Mbunge wa Geita Mjini ashauri wananchi kutotumia mikopo ya Halmashauri kulipa ada

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,663
2,000
Mbunge wa Geita Mjini, Constantine Kanyasu amewatahadharisha wananchi ambao ni wanufaika wa mikopo ya Halmashauri jimboni kwake kutoitumia mikopo hiyo kwa matumizi yasiyokusudiwa ikiwamo kulipa ada za shule kwani kufanya hivyo kutawafanya washindwe kuirejesha na kuishia kwenye mikono ya sheria.

Kanyasu alitoa tahadhari hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akizungumza na vikundi 65 vya wanufaika wa awamu ya pili ya mikopo ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita na kusisitiza kuwa mikopo hiyo inatolewa kama mitaji ya biashara kwa lengo la kuwainua kiuchumi wajasiriamali wadogo.

“Halmashauri inapotoa mikopo kwa makundi maalumu ya vijana, kina mama na walemavu inatarajia kuona wanaitumia kama mbegu watakayoipanda iwasaidie kupiga hatua kwenye biashara zao hivyo watakaobahatika kuipata waitumie kama ilivyotarajiwa ili wapate faida warejeshe wakopeshwe tena na tena na wengine.”

"Wananchi waelewe mikopo hii ni lazima irejeshwe, hizi ni pesa za umma zimefanyiwa tathimini na ukaguzi na zinatakiwa kurejeshwa, sasa unapotumia mkopo kulipa ada au kufanya sherehe unajiweka matatizoni kwani tumeshapitisha bungeni sheria itakayowatia hatiani wote watakaoshindwa kurejesha mikopo," alisema Kanyasu.

Ofisa Maendeleo ya Vijana wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Zengo Pole alisema kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021 wametoa takribani Sh milioni 547 kama mikopo, ambapo kwa awamu ya kwanza walitoa Sh milioni 233 kwa vikundi vya vijana 31, vikundi vya kina mama 16 na kikundi cha walemavu kimoja.

Alisema kwa awamu ya pili wanatarajia kutoa mikopo ya takribani Sh milioni 314 kwa vikundi vya wanawake 41, vikundi vya vijana 24 na vikundi viwili vya walemavu.

Alisema marejesho bado ni changamoto kwani kwa robo ya kwanza yalikuwa chini ya Sh milioni 200.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Geita, Mwinyikheri Baraza aliipongeza halmashauri hiyo kwa kutenga asilimia 10 kwa ajili ya mikopo ya makundi maalumu na kuwataka wote watakaopata wasiitumie kufanya starehe badala yake wafanye uwekezaji.

Diwani wa Kata ya Kalangalala (CCM), Prudence Temba aliiomba halmashauri hiyo kutoa elimu ya uainishaji wa miradi kwa wanufaika wote wa mikopo hiyo ili kabla ya kukopeshwa wafahamu wanaenda kuifanyia nini na kuepuka kuitumia kwa matumizi yasiyokusudiwa.
 

ngakotecture

JF-Expert Member
Dec 30, 2014
1,650
2,000
Hivi wakuu wa wazoefu wa izi pesa za halmashauri mtu au kikundi wanachukuliwa hatua gani wasipozirudisha msaada tafadhari maana nina wasiwasi.
 

Deceiver

JF-Expert Member
Apr 19, 2018
5,263
2,000
Mkopo wangu au wake?
Geita kukoje huko?
Mara mkurugenzi anunue gari ya Bei mbaya. Mara waziri aseme utajengwa uwanja wa mpira Kama kivutio Cha utalii; Mara waziri wa China atoe msaada wa $50k.
Mara Geita wanavua asilimia kumi ya samaki wanaovuliwa ziwa Victoria. Nataka na Mimi nikaishi huko. Mabasi ya kwenda huko Ni yepi??
 

Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
8,565
2,000
Najiuliza ni biashara gani, vikundi vyote hivi itafanya bila ya kuigiliziana na wateja watatoka wapi? Bila ya mipango madhubuti, nia njema itaishia kuwa hasara kwa serikali na wananchi.
 

Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
8,565
2,000
Geita kukoje huko?
Mara mkurugenzi anunue gari ya Bei mbaya. Mara waziri aseme utajengwa uwanja wa mpira Kama kivutio Cha utalii; Mara waziri wa China atoe msaada wa $50k.
Mara Geita wanavua asilimia kumi ya samaki wanaovuliwa ziwa Victoria. Nataka na Mimi nikaishi huko. Mabasi ya kwenda huko Ni yepi??
Huko ni ndege tu!
 

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
38,066
2,000
Mkuu ukifika usisahau mrejesho nami niungane nawe katika safari hiyo.
Geita kukoje huko?
Mara mkurugenzi anunue gari ya Bei mbaya. Mara waziri aseme utajengwa uwanja wa mpira Kama kivutio Cha utalii; Mara waziri wa China atoe msaada wa $50k.
Mara Geita wanavua asilimia kumi ya samaki wanaovuliwa ziwa Victoria. Nataka na Mimi nikaishi huko. Mabasi ya kwenda huko Ni yepi??
 

SACO

JF-Expert Member
Jul 25, 2011
1,284
2,000
Halmashauri yenye watumishi zaidi ya 2500 mmewakopesha 30, halafu mnakuja kubweka hadharani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom