Mbunge wa Ilala (CCM) Mussa Zungu: Wafanyabiashara wamekimbia nchini Tanzania kutokana na kukosekana kwa mazingira rafiki katika masuala ya kodi

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
Mbunge wa Ilala (CCM) Mussa Zungu amesema wafanyabiashara wamekimbia nchini Tanzania kutokana na kukosekana kwa mazingira rafiki katika masuala ya kodi na ushuru. Zungu atoa sababu wafanyabiashara kuikimbia Tanzania

----

Dodoma. Mbunge wa Ilala (CCM) Mussa Zungu amesema wafanyabiashara wamekimbia nchini Tanzania kutokana na kukosekana kwa mazingira rafiki katika masuala ya kodi na ushuru.

Zungu ameyasema hayo bungeni leo Alhamisi Novemba 8, 2018, wakati akichangia Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2019/20.

Amesema bishara katika maeneo ya bandari na maeneo mengine si rafiki kwa wasafirishaji na waingizaji wa bidhaa nchini.
Amesema gharama ya kontena la futi 20 katika Bandari ya Kenya ni Dola za Kimarekani 80 ambayo wamepunguza kutoka Dola za Marekani 103.

Hata hivyo, amesema kwa Tanzania kontena lenye ukubwa huo gharama zake ni Dola za Marekani 170 ni vigumu kwa waingizaji wa bidhaa kuvutiwa kuitumia.

Amesema katika Bandari ya Dar es Salaam inayotegemewa ‘handling charge’ kwa usafirishaji ni Dola za Marekani 100 lakini Kenya ni Dola za Marekani 60.

“Utakuta lazima watu wengi wanahamia katika bandari yenye unafuu, namuomba waziri aendelee kuchagua ushauri wa namna gani anaweza kupunguza tariff (kodi) na kodi za ‘importation’ ishuke ziwe rafiki kwa wafanyabiashara,” amesema.

Aidha, ameitaka Serikali kutazama gharama za kodi na kwamba wakati wanaanza kutoza VAT walianza na kiwango cha asilimia 20 lakini ikaendelea kupungua hadi kufikia 18.

Amesema uzalishaji wa vinywaji baridi umeshuka kwa sababu gharama ni kubwa na Watanzania hawawezi kumudu kununua.
Amesema ukipunguza kodi uzalishaji utakuwa mkubwa na kwamba Serikali haitapoteza kodi bali itaongeza.

Zungu amemtaka Waziri wa Fedha na Mipango kutazama gharama za uingizaji wa sukari ya viwandani na kwamba wawekezaji wanalalamika hawajarudishiwa fedha walizoweka kama deposit kwa miaka mitatu.

“Sasa zimefika zaidi ya Sh45bilioni na hii ni mitaji ya wafanyabiashara na wanalipa kodi vizuri. Serikali ikitazama maeneo ya kushirikiana nayo mapato mengi ya kodi itayapata. Viwango vikubwa vya kodi tunavyoviweka vinawakimbiza wafanyabiashara,” amesema.

Amesema wafanyabiashara wengi wanakimbilia nchi nyingine na kuomba kuwa na utaratibu mzuri wa kodi ambao utawavutia wafanyabiashara wengi nchini.

Chanzo: Mwananchi
 
Rejea Gazeti Mwananchi ,Ndio hali halisi hofu na mazingira yasiyo rafiki. Unadhani MO na mtL wame hold mipango mingapi!?
 
Mazingira yakifanywa Rafiki Kwa Wafanyabiashara Pia tunalalamika

Tax holiday Ni Moja ya hayo Mazingira Rafiki lakin tukawa tunaponda
 
Hali tete kweli, Tanzania ya leo si vijana, si watoto, si wazee wote wanapigana vikumbo kwenye kubeti.

Ukute sasa wanaombana peni halafu deadline imekaribia, wanavyotukanana sasa kama wote rika moja vile kumbe ni mtu na mwanae/mjukuu.

Na haya ndio matokeo ya utawala wa jiwe, anatuambia uchumi unapanda tutembee vifua mbele, kweli???
 
Mbunge wa Ilala (CCM) Mussa Zungu amesema wafanyabiashara wamekimbia nchini Tanzania kutokana na kukosekana kwa mazingira rafiki katika masuala ya kodi na ushuru. Zungu atoa sababu wafanyabiashara kuikimbia Tanzania

----

Dodoma. Mbunge wa Ilala (CCM) Mussa Zungu amesema wafanyabiashara wamekimbia nchini Tanzania kutokana na kukosekana kwa mazingira rafiki katika masuala ya kodi na ushuru.

Zungu ameyasema hayo bungeni leo Alhamisi Novemba 8, 2018, wakati akichangia Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2019/20.

