Mbunge wa chadema iringa mjini atishiwa na mbunge viti maalum chadema(chiku abwao)

Nilidhani maelezo niliyoyatoa kwenye ile thread ya TUNTEMEKE yalikuwa yanajitosheleza lakini kumbe sikueleweka. Sasa nadhani kuna watu wana maslahi hasi dhidi ya CHADEMA kwenye suala hili. Kwenye Thread ile nilisema na bado nasimama hapo kwamba mimi si msemaji wa Kamati Kuu na kama Katibu wa CHADEMA Mko wa Iringa sijapewa taarifa rasmi kutoka Ofisi ya Katibu Mkuu kuhusu uteuzi wa Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa. Mwenye uwezo na mamlaka ya kulizungumzia hilo ni John Mnyika.

Kwa taarifa nilizo nazo sasa hivi ni kwamba Chiku bado yuko Dar es salaam na Msigwa tangu Juzi ameingia hapa mjini Iringa na saa hizi yuko kwenye siku ya wanahabari kwa taarifa nilizopewa. Kwa hiyo kusema hawa wabunge wetu wanatishiana na hali ya chama hapa Iringa si shwari ni Uzushi mwingine ambao sielewi lengo lake ni nini.

Tuko Imara wala hakuna mvurugano wowote ule na wote tunaohusika kwenye kuendesha chama hatutishiani wala kuchukiana. Ila naamini kuna kundi la watu wenye malengo ambayo mpaka ssasa sijui ni malengo gani ingawa naamni kwamba si malengo mazuri kwa CHADEMA na Mkoa wa Iringa.

Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Iringa

USIFICHE malazi kijana,Kwani hujui kuwa cc ya chadema ilipokutana juzi ililizungumzia hili la Chiku a
na Msigwa? au unataka kuasafisha nyota hapa........ukweli ni kwamba chiku na Msigwa wapo kwenye msuguano mkubwa sana ambao umeanzia kule kwenye uchaguzi wa mwenyekiti wa mkoa.Acha kupotosha watu ww unayejiita katibu wa chadema iringa.
 
Back
Top Bottom