Mbunge wa CUF Magdalena Sakaya na viongozi waandamizi wa CUF wanyimwa dhamana mara ya pili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge wa CUF Magdalena Sakaya na viongozi waandamizi wa CUF wanyimwa dhamana mara ya pili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mtutuma, Jun 6, 2011.

 1. m

  mtutuma Member

  #1
  Jun 6, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MBUNGE WA CUF MAGDALENA SAKAYA, WAJUMBE WA BARAZA KUU CUF, OFISA WA HAKI ZA BINADAMU NA SHERIA NA VIONGOZI WAANDAMIZI WA WILAYA NA KATA WANYIMWA DHAMANA BAADA YA KUPEWA MASHARTI MAGUMU.
  Katika hali ya kushangaza leo asubuhi,
  Hakimu wa mahakama ya wilaya ya Urambo Mkoani Tabora Mhe. Bulugu amewanyima dhamana viongozi waandamizi wa CUF.
  Viongozi waliopandishwa kizimbani NA KUNYIMWA DHAMANA ni;
  1. Magdalena Sakaya – Mbunge wa Viti Maalum
  2. Wajumbe wa baraza kuu watatu – Mhe Yasin Mrotwa, Mhe Doyo Hassan na Bi. Zainab Nyumba.
  3. Hashim Bakari – Ofisa Haki za binadamu na sheria CUF Taifa,
  4. Amir Kirungi – Mgombea wa CUF katika jimbo la Urambo magharibi 2010,
  5. Viongozi waandamizi saba 7 wa kata na wilaya Mrisho Swedi, Singu Yustu, Changu Salum, Idd S Matola, Msafiri Alkado, Ukiwa Juma na Peter Charles.
  Kiongozi wa kwanza wa kwanza kupandishwa kizimbani alikuwa ni IDD S MATOLA katika kesi ya jinai namba 60/ 2011. Dhamana yake iliwekwa wazi na wadhamini walisimama kuanza taratibu. Hakimu Bulugu alimtaka mwendesha mashtaka athibitishe hati za dhamana na mwendesha mashtaka alijiridhisha na kumjulisha hivyo hakimu. Hakimu Bulugu naye aliziomba na alipoziona aliweka pingamizi kuwa hati husika hazijapitia kwa mtendaji wa kata kwa uthibitisho.
  Hali hiyo iliua sintofahamu na ilimbidi wakili wa mshtakiwa Mhe Twaha Taslima aingilie kati na kumtaka hakimu aziruhusu hati hizo kwani zimethibitishwa na mtendaji wa kijiji ambaye mahakama zote zinamtambua.
  Hakimu Bulugu akijibu hoja ya Mhe. Twaha Taslima alieleza kuwa mahakama yake imejiwekea utaratibu huo na ni lazima ufuatwe, hata pale wakili wa mtuhumiwa alipozidi kutoa utetezi kuwa dhamana kwa makosa ya kawaida hutumika hati za dhamana kutoka kwa mtendaji wa kijiji na siyo lazima kata- hakimu Bulugu alikataa katakata na kudai utaratibu wa kupokea barua za utambulisha kutoka kwa mtendaji wa kata ndio utakaoutumika japo alikiri kuwa umeanza hivi karibuni kwatika mahakama yake na kuwa wananchi watauzoea.
  Ilipoitwa kesi ya jinai namba 57/2011 ambayo washtakiwa ni Mhe Sakaya na wenzake 11 isipokuwa IDD S. MATOLA washtakiwa wote 11 walipanda kizimbani.
  Mwendesha mashtaka alieleza hana pingamizi na dhamana kwa kuwa hali ya Kata ya Usinge ambako vurugu zilitokea na viongozi hao kuhusishwa kwa sasa pako shwari lakini mwendesha mashtaka akaweka pingamizi kuwa ni muhimu mahakama izuie watuhumiwa wote wanaotoka nje ya Usinge wasiende usinge kwa Shughuli zozote hadi kesi itakapoisha.