Amesema bishara katika maeneo ya bandari na maeneo mengine si rafiki kwa wasafirishaji na waingizaji wa bidhaa nchini.
Amesema gharama ya kontena la futi 20 katika Bandari ya Kenya ni Dola za Kimarekani 80 ambayo wamepunguza kutoka Dola za Marekani 103.

Hata hivyo, amesema kwa Tanzania kontena lenye ukubwa huo gharama zake ni Dola za Marekani 170 ni vigumu kwa waingizaji wa bidhaa kuvutiwa kuitumia.

Amesema katika Bandari ya Dar es Salaam inayotegemewa ‘handling charge’ kwa usafirishaji ni Dola za Marekani 100 lakini Kenya ni Dola za Marekani 60.

“Utakuta lazima watu wengi wanahamia katika bandari yenye unafuu, namuomba waziri aendelee kuchagua ushauri wa namna gani anaweza kupunguza tariff (kodi) na kodi za ‘importation’ ishuke ziwe rafiki kwa wafanyabiashara,” amesema.

Aidha, ameitaka Serikali kutazama gharama za kodi na kwamba wakati wanaanza kutoza VAT walianza na kiwango cha asilimia 20 lakini ikaendelea kupungua hadi kufikia 18.

Amesema uzalishaji wa vinywaji baridi umeshuka kwa sababu gharama ni kubwa na Watanzania hawawezi kumudu kununua.
Amesema ukipunguza kodi uzalishaji utakuwa mkubwa na kwamba Serikali haitapoteza kodi bali itaongeza.

Zungu amemtaka Waziri wa Fedha na Mipango kutazama gharama za uingizaji wa sukari ya viwandani na kwamba wawekezaji wanalalamika hawajarudishiwa fedha walizoweka kama deposit kwa miaka mitatu.

“Sasa zimefika zaidi ya Sh45bilioni na hii ni mitaji ya wafanyabiashara na wanalipa kodi vizuri. Serikali ikitazama maeneo ya kushirikiana nayo mapato mengi ya kodi itayapata. Viwango vikubwa vya kodi tunavyoviweka vinawakimbiza wafanyabiashara,” amesema.

Amesema wafanyabiashara wengi wanakimbilia nchi nyingine na kuomba kuwa na utaratibu mzuri wa kodi ambao utawavutia wafanyabiashara wengi nchini.

Chanzo: Mwananchi
mh jamani tutafika kweli
 
Kwa wale ambao awamu ya tano imewachapa vilivyo nyumbani kwa mzee Masaki huduma za catering zinaendelea kama kawaida mpaka kesho karibuni sana.
 
Mbunge wa Ilala (CCM) Mussa Zungu amesema wafanyabiashara wamekimbia nchini Tanzania kutokana na kukosekana kwa mazingira rafiki katika masuala ya kodi na ushuru. Zungu atoa sababu wafanyabiashara kuikimbia Tanzania
kesho nyumbani kwa Zungu movie itakuwa hivi.....

sauti inagonga mlangoni: ngo! ngo! ngo!
Zungu: who's there?
sauti ya mtu toka mlangoni: mkuu, sisi ni maofisaa toka uhamiaji!
Zungu: uhamiaji?
sauti toka mlangoni: ndiyo mkuu.

Zungu anafungua mlango.. vijana watatu wanaingia wanajitambulisha wametoka ofisi ya uhamiaji. shikamoo/marahaba zinapita.

Zungu: niwasaidieni nini vijana?
vijana wageni: mkuu, tumekuja kukutaarifu kuwa kesho ufike uhamiaji makao makuu ukiwa na passport yako
Zungu: kwani kuna nini?
vijana wageni: mkurugenzi ndiye ana maelezo yote mkuu.

Zungu kaishiwa nguvu...

Dhisi kantri buana!!
 
Hapana @nudawote penye ukweli acha pabaki kuwa kweli... Zungu ni mwathirika katika biashara zinazosimaniwa na ndugu zake walio nje ya nchi
Wewe unajitambua sana,hukuwa na Sababu ya kumwelewesha huyo hayawani wa kuzimu,hana analojua zaidi ya CCM ni nzuri na magufuli ndo mungu wake,ndo maana kazi yao ni kusifia kila uharo,it's only almighty God who deserves praise and not a mankind
 
Wewe bwaya, usimuwekee maneno mdomoni Mh. Zungu, kada mwaminifu wa CCM
Yani unafikiri Mh Zungu anaishi maisha yake kutokana na ukada wake wa CCM tu..?

Kwamba ukishakuwa mwana CCM una kazi ya kusifia tu..pumbafff sana.

Kwa taarifa yako Mh Zungu ni Mfanyabiashara mzuri tu, he is one of the good importers kwenye motor vehicle spare parts na vitu vingine..

So he talks what he knows in deep na anachosema ndio uhalisia wenyewe.
 
Back
Top Bottom