Mbunge wa Geita Mjini anatia mashaka. Anataka kusema Musukuma ni muongo?

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,087
6,568
Nimemsikiliza mbunge wa Geita mjini ndugu Costantine Kanyasu kwa kweli anashangaza sana. Nini kimemfanya akurupuke kuanza kutoa maoni kama haya kabla ya uchunguzi?

Nilimsikiliza waziri Jaffo alipopewa kazi yake ya kwanza kuunda tume kuchunguza ubadhilifu halimashauri ya Geita,alisema pesa mil 400 zilizotumika hazikupitishwa na baraza la madiwani.

Nashangaa nimemsikiliza mbunge wa Geita anaongea na media na kudai kuwa amepitia document hapo halmashauri na amebaini kuwa pesa hizo zilipitishwa na baraza la madiwani,pia anasisitiza Gpsa walitumiwa kununua hilo gari la mil 400,kwa hiyo taratibu zote zilifuatwa maana Gpsa ndie wakala wa manunuzi wa serikali.

Mbali na hayo anasema mkurugenzi aliyesimamishwa ni muadilifu na amekuwa akipambana na ufisadi kwa muda mrefu. Je ina maana Mbunge wa Geita vijijini ni muongo? Anaropoka hovyo na kumdanganya rais,maana huyu ndie aliyemlipua mkurugenzi kuwa alifanya ubadhirifu wa mil 400.
 
Hawa wasukuma Bwana Naona wanashida vichwani mwai.Infact ulimsikiliza yule mkurugenzi inaonekana taratibu zote zilifuatwa Kama mpaka ofisi ya waziri mkuu ilitia nataka then Naona yule mkurugenzi Hana kosa na ninachokiona Hapo kuna hidden agenda.Mgao.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Inatia mashaka,je huyu anayemtetea mkurugenzi alipata mgao?
 
Mkurugenzi hajatendewa haki. Kama kweli wanamaanisha kupambana na uzembe wa kwanza kuondolewa alipaswa kuwa Majaliwa akifuatiwa na Jaffo.

Ofisi zao ndizo zilizobariki manunuzi ya gari hilo.
Pia Tamesa.kwa nn wao hawaguswi wakati wao ndo huthibitisha ubora wa magari. Kama wanataka haki itendeke waanze na madiwani,kamati ya fedha na manunuzi,temesa na ofisi ya waziri mkuu.
 
Hawa wasukuma Bwana Naona wanashida vichwani mwai.Infact ulimsikiliza yule mkurugenzi inaonekana taratibu zote zilifuatwa Kama mpaka ofisi ya waziri mkuu ilitia nataka then Naona yule mkurugenzi Hana kosa na ninachokiona Hapo kuna hidden agenda.Mgao.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Inawezekana taratibu zilifutwa tu Kama mfumo,lakini nyuma ya pazia lilikua chezo,Sasa limegundulika!!
 
Back
Top Bottom