufuli anaiendeleza tu. Ni tabia mbaya ambayo mwisho wake hulazimisha wananchi waliokata tamaa ya mabadiliko waamue kutumia njia za mkato.
Ukimfufua Mobutu wa Zaire ya zamani atatoa ushahidi wa hili ninalolisema. Alinunua hadi vyama; wananchi walipochoka walitumia nguvu, na kwa sababu wengi serikalini na katika vyombo vyake vya ulinzi na usalama hawakuwa wakiridhika na matendo haya, hawakuwa tena na morali ya kuitetea serikali yake. Alianguka.
Pia Mzee Lowasa ametudhihirishia wazi kuwa kumbe hawa viongozi wa upinzani wanashawishiwa aidha na Rais mwenyewe au na walio chini yake. Hali ya aina hii ni mbaya kwa ustawi wa demokrasia nchini. Kwa kweli adui wa demokrasia ni adui wa watu na maendeleo yao. CCM na Mwenyekiti wake katika hili ni maadui wakubwa wa demokrasia na kwa upande mwingine si tu ni watoaji wa rushwa bali pia ni wahujumu uchumi wa nchi.
 
We jamaa unachekesha kweli... eti wanashawishiwa! Kwahiyo wakishawishiwa ndo wanakuwa sio wala rushwa? Au wanashawishiwa huku wameshikiwa mtutu wa bunduki?!

Narudia: Kama kweli wanashawishiwa na wanakubali kushawishiwa hata na akina Polepole; baada ya kupewa nchi wangeshindwa nini kushawishika na kufanya yaliyokuwa yanafanywa na akina Chenge?

Btw, unajigamba kutumia ubongo lakini bado unashindwa kuona hata jinsi mwenyekiti wenu na mwenyewe alivyo sokoni.
 
kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,870
2,000
Mtoa rushwa na mpokea rushwa wote ni mafisadi yasiyostahili!

Sasa badala ya kuendelea kulalamika kwamba CCM wananunua wapinzani ni wakati wenu tuone mnakataa kununuliwa ili ionekane tofauti kati ya Wanunuzi/Watoa Rushwa CCM na CHADEMA wanaokataa rushwa!!!

Kama kweli mnanunuliwa na bado mkaendelea kununuliwa, basi hamna tofauti yoyote ile na CCM!!

Ikiwa leo mnaweza kununuliwa na watu kama akina Humphrey Polepole, mngeshindwa kununuliwa na multinational companies endapo CHADEMA mngepewa nchi kuongoza?!

What's the difference?!

Ndo maana kila wakati huwa nasema hii nchi imerogwa kwa ufisadi! CCM tangu kuzaliwa kwake hadi kesho ni mafisadi, upinzani na wenyewe hawana tofauti yoyote na hao CCM!

I hate to say this lakini ndo vile tu watu wanalazimika kuchagua upande but no one better side than the other!

Y'all corrupt!
Wewe siyo mzima, chadema haijawahi kununuliwa na ccm , chadema ni taasisi wanaonunuliwa ni individuals na transaction zinafanywa kati ya ccm na individual person kama mtulia wala siyo CUF
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,957
2,000
Wewe siyo mzima, chadema haijawahi kununuliwa na ccm , chadema ni taasisi wanaonunuliwa ni individuals na transaction zinafanywa kati ya ccm na individual person kama mtulia wala siyo CUF
Wewe mwenyewe unavyojiona hapo ni mzima?! Kwani tunavyosema CCM mafisadi reference yetu ni nini kama sio individual leaders wanaotokana na CCM?!

Na hoja ya msingi ni kwamba: Kama wananunuliwa na CCM wangeshindwa nini kununuliwa na wafanyabiashara baada ya kupewa nchi kuongoza?

Hawa wabunge mnaosema wananunuliwa na CCM wangekuwa ndio possible ministers!

Sasa kama leo wananunuliwa na akina Polepole; wangekuwa mawaziri si wangekuwa wateja wa akina Acacia? So, wana tofauti gani na mifisadi ya CCM?!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom