Mpekuzi Tanzania
JF-Expert Member
- Mar 11, 2018
- 585
- 906
Sikiliza Video fupi ya Mchango wa Mbunge wa Jimbo la Igunga kwenye kuchangia Mpango wa Maendeleo wa Taifa Bungeni
=======
Akizungumzia suala la Ushirikishwaji katika Utumishi Umma, Mbunge wa Igunga, Nicholaus Ngassa amesema:
"Kuna changamoto kwenye Utumishi wa Umma. Tuna Sheria ya Utumishi wa Umma No. 8 ya 2002; tuna Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za 2003; na Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za 2009. Vyote katika muundo wake na maelezo yake havitoi havitoi nafasi katika suala la ujuzi...
Malaysia walipofanya mabadiliko ya kilimo na viwanda walikuja na kitu wanakiita Energizing Civil Service. Waliamua kuweka nguvu kwenye kubadilisha mfumo wa Utumishi wa Umma wakawa na mfumo unaoangalia Knowlegde, Skills na Ability ambavyo vikawa ndo vinampa mtu nafasi ya kufanya maamuzi katika Utumishi wa Umma...
Sisi bado tuna mfumo wa Meritocracy, ambao ni mfumo wa kizamani. Na ndiyo maana mfumo wetu wa Utumishi wa Umma umejengwa vizuri sana lakini unafanya kazi kizamani. Bado tunatumia model za kina Max Weber, za seniority.
Unapotumia mifumo ya seniority maana yake watu wenye uwezo, wenye ubunifu wanakosa nafasi za kufanya maamuzi. Michango yao inaishia chini. Unakuta maamuzi yanaishia kufanywa na Wakurugenzi, Wakuu wa Idara na Wakuu wa Vitengo.
Tuunde mfumo sheria hizi zibadilishwe kuwe na mfumo wa kubadilisha vikao vya maamuzi vijumuishe watumishi wa kawaida ambao wengi wanakuwa na uelewa mpana. Tunapokuwa na mawazo ya wachache, matokeo yake kwenye utekelezaji tunakwama...
Tunatolea mfano suala la ubunifu wa vyanzo vya mapato. Kila siku vyanzo vinarudi vilevile; utaishia sijui vichungi vya sigara, vileo vikali. Wanaobuni vyanzo vya mapato ni walewale miaka yote, watumishi wa chini hawashirikishwi..."