Mbunge wa Igunga, Dalaly Kafumu mikononi mwa TAKUKURU

Wanajuana wale kesi za takakuku ziko wapi zinapambagwa hivyo hivyo zinaishia hewani, mnakumbuka bwana ninja na watu wake tena jezi zao
 
Mbunge wa Igunga Dalali Kafumu anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa tuhuma za kugawa milungula kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa JIMBO ili waweza kumpa kura kwenye mchakato wa uteuzi wa wagombea.

Heko kwenu takukuru lakini msiishie kuhoji tunataka kuona wakifikishwa mahakamani kujibu tuhuma, Sheria yenu ya 2007 inawapa Mamlaka.

Tunataka Taifa lenye mwelekeo wa maono ya Mkuu wa Nchi kuelekea uchumi wa kati

Jamaa ana bahati mbaya sana huyu!!
 
Ndio yule mheshimiwa Rais alisema kamera zilimnasa anawawinda wajumbe wa KAMATI YA MAKINIKIA APINDISHE ripoti ya kamati kwa kutumwa na mabeberu
Huyu amekwisha! Nahisi pia hana upepo na siasa. Ni mtu ana Ph.D lakini hakuwahi hata kupata unaibu waziri. Mbaya zaidi akapatikana na hilo la makinikia. Sasa tena PCCB!
 
Siasa haziaminiki. Inaweza kuwa ni maandalizi ya mchezo urakaokuja kuwagharim upinzani. Wao watakamatwa kuhojiwa wakati ambao wanatakiwa kwenye shughuli za uchaguzi.

Mara hii mmesahau ushindi wa kesi za uchaguzi zilivyopigwa kwa ustadi?
 
Hakuna cha mlungula wala nini sema haziivi mzee mkubwa
Mbunge wa Igunga Dalali Kafumu anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa tuhuma za kugawa milungula kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa JIMBO ili waweza kumpa kura kwenye mchakato wa uteuzi wa wagombea.

Heko kwenu takukuru lakini msiishie kuhoji tunataka kuona wakifikishwa mahakamani kujibu tuhuma, Sheria yenu ya 2007 inawapa Mamlaka.

Tunataka Taifa lenye mwelekeo wa maono ya Mkuu wa Nchi kuelekea uchumi wa kati

Huyu amekwisha! Nahisi pia hana upepo na siasa. Ni mtu ana Ph.D lakini hakuwahi hata kupata unaibu waziri. Mbaya zaidi akapatikana na hilo la makinikia. Sasa tena PCCB!
PhD anangangania siasa ndy ajira
Kweli siasa inalipa boongo

Ova
 
Kafumu hata asingekamatwa na takukuru,bado asingepitishwa kugombea ubunge na itategemea nimeamkaje

Wana bifu la muda mrefu sana,na hapo ni machinjioni kwake
 
Hakuna jitu fisadi kama hilo Dalali Kafumu mikataba yote ya wizi Ya Marino limo hilo loo!!!.Andrew Chenge na huyo Kafumu CCM wasiwarudishe. Raisi Magufuli hawa wawili ukiwarudisha kugombea ubunge utakuwa hujawatendea haki watanzania
 
Mambo ya kumpangia malaika mkuu mmeanza lini? Alishasema apangiwi
 
Back
Top Bottom