The Stig
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 1,113
- 1,105
Mtazamo wangu ni kwa kiongozi yeyote awe wa kuchaguliwa si wa CCM wala CHADEMA na hata wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wa kupewa si afikiani nalo kabisa na natumai katiba mpya itabadilisha hizi nyadhifa za upendeleo.
Zaidi ya hayo, ningependa kuona Tanzania hata wale viongozi wanaoteuliwa na Rais, kama makatibu wakuu, majaji na wakurugenzi wa sehemu nyeti wawe pia wanapitishwa bungeni kuhakikiwa na kupitishwa pale tu bunge litaridhia.
Nachokukubali Faiza ni kuwa post zako unatumia lugha nyepesi na zisizo na mauzi ya kupitiliza. Kwamba sikubaliani na mtazamo wako mara nyingi haijalishi, huwa napenda kukusoma.
Lakini hii post ya leo, umenifurahisha sana. Hongera kwa kuzungumza kitu nachokubaliana nacho!
Ila isije ikawa ni kwa sababu tu Suzan Lyimo ni wa kuteuliwa ndiyo ukaamua kusema haupendi vitu maalum! Iwe kotekote.