Mbunge wa Igunga, Nicholaus Ngassa: Kuna changamoto kwenye Utumishi wa Umma. Wenye ubunifu wanakosa kufanya maamuzi, michango yao inaishia chini

Mpekuzi Tanzania

Senior Member
Mar 11, 2018
185
500
Sikiliza Video fupi ya Mchango wa Mbunge wa Jimbo la Igunga kwenye kuchangia Mpango wa Maendeleo wa Taifa Bungeni

=======

Akizungumzia suala la Ushirikishwaji katika Utumishi Umma, Mbunge wa Igunga, Nicholaus Ngassa amesema:

"Kuna changamoto kwenye Utumishi wa Umma. Tuna Sheria ya Utumishi wa Umma No. 8 ya 2002; tuna Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za 2003; na Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za 2009. Vyote katika muundo wake na maelezo yake havitoi havitoi nafasi katika suala la ujuzi...

Malaysia walipofanya mabadiliko ya kilimo na viwanda walikuja na kitu wanakiita Energizing Civil Service. Waliamua kuweka nguvu kwenye kubadilisha mfumo wa Utumishi wa Umma wakawa na mfumo unaoangalia Knowlegde, Skills na Ability ambavyo vikawa ndo vinampa mtu nafasi ya kufanya maamuzi katika Utumishi wa Umma...

Sisi bado tuna mfumo wa Meritocracy, ambao ni mfumo wa kizamani. Na ndiyo maana mfumo wetu wa Utumishi wa Umma umejengwa vizuri sana lakini unafanya kazi kizamani. Bado tunatumia model za kina Max Weber, za seniority.

Unapotumia mifumo ya seniority maana yake watu wenye uwezo, wenye ubunifu wanakosa nafasi za kufanya maamuzi. Michango yao inaishia chini. Unakuta maamuzi yanaishia kufanywa na Wakurugenzi, Wakuu wa Idara na Wakuu wa Vitengo.

Tuunde mfumo sheria hizi zibadilishwe kuwe na mfumo wa kubadilisha vikao vya maamuzi vijumuishe watumishi wa kawaida ambao wengi wanakuwa na uelewa mpana. Tunapokuwa na mawazo ya wachache, matokeo yake kwenye utekelezaji tunakwama...

Tunatolea mfano suala la ubunifu wa vyanzo vya mapato. Kila siku vyanzo vinarudi vilevile; utaishia sijui vichungi vya sigara, vileo vikali. Wanaobuni vyanzo vya mapato ni walewale miaka yote, watumishi wa chini hawashirikishwi..."

Mbilima yimo

Senior Member
Sep 14, 2020
162
250

Muda wa kutunga hizo sheria nzuri wautoe wapi wakati wao wana muda wa kutunga sheria za kuwalinda wao waendelee kutawala na za kuwabana wanaoonekana kuwakosoa.
 
Omera Yawa

JF-Expert Member
May 5, 2016
945
1,000
ila hili suala la vyanzo kubuniwa na wa chini inaweza kuwa na matokeo chanya au la, sababu ubunifu na mawazo chanya yanaweza kutokea kwa yoyote yule sio kwa kigezo cha wa chini tu, maana hata hao waliopo juu sasa hivi nao walikuwa chini hapo kabla...ni wachache sana ambao hawajawahi kuanzia chini

cha msingi mifumo itoe kipaumbele kwa wenye mawazo chanya na endelevu bila kujali nafasi walizopo
 
jiwe angavu

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
2,884
2,000
Sikuhizi kuna Google form watengeneze..kisha wasambaze link kwenye groups mbalimbali..mbona watapata mawazo mengi mpaka watachoka..shida ni uvivu wa kufikiri wakiamini wanajua kila kitu.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom