Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini kupitia CHADEMA mh Peter Msigwa akutana na waandishi wa habari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini kupitia CHADEMA mh Peter Msigwa akutana na waandishi wa habari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 19, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145


  [h=3]Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini kupitia CHADEMA mh Peter Msigwa akutana na waandishi wa habari nakuzungumzia kifo cha mwandishi wa habari wa channel ten na mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari Iringa Daudi Mwangosi.[/h]


  [​IMG]
  [​IMG]

  Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini kupitia CHADEMA mh Peter Msigwa akiongea na waandishi wa habari mkoani iringa jana.

  ---
  Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini kupitia CHADEMA mh Peter Msigwa amesikitishwa kuona viongozi wakuu wa serikali kukaa kimya kutokana na kifo cha mwandishi wa habari wa channel ten na mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari Iringa Daudi Mwangosi.  Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Msigwa amesema amesikitishwa sana na kifo cha Mwandishi mwangosi kwani hata kilipotokea yeye alikuwa safarini kuelekea Ujerumani lakini kwa kuufahamu mchango mkubwa aliokuwa nao Mwangosi katika kutetea haki kwa wananchi wa Iringa na tasnia ya habari ilimbidi ahairishe ili kuweza kutoa pole kwa familia ya marehemu.


  Ameeeleza kuwa yeye kama mbunge amesikitishwa sana na kuona viongozi wakuu wanchi kama rais kutozungumzia suala hili na haswa kwa viongozi wa ngazi ya mkoa na wilaya ambao marehemu alikuwa akifanya nao kazi kwa karibu sana.  “Nimesikitishwa sana kuona kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa kuzidi kuwepo ofisini kwa lile lilitotokea, mikono ya kamuhanda na mikono ya Said Mwema imejaa damu, na mimi naungana na wanahabari kuugomea uongozi wa RPC Iringa” alisema.  Ameongeza kuwa anasikitiswa sana Meya wa manispaa wa Iringa Amani Mamwindi kuhusika katika utoaji wa amri ya kuvunjwa kwa vijiwe vya wananchama wa CHADEMA.“Meya ametoa amri ya kubomoa vijiwe vya chadema akieeza kuwa ni amri ya jiji na kuacha jukumu lake kubwa la kuhakikisha kuwa takataka za mji zinatolewa na kuhakikisha uchumi unaendelea na badala yake kuhusika kubomoa vijiwe vya wanachama pamoja na kutoa bendera na hatutaruhusu hali hii iendelee” aliongeza msigwa.  Kuhusu yeye kutoonekana kuwajibika jimboni na kuwa na ziara nyingi za nje Msigwa amesema haendi huko tuu kwa maslahi yake binafsi ila anafanya ili kujifunza mambo mengi ambayo yatakuja kuwasaidia wananchi baadae nahii inatokana na yeye kuwepo katika uongozi wa katika wizara mbalimbali ambapo ziara hizo zina maslahi kwa jamii nzima.  Kutokana na hali hiyo mbunge huyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika mkutano utakaofanyika katika eneo la soko kuu kuanzia saa nane kamili na kuongea na wananchi kuhusiana na mambo mengi yanayohusiana na maendeleo ya jimbo.
  [​IMG]
   
 2. p

  politiki JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  mheshmiwa Msigwa, keep up a Good job, swala la RPC liko wazi kisheria inabidi achukuliwe kwa kwenda kinyume na taaluma ambayo ni kulinda maisha ya watu na siyo kuuwa watu. kuhusu viongozi wa mkoa hao ni makuhaidi wa CCM maadam wakubwa zao wamekaa kimya tegemea nao kukaa kimya nakukumbusha hotuba kabambe ya april 2012 kuwa usitegemee vingozi hao hao walioaribu nchi kuwa na akili au mawazo ya ghafla ya kujenga nchi hii haiwezekani.

  " insanity is doing the same thing and expecting different result" mhe.Frank Msigwa Bungeni april 2012
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Sep 19, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Siamini kama tupo Tanzania, nchi ambayo inasemekana inafuata misingi ya kidemokrasia, haki na utu wa kila moja!
  Siamini kabisa!
   
 4. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,275
  Trophy Points: 280
  Hivi samahani mkuu kwani wewe unaishi nchi gani? maana mabandiko yako mengi huwa unaposti habari za jana au magazeti ya jana!! labda nchi uliyopo tunatofautiana sana masaa?
   
 5. n

  nyantella JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Aisee Mungi!
  unataka kula keki halafu bado ubakie nayo? Tafakari, chukua hatua!!!
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Sep 19, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  chadema wana watu, ccm wana serikali, jeshi, mahakama na magereza
   
 7. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  msigwa ni jembe saana na kauli zake zimesimama saana
   
Loading...