  Wakili wa watuhumiwa wote 12 Mhe Twaha Taslima aliiomba mahakama itupilie mbali ombi la upande wa mashtaka la kuwazuia wateja wake wanaotoka nje ya Using e wasifike Usinge kwa sababu –;
  1. Mahakama haina uwezo wa kuzuia watu wasitembee maeneo kadhaa ndani ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
  2. Pili baadhi ya washtakiwa wanaotoka nje ya Usinge wana shughuli za kijamii wanazozifanya katika maeneo hayo kwani ni viongozi na lazima waendelee na shughuli za kijamii, kisiasa na kimaendeleo mahali kokote.
  Hakimu Bulugu alitumia dakika 12 kupitia vifungu vya sheria na kisha akatoa uamuzi kuwa washtakiwa hawawezi kuzuiwa kwenda Usinge siku zote bali wale wanaotoka nje ya Usinge hawataruhusiwa kukanyaga huko hadi siku 7 zipite na ikiwa pana ulazima wa kufanya hivyo itampasa mhusika akaombe barua kutoka kwa OCD.
  Baada ya kutoa uamuzi huo hakimu Bulugu alitoa uamuzi wa dhamana na kudai dhamana kwa watuhumiwa itakuwa na masharti yafuatayo kwa pamoja;
  1. Watuhumiwa watapaswa kujidhamini kwa barua zenye commitment ya TZS 3,000,000/- .
  2. Kila mtuhumiwa atadhaminiwa na mdhamini mmoja ANAYEISHI ndani ya wilaya ya Urambo mwenye hati ya nyumba ya thamani ya TZS 3,000,000/- au atakayewasilisha mahakamani shilingi 3,000,000/- taslimu.
  3. Kila mtuhumiwa lazima awe na barua ya utambulisho kutoka kwa mtendaji wa kijiji iliyothibitishwa na kata na siyo kijiji ambayo haijathibitishwa na kata kama ilivyozoeleka.
  Baada ya kutoa masharti hayo magumu, wakili wa washtakiwa Mhe Twaha Taslima aliiomba mahakama ilitizame suala hilo kwa upana kwani sharti la kutaka hati ya utambulisho iliyothibitishwa na mtendaji wa kata ni suala geni na linafanyika kwa kesi ya kina Sakaya tu.
  Hakimu Bulugu alibakia na msimamo huo wa mahakama na akaiahirisha kesi hiyo hadi 15 Juni 2011 ambapo watuhumiwa hao watarudishwa.
  Hii ina maana kuwa mhe Sakaya na viongozi waandamizi wa CUF watakaa gerezani kwa siku 9 zaidi na hii itakamilisha siku 20 za kukaa gerezani kwa kunyimwa dhamana.
  Hata hivyo , wananchi kadhaa waliohojiwa na waandishi wa redio kadhaa zilizohudhuria mahakamani walisema kuwa hadi ijumaa iliyopita watu walidhaminiwa kwa barua za kutoka kwa watendaji wa vijiji tu na walishangazwa na utaratibu mpya ulioanza katika kesi ya kina Sakaya na kuwakosesha dhamana.
  Alipokuwa akihojiwa nje ya mahakama hiyo Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara Mhe Julius Mtatiro alikiri kushangazwa na uamuzi huo wa mahakama na akasema hawezi kuingilia sana suala hilo kwa undani na kuwa kazi yake kama Naibu Katibu Mkuu kwa sasa ni kuhakikisha kuwa masharti hayo magumu yaliyotolewa na mahakama yanatafutiwa ufumbuzi.
  Wakili wa washtakiwa MHE TWAHA TASLIMA amesema anaanzisha utaratibu kuhakikisha viongozi hao wanapata dhamana haraka iwezekanavyo kabla ya terehe 15 Mei 2011.

