TANZIA Mbunge wa Jimbo la Konde Zanzibar, Khatib Haji afariki Dunia

Pole kwa familia yake na wa-Zanzibar kwa ujumla.

Zitto amekuwa mnafki na amekuwa kama tissue ya CCM, ni ngumu kumpa pole zitto, labda watu wengine. Ndiye anachangia kuua upinzani Tanzania na kuendelea kuongozwa kimabavu.
Zitto kachangiaje kujifia kwa chadema?
 
Mbunge wa Jimbo la Konde Ndugu, Khatib Haji wa Chama cha ACT Wazalendo, amefariki Dunia. Umauti umemfika katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili akipatiwa matibabu Alfajiri ya leo.

Khatibu aliwahi kuwa Mbunge wa Konde kupitia Chama cha Wananchi CUF mwaka 2010 hadi 2020. Alishawahi kushika nafasi ya Waziri wa Kilimo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mwaka 1984 hadi 1987

Katika Bunge hili la 12, Khatib amekuwa Mbunge wa tatu kufariki tangu Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. January 21 2021 Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Manyara, Martha Umbulla alifariki dunia na Feb 12, 2021 Mbunge wa Jimbo la Muhambwe, Mkoa wa Kigoma Atashasta Nditiye alifariki Dunia baada ya kupata ajali ya gari.

View attachment 1791420
Mbunge wa Jimbo la Konde Ndugu, Khatib Haji​
Poleni Wafiwa Kazi ya Mungu haina Makosa
 
Mbona Gwajima alijiapiza kuwa kwa kipindi yeye yupo bungeni hakuna Mbunge atakufa kwa Corona? Ndiyo maana nasema huyu Chidi ni mwongo na asiaminiwe kabisa.
 
Hakika sisi ni wa ALLAH na kwake tutarejea, Allah ampe kauli thabit
 
Mtu asie hoja hukimbilia majibu kama haya
unaulizaje swali la kitoto kuhusika kwa Zitto kuifikisha CHADEMA ilipo? na si CHADEMA peke yake bali upinzani kwa ujumla?
Yale mambo ya ujerumani kipindi cha 2013, mambo ya ku-collude na etc ulafu unauliza maswali ya chekechea hapa huo muda si ungeenda hapo kwenu ushetu ukalime mtama
 
unaulizaje swali la kitoto kuhusika kwa Zitto kuifikisha CHADEMA ilipo? na si CHADEMA peke yake bali upinzani kwa ujumla?
Yale mambo ya ujerumani kipindi cha 2013, mambo ya ku-collude na etc ulafu unauliza maswali ya chekechea hapa huo muda si ungeenda hapo kwenu ushetu ukalime mtama
Ndio maana nikakwambia weka hoja zako hapa tuone jinsi anavyochangia kuififisha chadema.
 
Kwani ACT wasaliti waliambulia jimbo lolote kule Zenj baada ya ile dhuluma iliyohusika ikiwemo mauaji?
Kwani wewe uliposema kashinda juzi juzi ulimaanisha alishinda kwa chama gan?
 
Back
Top Bottom