Mbunge wa Jimbo la Hai kwa tiketi ya CCM agoma kuanzisha Kamati ya kusimamia fedha za mfuko wa Jimbo

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,624
21,026
Jimbo la Hai, Kilimanjaro mbunge wake ameamua matumizi ya fedha za mfuko wa jimbo ni zake na fedha hizo zimekuwa siri, kwa mbunge na ameamua kutokuweka wazi matumizi yake kwa kuunda kamati ya kusimamia mfuko huo.

“ kamati ya mfuko wa jimbo, ingehusisha madiwani wote na watendaji wa taasisi za kiraia ili kuangalia ni wapi penye changamoto zaidi papewe kipaumbele,”.

Kinachoendelea Hai ni mbunge kutumia fedha za mfuko wa Jimbo kwa matumizi binafsi na wadiwani wakimuuliza unajenga uadui mkubwa.

===================

Mbunge atoa ufafanuzi kuhusu madai hayo


Akijibu taarifa hizo, Mbunge wa Jimbo la Hai, Saashisha Mafuwe amekanusha uwepo wa madai hayo ya matumizi mabaya ya Fedha za Mfuko wa Jimbo akieleza hakuna ukweli katika suala hilo.

Anasema “Fedha hizo zipo kwa mujibu wa Sheria, haziingii kwenye akaunti ya Mbunge kama wengi wanavyodhani, zinaingia katika akaunti ya Mkurugenzi wa Halmashauri. Zikiingia Mkurugenzi anamtaarifu Mbunge kama Mwneykiti wa Mfuko wa Jimbo ambaye anaitisha kikao kwa ajili ya maelekezo, fedha hizo zinaenda kwenye miradi ya Serikali.

“Mimi huwa huwa ninaita Madiwani tunajadili kuhusu miradi na kuidhinisha, lakini wanaonunua, wanaosambaza, wanaosimamia ni Halmashauri na siyo mimi Mbunge.”

Ametaja Wajumbe wa Mfuko wa Jimbo kuwa ni:

1. Saashisha E Mafuwe (Mb)- Mwenyekiti
2. Leonard Luhwavi - Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na uratibu -Katibu.
3. Judica J. Munisi - Diwani wa Machane Kaskazin -Mjumbe
4. Zanika A. Mushi Diwani V/Maalum-Mjumbe.
5. Hellen J. Munuo- Mtendaji Kata ya Muungano-Mjumbe.
6. Andrew E. Msuya - Mtendaji Kata ya Masama Mashar - Mjumbe.
7. Asifiwe James Malya - Mwakilishi kutoka NGO

Pia soma;

 
Mbona kila kukicha Mafue amekataa kukupa rushwa sasa naona unahangaika naye si uhamie Chadema.
 
Jimbo la Hai, Kilimanjaro mbunge wake ameamua matumizi ya fedha za mfuko wa jimbo ni zake na fedha hizo zimekuwa siri, kwa mbunge na ameamua kutokuweka wazi matumizi yake kwa kuunda kamati ya kusimamia mfuko huo.

“ kamati ya mfuko wa jimbo, ingehusisha madiwani wote na watendaji wa taasisi za kiraia ili kuangalia ni wapi penye changamoto zaidi papewe kipaumbele,”.

Kinachoendelea Hai ni mbunge kutumia fedha za mfuko wa Jimbo kwa matumizi binafsi na wadiwani wakimuuliza unajenga uadui mkubwa.
uliona wapi,! kwa urasimu wa hizo fedha haiwezekani.
 
Kamanda Peno, Fedha za Mfuko wa Jimbo zimetumika hapa machame kukarabati Shule ya Lambo Extended ambayo amesomea Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe, Shule ilikosa hata choo wanafunzi wakawa wanajisaidia machakani ilhali Kuna Mbunge tena Mwanachadema Mwenzetu.

Naona Saashisha Mafuwe kaja kujenga choo na kuijenga upya shule hii, aiseee inabidi tumhoji freeman Mbowe alikopeleka Fedha za Mfuko wa Jimbo wakati wake maana ndie kasababisha masaibu yote Kwa Saashisha. Mbunge Saashisha kakuta Kila kitu Kiko hovyo, Fedha za Mfuko wa Jimbo zimetumika Hadi zimeisha imebidi mbunge aingie fukoni kwenye mshahara wake.
 
Naona ni kheri Saashisha anaetumia Mfuko wa Jimbo Kwa maendeleo ya Jimbo Zima, kuliko Freeman Mbowe ambae alitaka Fedha za Mfuko huo zigawiwe Kwa wenyeviti wa matawi ya Chadema Jimbo Zima Ili zimlinde kwenye uchaguzi wa 2020

Chadema tulieni dawa iwaingie, Mbunge tunaona kazi zake Kila mahali, miundombinu imeimarika Kila mahali.
 
Nasikia Saashisha hataki madada poa, namuunga Mkono maana ni Laana kubwa sana.
Dada Peno ukikataliwa inabidi ukubali tu
 
Freeman Mbowe hata ufanye juhudi gani za kuandika uzandiki Wananchi walishakukataa Kipindi kirefu tu,

Hawa chawa wako wanaandika ugoro na matangopori wanayolishwa na Hawa wahuni wenu waliojificha CCM, muda sio mrefu mtaungana nao uko Chadema
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom