Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,182
na Neema Kishebuka, Tanga
MBUNGE wa Viti Maalumu, Amina Mwindau (CUF), amemwaga machozi, baada ya kuelezwa changamoto zinazowakabili watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Ansaar Muslim Youth Center kilichoko Makorora, jijini hapa.
Mbunge huyo aliyeambatana na viongozi mbalimbali wa chama hicho, alitoa machozi hayo jana baada ya kusomewa historia fupi na changamoto zinazowakabili yatima hao wapatao 65 ambao wana umri chini ya miaka 15.
Akisoma taarifa ya watoto hao, Sheikh Hassan Waziri ambaye ndiye mlezi wao, alisema wanakabiliwa na uhaba wa chakula kwani wahisani wengi wamejitoa na kuwaacha watoto hao wakitegemea msaada pekee toka kwa mtu mmoja wa hapa jijini na wachache kama wageni wanaofika kituoni hapa mara moja moja.
Hata ninapotaka kurudi kwetu kutokana na taasisi kulegalega, lakini najifikiria nitafanya nini na ninabaki na kidonda rohoni nitawaacha na nani watoto hawa hapa? alisema mlezi huo ambaye kabla hajamaliza alianza kulia kwa uchungu huku akifuatiwa na watoto hao.
Kilio hicho ndicho kilichosababisha Mwindau naye kuangua kilio huku akifuatiwa na wanachama wenzake alioongozana nao.
Awali akisoma taarifa ya kituo hicho, Sheik Hassan alisema watu wengi wamewafanya watoto yatima kama miradi na pia wengine wanawachukua watoto wa mitaani na kusema kuwa ni yatima huku wakipatiwa misaada wakati yatima wa kweli wakibaki wanateseka.
Alisema watoto hao ambao wengi wanasoma wanakabiliwa na ukosefu wa chakula, ada za shule pamoja na sare za shule na kuwataka watu waliojaaliwa kujitoa kuwasaidia watoto hao.
Kwa upande wake, mbunge huyo wa CUF aliiomba jamii kujenga utamaduni wa kuwatembelea watoto yatima hasa katika nyakati za sikukuu ili na wao wajione kama watoto wengine wasijisikie upweke.