Mbunge wa Hanang Mhandisi Hayuma asisitiza wanafunzi kula Shuleni.

John Walter

Member
Aug 14, 2017
59
57
Na John Walter-Hanang

Mbunge wa Jimbo la Hanang mkoani Manyara Mhandisi Samwel Hayuma amewataka wazazi na walezi kutimiza wajibu wao wa kuhakikisha wanafunzi wanakula chakula cha mchana shuleni .

Hayuma ametoa Kauli hiyo wakati wa mahafali ya 22 katika shule ya msingi Bassotughang iliyopo Kata ya Hidet Wilayani humo ambapo amesema wazazi na walezi wa shule hiyo pamoja na shule nyingine wilayani hapo wanapaswa kuhakikisha wanatimiza majukumu yao kwa wanafunzi hao kwani serikali imeshatekeleza wajibu wake kupitia elimu bila malipo.

Amesema wanafunzi wanapokuwa wanakula shuleni kiwango cha taaluma huongezeka.

Amesema, mpango wa utoaji wa chakula Shuleni ambao wazazi hutakiwa kuchangia kwa mujibu wa sera ya Elimu pasipo malipo, husaidia kuleta usawa kati ya walionacho na wasionacho, kuimarisha mahudhurio na kutunza muda wa ratiba za shule na kusisitiza kuwa endapo mambo haya yote yatafanyika kiusahihi yanamchango mkubwa kwa wanafunzi kufanya vizuri darasani.

Hata hivyo ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika shule hiyo katika kuboreha miundombinu yake kwani naye alisoma hapo elimu yake ya msingi mwaka 1990.

vlcsnap-2021-09-29-14h27m44s7.png
 
View attachment 1957148
Wazazi wote wana uwezo wa kuchangia?

Mbunge anasema wajitahidi kutimiza wajibu wao, je nyumbani wanao uwezo wa kutimiza wajibu wa kuhakikisha wanakula mlo wa usiku pia?. Kwa kulazimisha wachangie chakula cha shule haoni kuna uwezekano chakula chote cha familia hasa zile maskini kikapelekwa shule anayosoma mtoto mmoja tu wa familia na kusababisha watoto wengine wa familia kukosa mlo mchana?
 
Kwahiyo nini kifanyike?
 
Kwahiyo nini kifanyike?
Suala la chakula aachiwe mzazi ndiye apange mwanae ale nini kulingana na uwezo wa mzazi. Hilo ni jambo binafsi huwezi kupanga watoto wale nini wakati hujui uwezo wa mzazi.
 
Kwahiyo wabebe chakula? Maana kula ni hitaji la lazima kwa binadamu.
 
Wewe ni mtanzania ? maana nashangaa swali lako!. Kwani wewe kama una watoto ili wale unafanyaje?

Kwani watu wanalishwa bure? Unafahamu kuna shule wanakula chipsi kuku kwa sababu wazazi wao wanao uwezo. Kama mzazi hana uwezo mwanae atakula nyumbani na wenzake kile wazazi walichojaliwa kupata siku hiyo. Kama unawahurumia watoto wasio na uwezo uwalishe bure siio mbunge ajifanye ana uchungu na watoto huku anawaongezea umaskini wazazi kwa kuwalazimisha waingie katika programu ambayo hawana uwezo nayo. Chakula hicho kinachochangwa kwanza kuna wizi humo humo kinaanza kuibwa kuanzia stoo, wapishi na waalimu; plus hicho kinachomfikia mtoto chote hicho anagharimia mzazi. Pia watoto wengine kutokana na levo za wazazi wao hawali chakula hicho ambacho ni inferior hivyo kuwachangisha ni kuwaongezea gharama zisizowahusu.

Wanasiasa waache tabia ya kujifanya wana uchungu na mtu kuliko mtu mwenyewe.
 
Aiseee!!!
 
Back
Top Bottom