Mbunge wa Gairo, ataja sababu za ukata wa fedha mitaani

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,113
7,688
Mbunge wa Jimbo la Gairo Shabiby akiwa anatoa maoni yake Bungeni, amesema sababu ya ukata wa fedha mitaani umesababishwa na Serikali kuto kuongeza mishahara ya watumishi wa umma kwa miaka mingi hivyo kupelekea mzunguko wa fedha kuwa mdogo.

Amesisitiza kuwa mzunguko mkubwa wa fedha ktk jamii husababishwa na watumishi wa umma kwani ndio watumiaji wazuri wa fedha ktk manunuzi mbalimbali lkn pia ndio wmetapakaa nchi nzima.

Amesisitiza kuwa kuelekeza fedha nyingi kwenye miradi pekee kamwe haiwezi kubadilisha maisha ya watanzania zaidi ya kuongeza mishahara ya watumishi.

Hoja nyepesi sana hiyo naona wanajipigia upatu watumishi eti ndiyo wengi na wanafanya manunuzi sana
tapatalk_-1401561280.jpg
 
CCM wanatuchanganya sana Mara uchumi umefunguka, pesa mtaani zipo, TRA wamevunja record mara faida kwenye Bank zimeongeza.
Ukweli mtaani pesa hakuna kabisa
Kazi iendelee
Wanakauliza zao UVCCM “Alipo Mama vijana tupo “

Kauli mbaya sana kwenye ulimwengu wa Roho.
 
Kiukweli mtaani bado hakujachangamka kabisa. Ni jambo tu la kumshukuru Mungu walau baadhi tunaishi maisha ya uchumi wa kati! Ila walio wengi wanateseka aisee.
 
CCM wanatuchanganya sana Mara uchumi umefunguka, pesa mtaani zipo, TRA wamevunja record mara faida kwenye Bank zimeongeza.
Ukweli mtaani pesa hakuna kabisa
Kazi iendelee
Wanakauliza zao UVCCM “Alipo Mama vijana tupo “

Kauli mbaya sana kwenye ulimwengu wa Roho.

Aisee....mimi mwenyewe hata sielewi. Sielewi hata nani Waziri Mkuu kati ya Shaka/Chongolo na Kassim Majaliwa!
 
Rais wetu Samia anapambana kwa dhati kabisa kuhakikisha maisha ya watanzania wote ina boreka vyema.
wasaidizi wake wamsaidie kwa dhati waache unafiki wawe wakweli.
 
Sio kweli.
Pesa kuwa nyingi mtaani maana yake Serikali haina hela, mwenye hela ni mfanya biashara.
Mfanyabiashara kuwa na hela maana yake biashara hewa, magendo, rushwa, uhujumu uchumi, hongo za hovyohovyo zinazonunua haki za watu, hasa wale masikini
Pesa kuwa nyingi mtaani maana yake ni kwamba mfanyakazi ndiye anayeumia sana hasa wa zile sector ambazo hazizalishi, mfano: walimu, madaktari, vyombo vya usalama, nk
Hivyo, ukiona pesa sio nyingi mtaani maana yake ni kwamba Serikali iliyopo ni makini sana katika kudhibiti mapato na matumizi, na hivyo basi Hazina inakuwa imefurika mapesa mpaka yanamwagika sakafuni
 
Mfumko wa bei unaenda kulizika taifa hili, ukosefu wa mvua na njaa unaenda kutuweka pabaya sana mwakani.
Waachie pesa, na wapunguze kodi na tozo kwa wazalishaji then mambo yatakuwa sawa kwa wanyonge
Bro tangu nizaliwe safar hii ndo nimeushuhudia mfumuko wa bei daah bundle la bati za kawaida mwaka jana ilikua 290k sahivi kwenye baadhi ya mikoa inagonga had 420k kwa bundle moja vigae navyo havishikiki mafuta ni kila siku yanapanda alaf kwa wale waajiriwa mshahara bado uko palepale ni lazima maisha yawe magumu mtu akipata mshahara unaishia kwenye chakula tu hawez kugawana rizk na mafundi ujenzi, fundi nae akipata kazi anapunguza wasaidizi ili apate hela nzuri itakayo msogeza, maana kazi hamna, msaidizi wa fundi nae anakosa pakula hapo mzunguko unaenda hivyohivyo Hadi unamkuta kila mtu mwisho njaa na uhalifu unajaa mitaani
 
CCM wanatuchanganya sana Mara uchumi umefunguka, pesa mtaani zipo, TRA wamevunja record mara faida kwenye Bank zimeongeza.
Ukweli mtaani pesa hakuna kabisa
Kazi iendelee
Wanakauliza zao UVCCM “Alipo Mama vijana tupo “

Kauli mbaya sana kwenye ulimwengu wa Roho.
😂😂😂
 
Bro tangu nizaliwe safar hii ndo nimeushuhudia mfumuko wa bei daah bundle la bati za kawaida mwaka jana ilikua 290k sahivi kwenye baadhi ya mikoa inagonga had 420k kwa bundle moja vigae navyo havishikiki mafuta ni kila siku yanapanda alaf kwa wale waajiriwa mshahara bado uko palepale ni lazima maisha yawe magumu mtu akipata mshahara unaishia kwenye chakula tu hawez kugawana rizk na mafundi ujenzi, fundi nae akipata kazi anapunguza wasaidizi ili apate hela nzuri itakayo msogeza, maana kazi hamna, msaidizi wa fundi nae anakosa pakula hapo mzunguko unaenda hivyohivyo Hadi unamkuta kila mtu mwisho njaa na uhalifu unajaa mitaani
Hali ni mbaya sana kwa kweli haijawahi tokea. Hata vitu vidogo vidogo vya shilingi hamsini hadi mia moja vinapanda kwa asilimia 💯. Vifaa vya ujenzi ndio usiseme.
Wiki jana nilinunua simenti ya nyati 42.5 R kwa 19,500/-, leo nimeeda naambiwa shilingi 23,000 nikasema masikini atabaki kuwa masikini na hatajenga kabisa nchi hii. Wapangishaji wa nyumba na wa moto kweli tangu kuja kwa tozo ile kupitia luku sasa hapa asiyenacho ataendelea kutokuwa nacho tu.
Nchi hii imekuwa ngumu sana kwa mfumko wa bei tulio nao sasa hivi.
 
Back
Top Bottom