Mbunge wa CUF aangua kilio!

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
na Neema Kishebuka, Tanga

MBUNGE wa Viti Maalumu, Amina Mwindau (CUF), amemwaga machozi, baada ya kuelezwa changamoto zinazowakabili watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Ansaar Muslim Youth Center kilichoko Makorora, jijini hapa.

Mbunge huyo aliyeambatana na viongozi mbalimbali wa chama hicho, alitoa machozi hayo jana baada ya kusomewa historia fupi na changamoto zinazowakabili yatima hao wapatao 65 ambao wana umri chini ya miaka 15.

Akisoma taarifa ya watoto hao, Sheikh Hassan Waziri ambaye ndiye mlezi wao, alisema wanakabiliwa na uhaba wa chakula kwani wahisani wengi wamejitoa na kuwaacha watoto hao wakitegemea msaada pekee toka kwa mtu mmoja wa hapa jijini na wachache kama wageni wanaofika kituoni hapa mara moja moja.

“Hata ninapotaka kurudi kwetu kutokana na taasisi kulegalega, lakini najifikiria nitafanya nini na ninabaki na kidonda rohoni nitawaacha na nani watoto hawa hapa?” alisema mlezi huo ambaye kabla hajamaliza alianza kulia kwa uchungu huku akifuatiwa na watoto hao.

Kilio hicho ndicho kilichosababisha Mwindau naye kuangua kilio huku akifuatiwa na wanachama wenzake alioongozana nao.

Awali akisoma taarifa ya kituo hicho, Sheik Hassan alisema watu wengi wamewafanya watoto yatima kama miradi na pia wengine wanawachukua watoto wa mitaani na kusema kuwa ni yatima huku wakipatiwa misaada wakati yatima wa kweli wakibaki wanateseka.

Alisema watoto hao ambao wengi wanasoma wanakabiliwa na ukosefu wa chakula, ada za shule pamoja na sare za shule na kuwataka watu waliojaaliwa kujitoa kuwasaidia watoto hao.

Kwa upande wake, mbunge huyo wa CUF aliiomba jamii kujenga utamaduni wa kuwatembelea watoto yatima hasa katika nyakati za sikukuu ili na wao wajione kama watoto wengine wasijisikie upweke.
 
Neema Kishebuka wa Tanga, kama unaingia humu JF, naomba unipatie anuani za hiyo tasisi niwasiliane na viongozi wake, wanipe japo wawili, mimi nnahamu ya kulea, wanangu washa kuwa wakubwa na wanajitegemea.

Au mwengine yeyote mwenye anuani yao anipatie.
 
usisubiri kupewa anuani, kama kweli umeguswa na hali hiyo safiri nenda Tanga katoe msaada kwa watoto hao acha kujipa umaarufu hapa
 
usisubiri kupewa anuani, kama kweli umeguswa na hali hiyo safiri nenda Tanga katoe msaada kwa watoto hao acha kujipa umaarufu hapa

Wazo zuri, naelekea Tanga leo hii. Ningetaka umaarufu ningekuja na jina langu kamili humu JF.
 
usisubiri kupewa anuani, kama kweli umeguswa na hali hiyo safiri nenda Tanga katoe msaada kwa watoto hao acha kujipa umaarufu hapa

Tanga mbona mbali, kama yupo Dar apite tu barabara yeyote ile atakutana na watoto wenye hali ngumu ya kimaisha awachukue awalelee.
 
Tanga mbona mbali, kama yupo Dar apite tu barabara yeyote ile atakutana na watoto wenye hali ngumu ya kimaisha awachukue awalelee.

Dar nimeshachukuwa wawili wakiwa mmoja ana mwaka mmoja na nusu na mwingine miaka 10.

Wale unaowaona barabarani wakiomba omba, ukitazama vizuri pembeni utaona wazee wao wapo hapo, wanawatumia tu hawa watoto kama chambo cha kujiongezea kipato.
 
Aisee kumbe wanatumika kama mtaji tu.
Kuanzia leo ntakuwa najifikiria mara mbili mbili kuwasaidia wale watoto.
 
Neema Kishebuka wa Tanga, kama unaingia humu JF, naomba unipatie anuani za hiyo tasisi niwasiliane na viongozi wake, wanipe japo wawili, mimi nnahamu ya kulea, wanangu washa kuwa wakubwa na wanajitegemea.

Au mwengine yeyote mwenye anuani yao anipatie.

Mkuu mbona tatizo hili lipo hapa nchini kwetu miaka mingi sana!wewe ulikuwa ulijui?au ndiyo limekugusa sana baada ya huyu mbunge wa CUF kuangua kilio?
 
"Kwa upande wake, mbunge huyo wa CUF aliiomba jamii kujenga utamaduni wa kuwatembelea watoto yatima hasa katika nyakati za sikukuu ili na wao wajione kama watoto wengine wasijisikie upweke."

Hivi kwanini kuwasaidia yatima "haswa nyakati za sikukuu"????!! Hizo siku nyingine kweli huwa hawajisikii upweke???... "Silaha ya mnafiki..... ni machozi yake mweneyewe...."
 
Back
Top Bottom