Mbunge wa CUF: Mbio za mwenge zifutwe

mgosani

JF-Expert Member
Dec 25, 2014
1,005
1,136
Mbunge wa Masoud Salim (CUF) wa jimbo la Mtambile znz ameishauri serikali wafute mbio za Mwenge na sherehe za madhimisho ya kitaifa yasiwepo na fedha zinazogharamia sherehe hizo zitengwe kwenye shughuli ya kupima Ardhi ili kubainisha matumizi bora na kuepusha migogoro inayosababisha uadui katika jamii. Mbunge Masoud aliyasema hayo jana wakati wa kujadili ripoti ya kamati iliyoundwa na Bunge kuchunguza migogoro hiyo.

Serikali itafute suluhisho la kudumu kuepusha migogoro hiyo ikibidi mabilioni fedha yanayopotea kwenye sherehe mbali mbali za kitaifa yaelekezwe kwenye kupima Ardhi
 
Hoja hii mzito kma ukiangalia kwa jicho la tatu...ni vyema hzi pesa zinazotumika bila kumnufaisha mwananchi bhasi zitumike ktk shughuli hzo za kijamii
 
kuna uzi unaendelea humu ndani ya jukwa kuwa serikali inasambaza kofia za kapelo za katiba pendekezwa zilizonunuliwa kwa gharama ya shillingi bilioni 122!
kwani hizi pesa zingetumika kuwalipa maafisa Ardhi kusudi watengeneze Mpango wa matumizi bora ya Ardhi kwa wakulima,wafugaji na wawekezaji migogoro ya Ardhi ikatatuliwa isingewezekana?
 
Back
Top Bottom