Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu hajui kuwa tumaini pekee walilobakiwa nalo Vijana wa Tanzania ni Mitandao ya simu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,884
ZUNGU HAJUI MITANDAO YA SIMU, NDIO FARAJA PEKEE WALIOBAKI NAYO VIJANA WA TANZANIA??

Na, Robert Heriel

Vijana wengi walikuwa na ndoto kubwa kwenye maisha, wapo waliokuwa na ndoto ya kuwa kupata kazi nzuri wakasoma mpaka Elimu ya juu lakini walipohitimu wakajikuta hawana Ajira.

Wapo Vijana waliokuwa na ndoto ya kuwa wafanyabiashara wakubwa lakini wakajikuta hawana mitaji na waliobahatika kuwa na mitaji wakashindwa kwa sababu ya kodi kuwa nyingi.

Wapo waliotamani kuoa na kuolewa na wenza wazuri wa maumbile na waliojaliwa Utajiri lakini umri ulipofika wa kupata Mwenza wamejikuta hawana hao wenza, miaka inawatupa mkono wamebaki hawaamini.

Wapo waliokuwa na ndoto za kumiliki Majumba ya kifahari lakini mpaka muda huu hawana hata Godoro la kulalalia na umri unawadhihaki kwa tambo.

Wapo waliokuwa na ndoto ya kumiliki magari lakini hata Baiskeli wameshindwa kununua.

Wapo waliotamani kuwa wanasiasa Mahiri lakini baadhi Yao waliishia kujeruhiwa na kuwekwa Korokoroni.

Wapo waliotamani kuwa wanamuziki na waigizaji mahiri lakini wamejikuta wakiwa Mario na wadangaji kama sio Mapunda wabeba Madawa ya kulevya.

Wapo walioona sehemu iliyobaki ni kumtumikia Mungu wakaenda kanisanj na misikitini wakakutana na maji ya upako na maji ya zamzam kutoka Dubai. Dooooh!

Wapo wasioamua kujitolea kufanya kazi bure walau wapate uzoefu Na connection lakini wakajikuta miaka imeenda hawajapata connection wamejikuta muda umeenda bure wakizalishia watu wengine bila kupata faida.

Wapo waliosomesha watoto wao wakitegemea kula matunda ya watoto wao lakini wameambulia patupuu!

Wengine wakaamua kuwa Chawa wa watu mashuhuri ili wajipatie Ulaji wakajikuta wanakuwa Mashoga, na wambeya wenye Tabia za kike.

Wapo walioamua kukopa kwenye taasisi za kifedha ili wafanye biashara wajaribu bahati yao lakini waliishia kufilisiwa hata kile kidogo walichokuwa nacho.

Wapo walioamua kujitoa Mhanga wakaoa na kujipatia wake kwa harusi za kuchangishana kwa jasho na damu. Pasipokuwa na kazi ya uhakika wakaishia kugombana na wake zao baada ya kushindwa kuwatunza. Michepuko ikawa ndio inaendesha familia zao. Hapo ndipo Jina KUDANGA likajitokeza kwa lengo la kupunguza Ukali wa neno UMALAYA.

Umalaya ndio KUDANGA

Malaya hasa walioolewa waliamua kujipatia jina hilo ili Kulinda heshima zao ambazo kimsingi zilishapotea.

Wapo walioamua kujiajiri kupitia Youtube wakaambulia kuwekewa sheria ngumu ambazo wachache ndio wangeziweza, kidogo Rais huyu Aliyeingia Mhe. Samia Suluhu /。 ameliona.

Huko kwenye mambo ya misosi ndio usiseme, mafuta kwa sasa yanauzwa lita moja 6000 -7000Tsh. Vijana wanakula chakula kikavu na kwenda choo kigumu kwani mafuta ni gharama. Sijagusa Sukari.

Mhe. ZUNGU yapo mengi mno hata nikiyataja hapa sitamaliza leo.

Mimi Taikon nakusihi ufute tuu hiyo kauli yako.

Sehemu pekee Vijana waliobakisha ni mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, Jamii forum, Instagram, Til Tok n.k. Huko ndiko wapatapo Faraja ya maisha.

Kuongeza kodi katika mitandao ya simu ni kuathiri Vijana kwenye tumaini Lao la mitandao ya kijamii.

Mitandao ya kijamii kwa Vijana ni kijiwe cha stori. Vijana wote Duniani wanakutana na kujiona wapo sawa kwani hawakutani physically.

Mitandao ya kijamii ni kilinge cha kufurahia maisha kwa Vijana kwani kuna caption zenye vioja Na vichekesho. Kijana achapwapo na maisha halisi basi mtetezi wa furaha yake ni mitandao ya kijamii.

Mitandao ya kijamii ni uwanja wa matangazo ya kazi na biashara.

Vijana masikini hawawezi kulipia matangazo kwenye TV na Redio. Ni masikini. Elfu moja inamtosha kutangaza biashara zake mitandaoni kwenye makundi mbalimbali.

Wengi hupata wateja na kazi mtandaoni.

Mitandao ya simu siku hizi ni sehemu ya kutafutia marafki wapya sehemu ambazo Kijana hawezi kufika.

Mimi Taikon Nina marafiki mpaka nje ya nchi na nimeshatoka mara kadhaa kwa sababu ya mitandao ya kijamii kuniunganisha

Pia mitandao ya simu pia ni sehemu ya watu kutafutia Mwenza wa maisha. Wapo watu ninaowajua wamefunga ndoa wakiwa wamekutana kupitia mitandao ya kijamii.

Mitandao ya kijamii ni sehemu ya kuombea msaada. Wapo watu waliofanikiwa kupata Misaada mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii. Mathalani mtu kama Gj Malisa anatumia mitandao kuchangisha misaada kwa wahitaji.

Mzee ZUNGU, Kwetu Vijana mitandao ni mahali pa kula bata.

Kuelimisha jamii kwa sehemu kubwa kwani ukitoa post itakaowafikia ni wengi.

Ni sehemu ya kujitamba hasa kwa watu waliombali ndio maana kila Kijana akipost picha yake hutafuta location nzuri akiwa lava vizuri. Kujitamba na majigambo ni sehemu ya maisha ya umri wa ujana.

Hukushangaa kwa nini watu walilogwa mayowe vifurushwi vilipoongezwa gharama?

Mbona mafuta watu hawajapiga Kelele sana?

Mitandao ya simu kwa sasa ni kama mke/Mume kwa waliowengi

ZUNGU acha hizo

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro
 
Nakushangaa wewe unayeshangaa matamshi na akili za mbunge wa CCM. Hivi kumbe kuna watu wanategemea jambo jema toka kwa mbunge au mwanachama wa CCM hii?
 
Sisi tunamuachia Mungu.
FB_IMG_1627981456984.jpg
 
Back
Top Bottom