Mbunge wa CCM, Mhe. Esta Bulaya, Afanya Tukio la Kishujaa Mjini Dodoma! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge wa CCM, Mhe. Esta Bulaya, Afanya Tukio la Kishujaa Mjini Dodoma!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Apr 22, 2012.

 1. P

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 22,180
  Likes Received: 10,223
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Katika pita pita yangu viunga fulani hapa mjini Dodoma, nimepita mahali nikukata baadhi ya watu na heshima zao, wakimsifu huyu mbunge kijana wa CCM, Mhe, Esta Bulaya, kuwa amefanya tukio la ushajaa mkubwa katika medani za siasa.

  Kwa jinsi nilivyosikia kuhusu alichokifanya mbunge huyu, naomba nikiache kwanza kama tetesi, na nikisha thibitisha, nitarejea kuwapatia ushujaa huo wa Mhe. Esta Bulaya!.

  Kwa kusaidia tuu, ni kuwa mbunge huyu, amefanya kitendo fulani cha kishujaa kwa kuweka mbele maslahi ya taifa ambapo amesimama kuhesabiwa miongini mwa wabunge wachache wa CCM wenye uchungu wa ukweli na umasikini wa nchi hii, kinyume cha wengi wa wabunge wa CCM ambao wameingia bungeni kwa drive ya njaa zao kutafuta maslahi binafsi badala ya maslahi ya taifa, hivyo wanachosimamia mule bungeni, ni matumbo yao tuu!.

  Natafuta uthibitisho wa huo ushujaa wa Mhe. Esta Bulaya, ili tuliingize rasmi jina lake miongoni mwa mashujaa wa taifa hili!.

  Tuvute subira kidogo!.

  Wasalaam.

  Pasco.

  Dodoma!.

  Kabla ya huo ushujaa, Mhe. Ester Bulaya aliripotiwa hivi humu jf

  [h=2]"Re: Godfrey Zambi na Ester Bulaya bungeni waitabiria CCM yao kuanguka mwaka 2015"[/h]

  Update 1. jana usiku:
  Hatimaye ninepata uthibitisho wa kitendo hicho cha kishujaa cha Mbunge wa CCM, Mhe. Ester Bulaya!.

  Licha ya kupata uthibitisho huo, bado kitendo chenyewe sikitaji kwanza mpaka nitakapo pata go ahead ya relevant authorities!.

  Sababu pekee ya kuleta hii thread ni kuwajulisha tuu kuwa pamoja na ukweli kuwa CCM imeoza kwa rushwa na ufusadi na wanaitafuna nchi hii kama mchwa, tena wanaiba waziwazi mchana kweupe kama shamba la bibi, ndani ya hao hao mijizi na mifisadi ya CCM, kuna vijana wachache wazuri ambao sio mafisadi na wako tayari kusimama kuhesabiwa!.

  Wengi wa wabunge wa CCM wameingia bungeni sio ili kuwatumikia wananchi, bali kujineenesha wao na matumbo yao hivyo mule mjengoni wao wako kutetea maslahi yao!, lakini miongoni mwao, wamo wachache walioingia mle kutetea maslahi ya taifa na Mhe. Ester Bulaya yuu mmoja wao!.

  Nitamalizia hivi punde na kitendo chenyewe cha ushujaa wa mbunge huyu!.

  Kwa wale wenye mcheche sana, samahani sana endeleeni kuvuta subra!. Good things hazihitaji haraka wala papara!.

  Sababu ya kupost kabla ya uthibitisho ni kuhakikisha wewe kama mwana jf, be the first to know!.

  Mfano news za Nundu kwenye TV zote leo na kwenye magazeti yote ya kesho, is not news anymore kwa sababu jf tumejua kila kitu tangu mchana!

  Asanteni tuhifunze zaidi "managing divesity"

  Pasco!.

  Update 2: Final Update

  Confirmed,

  Mhe. Ester Bulaya ndie mbunge mwanamke kijana na shujaa wa CCM aliyesaini petition ya Mhe. Zitto kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.

  Wabunge kutoka CCM jumla ni 6 wakiongozwa na shujaa Mhe. Deo Filikunjombe. Jee kwa nini Ester ndio anayestahili pongezi mpaka kumuita shujaa!.

  Kati ya wote waliosaini, wengine wote ni wabunge wa majimbo isipokuwa Ester yeye ni mbunge wa hisani wa CCM!. Kitendo cha kutoogopa hisani na kusimama kuhesabiwa ni kitendo cha ushujaa wa hali ya juu!.

  Wenzake wote waliosaini ni watu wenye shughuli zao nyingine, ubunge kwao ni utumishi tuu kwa wananchi, hivyo kwao lolote liwalo, if anything happens to them in CCM, they have nothing to loose and everthing to gain from CCM, lakini kwa Ester kwake CCM ndio baba CCM ndio mama, if anything happens to Ester huko CCM, she has everthing to loose and nothing to gain from CCM!.