  Hii ni mara ya pili kwa mhe Sakaya na wenzie kunyimwa dhamana katika kesi hiyo kwani tarehe 30 Mei 2011 walipandishwa kizimbani katika mahakama ya Urambo na hakimu Bulugu aliwanyima dhamana baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha hati ya pingamizi ya dhamana kwa mahakama kwa madai kuwa washtakiwa wakiachiwa watahatarisha amani ya wananchi wengine.
  Mhe Sakaya na viongozi waandamizi wa CUF walikamatwa tarehe 28 Mei 2011 katika kata ya Usinge wilaya ya Urambo baada ya polisi kuua kijana mmoja kwa risasi na kujeruhi wengine katika rapsha iliyoanzishwa na polisi kwa wananchi waliokuwa wanatawanyika kurudi majumbani walipokuwa wakimsikiliza mhe Sakaya na Ujumbe wake ambao walikwenda katika kijiji hicho kutatua matatizo ya wafugaji kunyang’anywa mifugo yao na askari wa maliasili na polisi.
  Mtatiro alibainisha kuwa akifika Dar Es Saalam atawaeleza watanzania juu ya Ukatili usiomithilika unaofanya na vyombo vya dola kwa wananchi walio katika vijiji vinavyopakana na hifandhi ndani ya wilaya ya Urambo.
  Taarifa hii imeandikwa na;
  Mohammed Mtutuma.
  Msaidizi Maalum wa Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara (CUF).
  Urambo.
   
 2. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,823
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  CCM inaitumia mahakama kama sehemu yake ya kufanyia sanaa..hii ni aibu kwa mahakama ambayo haina maono mazuri ya kiutendaji.
   
 3. f

  few b Member

  #3
  Jun 6, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 72
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 15
  hakuna haja ya kuanza kulalamika jamani sisi tunasubiri tupewe "route" ya mtiti alio utangaza jana mh. Lipumba coz nimesha ona nchi hii bila nguvu ya uma mambo hayaendi kabisa!! Ni tarehe 12 wadau...
   
 4. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Duh poleni sana wana CUF, inasikitisha.
   
 5. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  wanachama wake si waandamane?
   
 6. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  No bail,kwa kesi gani hatari au mazingira hatarishi?...mzee Lipumba tabora pale si kwenu? Hebu nenda fasta kama ulivoenda central jana kwa kofia ya kituo cha demokrasia,go and shout to this people...hakimu si mungu bana,wana mapungufu pia kama binadamu
   
 7. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Inaumiza sana kusikia habari hii.
  Wezi wa EPA wako nje kwa dhamana
  wakina mgonja wapo nje
  watuhumiwa wa kumuua chegeni wapo nje
  viongozi wa CDM wapo nje
  why this lady sakaya na wenzie?
  Nawaheshimu sana wanatarime maana wangeshaenda kufungua milango..hebu waheshimiwa muwe na fair decision,mmesahau waliowagandamiza katika muswada wa sheria za mahakama ni fellow MPs from ruling party???
   
 8. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #8
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Huyo hakimu inafaa achunguzwe na au mtoa habari kama ni habari za kweli au walishindwa masharti mengine ya dhamana. Si vyema kuihusisha mahakama na CCM. Kama hakimu ana mapungufu basi huyo hakimu hatoungwa mkono na CCM. Na kama mwandishi wa hii habari ndio ana mapungufu nae pia achunguzwe.
   
 9. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,268
  Trophy Points: 280
  Mwanazuoni wa kiislamu sheikh Mataka leo ametutaka tusiingilie mambo ya mahakama, tuache sheria ifuate mkondo wake, kwa sababu ni msomi sana huyu sheikh basi tumsikilize.
   
 10. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #10
  Jun 6, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,948
  Likes Received: 1,274
  Trophy Points: 280
  MI NADHANI WEWE NDO UJICHUNGUZE. Cheki jina la aliyetuma na username
   
 11. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Kaka Matola usomi upi? Wa ilimu duniya ama nyota? Maana isije kuwa amerithi mwembechai
   
 12. M

  Mmongolilomo Senior Member

  #12
  Jun 6, 2011
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Inauma sana kila sehemu CCMagamba ipo. Haki za watu hivihivi, jamani mkuu wa bunge yuko wapi ktk kutetea uhuru wa himaya yake.
   
