Mbunge wa CHADEMA: Rais ashtakiwe kwa ahadi hewa

assadsyria3

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
6,904
4,050
Dodoma. Mbunge wa Viti Maalumu Suzana Lyimo ,ameitaka Serikali kuwapeleka mahakamani marais wanaoshindwa kutimiza ahadi zao hadi wanastaafu.

Lyimo alitoa pendekezo hilo jana bungeni alipouliza swali la nyongeza kuhusu ahadi za Rais Jakaya Kikwete ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wabunge wengi kutoka Chama Cha Mapinduzi.

“Mheshimiwa Spika, wabunge wengi wamekuwa wakilalamikia juu ya ahadi za Rais kila mahali na hasa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi, je inakuwaje Rais anaposhindwa kutimiza ahadi zake na wakati mwingine hadi anamaliza kipindi chake cha uongozi ni kwa nini asishtakiwe mahakamani kwa uongo,” alihoji Lyimo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi alisema kuwa hakuna tatizo kwa Rais kutotimiza ahadi zake kwani anapomaliza muda wake Rais anayemrithi huwa anatimiza ahadi hizo kwani ni ahadi za Rais sio anatoa fedha mfukoni mwake.

Awali katika swali la msingi Mbunge wa Mkinga Dustan Kitandula (CCM), alitaka kujua ni hatua zipi zimechukuliwa ili kutimiza ahadi ya Rais juu ya kujenga kwa haraka Hospitali ya Wilaya ya Mkinga.

Pia alihoji kuhusu kupandishwa hadhi Kituo cha Maramba.
 
Inamaana kama kikwete akiamua ifikapo 2014 akatoa ahadi lukuki na 2015 ikashinda cuf, chadema au nccr je wanapaswa kutimiza ahad hizo? Kama ndivyo kuna tatizo kwan anaweza fanya hayo kwa kukomoa ajaye, nashauri kama ni ahadi zinazotakiwa kuendelezwa ziwe zile ambazo zipo kwenye mipango ya maendeleo na kuidhinishwa na bunge,na si za kuropoka majukwaani.
 
Dah ! Sisi wa Mjini tuliahidiwa ' barabara za juu kwa juu ' aisee ! Sema mimi nilipomuangalia mkulu Machoni siku anaahidi hizi barabara za angani , nilijua hili ni CHANGA LA MACHO TU ! Zile kampeni zilimburuza sana Jk , kiasi cha kutumia ule mpango maarufu wa LIWALO NA LIWE , Yaani ni kuahidi hata vya uongo ili mradi siku zinasogea !
 
Inamaana kama kikwete akiamua ifikapo 2014 akatoa ahadi lukuki na 2015 ikashinda cuf, chadema au nccr je wanapaswa kutimiza ahad hizo? Kama ndivyo kuna tatizo kwan anaweza fanya hayo kwa kukomoa ajaye, nashauri kama ni ahadi zinazotakiwa kuendelezwa ziwe zile ambazo zipo kwenye mipango ya maendeleo na kuidhinishwa na bunge,na si za kuropoka majukwaani.

Lukuvi akiongea maneno 10 ,chukua moja tu !
 
Rais akiwa dhaifu hawezi kupokelewa upuuzi wake aloahidi na mrithi wake maana huwezi kurithi fuko la mavi la mtangulizi wako kisa alikuwa rais...Mtu kama jk anawa ahidi wapuuzi wenzie kwamba eti atajenga barabara juu na chini huu si ni upuuzi nadharau ya hali ya juu kwa wananchi
 
Mh. Lukuvi nae kiazi,sijui anadhani wananchi wa kawaida ni viazi kama yeye,kwanini haoni aibu kutoa hoja wakati uwezo wake wa kufikiri ni mdogo! bure kabisa
 
Ahadi za kisiasa Hukumu zake nizakisiasa vilevile.Hukumu inatakiwa iwe kwenye sanduku la Kura na sio Mahakamani.Tusichanganye Siasa na Taaluma.Hata akipelekwa Mahakamani atatoka kirahisi maana utetezi wake uko wazi kabisa.
 
Nawapenda sana CDM, lakini wabunge wake wengi wa viti maalum ni Mbumbumbu. Wapi duniani Rais alitimiza ahadi zake zote alizotoa wakati wa kampeni? Tuanze na Wabunge tuu, ni wangapi wametimiza ahadi zao?
 
Dodoma. Mbunge wa Viti Maalumu Suzana Lyimo ,ameitaka Serikali kuwapeleka mahakamani marais wanaoshindwa kutimiza ahadi zao hadi wanastaafu.

Lyimo alitoa pendekezo hilo jana bungeni alipouliza swali la nyongeza kuhusu ahadi za Rais Jakaya Kikwete ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wabunge wengi kutoka Chama Cha Mapinduzi.

"Mheshimiwa Spika, wabunge wengi wamekuwa wakilalamikia juu ya ahadi za Rais kila mahali na hasa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi, je inakuwaje Rais anaposhindwa kutimiza ahadi zake na wakati mwingine hadi anamaliza kipindi chake cha uongozi ni kwa nini asishtakiwe mahakamani kwa uongo," alihoji Lyimo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi alisema kuwa hakuna tatizo kwa Rais kutotimiza ahadi zake kwani anapomaliza muda wake Rais anayemrithi huwa anatimiza ahadi hizo kwani ni ahadi za Rais sio anatoa fedha mfukoni mwake.

Awali katika swali la msingi Mbunge wa Mkinga Dustan Kitandula (CCM), alitaka kujua ni hatua zipi zimechukuliwa ili kutimiza ahadi ya Rais juu ya kujenga kwa haraka Hospitali ya Wilaya ya Mkinga.

Pia alihoji kuhusu kupandishwa hadhi Kituo cha Maramba.
"LUKU-JIVI" asitudanganye hapa! yaani Dr Slaa aje atimize UTAPELI aliofanya MSANII aka dhaifu! NEVER! My president is a thinking president!! Siyo huyu kilaza!! bingwa wa "ngozi"
 
ametekeleza ahadi ambazo hakuahidi " NDUGU WANANCHI,ISHALAAA MWENYEZI MUNGU AKIPENDAA NTASAFIRI SAFIRI SANA NA SITAPATA MUDA WA KUKAA TANZANIA, LABDA KUWE NA MSIBA NIJE KUTOA POLE, SO NIPENI KULA (NO, NIMEKOSEA NAMAANISHA KURA).
 
nawapenda sana cdm, lakini wabunge wake wengi wa viti maalum ni mbumbumbu. Wapi duniani rais alitimiza ahadi zake zote alizotoa wakati wa kampeni? Tuanze na wabunge tuu, ni wangapi wametimiza ahadi zao?

wewe kweli mbumbu squire na mburula hujui kuwa kuhaidi kisichotekelezeka wakati wa kampeni ni utapeli na uhaini unastahili kufungwa ahadi zinazohadiwa pasipo uchaguzi ndio zipo kwenye fungu la kutokutekelezeka na zikapotezewa
 
Katiba:
hakuna mahakama itakayokuwa na uwezo wa kusikiliza shauri linalomkabili raisi kwa KUTENDA AMA KUKOSA KUTENDA JAMBO LOLOTE.
hapa ndo siri ilipo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom