Mbunge wa Dodoma Mjini, Mavunde akabidhi sare kwa kituo cha madereva taksi wa Uwanja wa Ndege Dodoma

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
664
829
Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe Mavunde Leo amekabidhi sare kwa kituo cha madereva taksi wa Uwanja wa Ndege Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuboresha huduma ya usafirishaji Jijini Dodoma.

"Nimekabidhi sare hizo leo kwa madereva taksi 30 zenye thamani ya Tsh 1,500,000 katika eneo la Uwanja wa Ndege kwa lengo la kuwafanya madereva hao kuwa nadhifu na kutambulisha kwa urahisi kwa wageni waingiao Dodoma kupitia Kiwanja hicho cha Ndege"

Ni dhahiri kwamba madereva taksi wa Uwanja wa Ndege mnapokea wageni kutoka maeneo mengi tofauti nchini na duniani,ni vyema wakawa na utambulisho mzuri kupitia sare na pia kuwa nadhifu muda wote ili wageni waingiao wapate sura halisi ya Dodoma kupitia wao.

Kwa kuwa Dodoma sasa ni makao makuu ya nchi,yatupasa kuboresha huduma hizi za usafiri kwa kuonesha utofauti na maeneo mengine kwa kuanzia kwenye unadhifu wa mavazi mpaka ukarimu kwa wageni wetu.

Mhe Mavunde amesema "Baada ya kumaliza suala hili la sare,najiandaa kuratibu semina kwa ajili ya mafunzo ya UKARIMU kwa watoa huduma mbalimbali katika Jiji la Dodoma ikiwemo ninyi wa sekta ya usafirishaji,lengo langu ni kuona huduma mbalimbali jijini Dodoma zinaenda na kasi ya ukuaji wa Jiji ma shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii"

Akishukuru kwa niaba ya madereva taksi wenzake, Mwenyekiti wa Chama cha Madereva Taksi-Uwanja wa Ndege Dodoma Ndg. Lotson Mushobozi Nkongo amenishukuru kwa kuwajali watoa huduma ya usafiri katika kituo cha Uwanja wa Ndege kwa sare nadhifu ambazo zitawatambulisha vyema kwa wageni na kuahidi kuitangaza vyema Dodoma na kutoa huduma bora kwa uaminifu na uadilifu mkubwa ili kulinda sifa ya Makao makuu Dodoma.

FB_IMG_1620241241641.jpg

FB_IMG_1620241247150.jpg
 
Mavunde, huyu akiwambunge badala ya kutoa Gari za Kubebea wagonjwa alitua gari ya kwenda kuzikia.
 
Apambane, maana Dodoma mjini haiongozwi na mbunge mmoja kwa vipindi viwili. Vile vimemo vya hayati vilimuokoa sana mwaka jana.
 
Back
Top Bottom