 13. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #13
  Jun 6, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Katika mambo ambayo huwa nawashangaa watanzania, basi ni pamoja na kujenga imani kwa jeshi la polisi na mahakama. Tanzania tuna jeshi la CCM na mahakama ya kutetea haki za CCM na za Matajiri. Mahakimu wanafanya kazi kutokana na maagizo ya CCM na hawana ubavu wowote wa kutoa maamuzi kulingana na vifungu vya sheria. Just recall back kifungo cha maisha cha Babu Seya na kuachiliwa kwa ditopile na Zombe, tena fikiria kwa karibu namna ambavyo mafisadi wanawekewa mashariti rahis ya dhamana huku viongozi wa upinzani ama wakinyimwa dhamana au kuwekewa mashariti magumu yasiyotekelezeka kwa makusudi kabisa. Ni siku nyingi sana mimi nilishapoteza imani na mahakama pamoja na Jeshi la polisi. Hawa wote ni wahuni tu. Tunatakiwa tufikirie kuunda chombo kingine cha kutetea haki za wanyonge out of jeshi la CCM na mahakama ya CCM. Kama mtu anataka kunidhulumu shilingi mia mbili bora nimwachie kuliko kwenda mahakamani nikatumie mia tano halafu na miambili isirudi.
   
 14. R

  Ray Isly Member

  #14
  Jun 6, 2011
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndo mana wanawekwa ndani kwa kashfa zenu hizi!kuikomboa hii nchi itakua kaz sana.MANA MNADHARAU WATU NINYI.DAH 2TAONA MWISHO WA HAYA. Ninyi Mapadre.NGOJENI MUONE WATAKAO IKOMBOA HII NCHI MUDA CO MWINGI SANA.
   
 15. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #15
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  tena haki za mbunge mwanamke mwenzie na wengineo
   
 16. N

  NDOFU JF-Expert Member

  #16
  Jun 6, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 656
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ccm wanakupa nin wewe dada? Mbona unakosa utu kwa kiwango hicho?! Inamaana ukiwa ccm hauwezi kuona mabaya ya upande wako? Haya bana kazi kwako cku mambo yakiwa mabaya.
   
 17. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #17
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Haaaaa haaaa! Ulikuwa unashangilia Mbowe alipokamatwa! Pole sana, umesahau kwamba CCM inajali mafisadi zaidi kuliko wananchi walalahoi! Wananchi wa Nyamongo wameonja machungu ya umaskini wao kwa sababu ya kuwalinda mafisadi wanaokazana kukwapua raslimali zetu huko mgodini North Mara na kutuachia urithi wa mashimo! Kama unategemea kuwa CCM na dola iliyo chini yake watabadilika ukapate kikombe cha babu wa Loliondo!
   
 18. U

  Unstoppable JF-Expert Member

  #18
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mmh! Naona Mtatiro anabeba mzigo wote; where is Hamad Rashid? Angekua mtu muhimu kufuatilia hii kesi kuhakikishwa mbunge wetu Magdalena anaachiwa/anapewa dhamana. As far as I know Hamad hana majukumu makubwa tena bungeni, huu ndio wakati wakuonyesha uzalendo wakujituma. Mshikamano ni muhimu sana ili mbunge Sakaya asijisikie hana support. Mimi sielewi wanavyosema akiachiliwa/pewa dhama ni hatari kwa jamii?
   
 19. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #19
  Jun 6, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Shameful
   
 20. Du Bois ideas

  Du Bois ideas JF-Expert Member

  #20
  Jun 7, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 428
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Angekuwa CDM angekuwa ametoka. Kwa nini CUF wasiwaite CDM kwenda kusaidia waone kazi ya Nyaucho Marando?
   
Loading...