  She has the guts to say no nonse!. Kuna wabunge wengi wa CCM akiwemo January ambao tuliwaona kama mashujaa, kitendo cha kutomuunga mkono Zitto ni uthibitisho tuu kuwa they are barking dogs only, seldom bite!. They don't have the guts to say no to nonsense!.

  Nawaombeni wanabodi wenzangu, mhesabuni Mhe. Ester Bulaya miongoni mwa mashujaa 76 wa taifa kwenye orodha ya Zitto na jina lake liingizwe kwenye list ya mashujaa ambao mwaka 2015 wata team up na timu ya ushindi kuelekea kwenye ukombozi wa pili wa taifa letu!.

  Kwa wale ambao mtatofautiana na mimi kwenye dhana ya ushujaa, naheshimu mitazamo yenu.

  Hongera sana Mhe. Ester Bulaya, CCM watakunyanyapaa, CCM watakutenga, Watanzania watasimama na wewe, na Mungu atakutangulia kunyoosha mapito yako!.

  Ubarikiwe Sana!.

  Pasco.
   
 2. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,078
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  kwanini usingesubiri uthibitisho kwanza,ulikua na haraka gani hasa au ulihisi kuna mtu atakuwahi ukaona uweke akiba ya maneno kabisa
   
 3. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,682
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Watu wenye heshima zenu hampaswi kufanya mambo ya kitoto Kama haya. Sasa ulochosema hapo ni nini?
   
 4. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 989
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 60
  Asante mkuu ngoja nisubiri uthibitisho,,,
   
 5. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,250
  Likes Received: 405
  Trophy Points: 180
  huyo ndo pasco bana, lazima awasifie magamba ata kama maji yashawafika shingoni, asubili m4c
   
 6. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,026
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  si useme kaweka sign kwenye kitabu cha zitto unaogopa nini sasa?
   
 7. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,219
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 160
  Kweli mkuu Kigogo, huyu Pasco ni mtetezi wa Magamba anapima upepo humu!!!:glasses-nerdy:
   
 8. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #8
  Apr 22, 2012
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,341
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  nini tena hii
   
 9. Prof Gamba

  Prof Gamba JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 387
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Watu wengine bwana!! Ndo umeongea nini na kwa nini usisubiri kwanza huo uthibitisho?
   
 10. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #10
  Apr 22, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,614
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  Pasco baada ya kumkandia bulaya juzi tayari ashakupa bahasha.una njaa msukuma wewe
   
 11. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #11
  Apr 22, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mboana hata Mwigulu ni shujaa nae? Kutembea na wake za watu tena ugenini ni zaidi ya Ushujaa!
   
 12. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #12
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 8,713
  Likes Received: 1,593
  Trophy Points: 280
  Hiki chama tawala kitakupeleka pabaya
  naona sasa umekua teja CCM.
   
 13. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,337
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  Sasa nayo hii ni habari?
   
 14. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #14
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,971
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  acha uzuzu unashusha heshima yako JF.
   
 15. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #15
  Apr 22, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  Bulaya si ndio yule walienda kufanya fujo na kufyatua risasi kwenye kambi ya cdm wakitokea disco na jamaa zake kule igunga halafu policcm wakamkamata mwita mwikabe?
   
 16. Mr.mzumbe

  Mr.mzumbe JF-Expert Member

  #16
  Apr 22, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 756
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Huyu kama yule jamaa aliyekuwa nchi ya mbali.Alimtumia baba barua lakini kwenye karatasi husika hakuandika chochote,eti alikuwa na haraka!!!
   
 17. Shardcole

  Shardcole JF-Expert Member

  #17
  Apr 22, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,541
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  Jamani tusimlaumu huyu pasco kwani huenda alikunywa mvinyo wa dom zas y akawa na haraka ya kupost uhuni wake humu kwani yy ameshindwa nn kusubiri ili apate vithibitisho ndo aje humu jf pia inaelekea anaanza kuwapaka mafuta magamba wenzake.
   
 18. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #18
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,971
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Kama kila member angekuwa anarusha thread kwa mtindo wako JF ingekufa ingejaa *****. Shiriki kutunza heshima ya JF
   
 19. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #19
  Apr 22, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 16,201
  Likes Received: 5,655
  Trophy Points: 280
  watu wanaoheshimiwa jukwaani ndio wanakua wa kwanza kulivunjia heshima jukwaa...
   
 20. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #20
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Nilidhani kajiuzulu ubunge kwa vile JK amepiga chini mapendekezo yao! kama ni kusaini kitabu cha wabunge 70 sioni ushujaa hapo kwa sababu wanapaswa kufanya hivyo hasa ili kutetea kauli zao bungeni.
   
Loading...