Mbunge wa CCM aumbuka kwenye jimbo lake (Maghembe) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge wa CCM aumbuka kwenye jimbo lake (Maghembe)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Henry Kilewo, May 29, 2011.

 1. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #1
  May 29, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  WAFUGAJI katika wilaya ya Mwanga kwa muda mrefu wamekuwa wakitaabika kutafuta maji kwa ajili ya mifugo yao.

  Hili limesababisha mifugo kusafirishwa umbali mrefu ili kufuata maji. Hali hii imekuwa ikichosha mifugo na wakati mwingine kufa kutokana na uhaba wa majani unaosababishwa na ukame.

  mbunge wa jimbo hilo muda mchache kabla ya uchaguzi aliwahadaa wananchi wa jimbo hilo ya kuwa atawapatia Lambo la kuhifashia maji hususani ni wale wa vijiji vya KIRURI NA LWAMI mpaka ikafikia hatua ya kumteua mwenyekiti wa mradi huwo ambaye ni bwana MSAMI MKWIZU.

  Mwenyekiti wa mradi huo, Msami Mkwizu anasema kwamba lambo hilo ambalo lilitarajiwa kumaliza kilio cha kihistory cha vijiji hivyo limegeuka kuwa kero kwake kwa wananchi kumfuata kila kukicha kwake juu ya swala hilo kana kwamba yeye ni mbunge, vile vile kijana huyo ambaye ni kijana mwenzangu amenieleza ya kuwa kila akimpigia mheshimiwa huyo simu anamueleza nipo kwenye kikao.

  Wananchi hawo wanalaani tabia ya mbunge wao kuwatelekeza na wameapa kutompa ushirikiano wa jambo lolote lile ila mwisho wake ni 2015 hata akishindana na jiwe litashinda jiwe.

  "Pia wananchi tumechangia kwa kiasi kidogo hasa katika kufyeka eneo husika ili wapimaji waweze kupima na kupendekeza ukubwa wa Lambo unaofaa," anasema Mkwizu wakati akinionyesha sehemu hiyo, nilitembelea kijiji changu nilipo kulia cha LWAMI ndipo nilipo kutana na kero hiyo na nyinginezo nyingi.

  MAONI YANGU
  maghembe nenda jimboni ukashughulikie kero za wananchi wa mwanga lasivyo yatakutokea kama ya mwenzako wa tarime na usitulaumu wananchi wa mwanga.
   
 2. n

  never JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Aisee kipindi cha kampeni tuliwaambia wananchi wa MWANGA ya kuwa mbunge wao ni kilaza ila kwa ubishi wao na ujauri wao walituona hatufai na kusababisha kufanya kampeni kwenye wakati mgumu sana, ila tuliwaambia mkichagua CCM mmechagua maafa sasa acha kwanza waonje joto ya jiwe then watakaa sawa sawa.
   
 3. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu, wana Mwanga ishakula kwenu mpaka miaka mitano iishe, mtajuuuuuta.
   
 4. R

  Red one Member

  #4
  May 29, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Dr slaa alisema, kuichagua CCMni janga la kitaifa ila kwakuwa wtanzania wa mwanga ni viburi kweli kweli waka mpa maghembe na kikwete kura nyingi kweli kweli , sasa wanamwanga endeleeni kuumia kama mlivyo sema mpaka hiyo miaka 5 iishe then mjirekebishe acheni tabia za nethienda itawamaliza vibaya sana lazima mbadilike mwingia kwenye dunia nyingi la sivyo mtakuwa wa mwisho
   
 5. MAYOO

  MAYOO JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Huko mwanga ndo ishakula kwenu, anyway kwavile wabunge wa cdm ni wa taifa watawasaidia. Siku nyingine mtumie akili si ushabiki. Si mmeona yalowakuta mbunge wenu yuko busy huku dar wala hana habari
   
 6. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #6
  May 29, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huyu Maghembe ateweza kushughulikia matatizo ya wsafugaji ilihali yeye si mfugaji? Tusubiri tuone!
   
 7. Ngigana

  Ngigana JF-Expert Member

  #7
  May 29, 2011
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 1,259
  Likes Received: 373
  Trophy Points: 180
  Jambo moja huwa silielewi sawasawa labda kwa kuwa shule ilinipita pembeni. Hivi yale maeneo ya Mwanga , same nk huwa naona wakati wa mvua kuna maji yanaporomoka toka milimani na wakati mwingine yanakata barabara au husababisha hata safari za Arusha/Dar kutatizika. Hivi kinagomba nini kuvuna yale maji let us say kwa kuchimba lambo maji yale yote yakakusanywa ili yafae si kwa wafugaji tuu, bali hata kwa kilimo cha umwagiliaji? bado huwa sipati jibu?:mod:
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  May 29, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mie sina huruma nao hao watu wa Mwanga maana kama walionywa hawakusikia basi poa acha wamtambue Maghembe yeye anamalizia miaka 5 then hakuna kitu hataomba tena .
   
 9. z

  zamlock JF-Expert Member

  #9
  May 30, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  haya kazi wanayo
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  May 30, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,407
  Likes Received: 81,436
  Trophy Points: 280
  CCM yachafuka

  • Vijana wawakaanga Lowassa, Chenge, Rostam

  na Mwandishi wetu
  TANZANIA DAIMA  HALI ya kisiasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inazidi kwenda mrama baada ya vijana na makada wa chama hicho kutaka watuhumiwa wa ufisadi wang’olewe haraka ili kukinusuru chama.

  Vijana hao wamebainisha kuwa uwepo wa mapacha watatu ndani ya chama hicho kutakifanya chama hicho kuwa cha upinzani mwaka 2015, jambo ambalo hawapendi litokee.

  Wakizungumza katika mkutano wa kuangalia namna ya kukinusuru chama hicho jana katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, vijana hao walisema watuhumiwa hao hivi sasa wanakimaliza chama kwa kutumia fedha zao kuanzisha makundi ya kuwachafua makada wenzao.

  Vijana hao walisema kuwa CCM si nyumba ya kupanga, hivyo hakuna sababu ya kutoa muda kwa wanachama wanaotuhumiwa kwa ufisadi.

  Walibainisha kuwa kadiri Rais Jakaya Kikwete anavyozidi kuchelea kuwachukulia hatua watuhumiwa hao ndivyo anavyokiweka rehani chama hicho kikongwe kilichodumu madarakani kwa takriban miaka 34.

  Walisema hivi sasa vijana wamekuwa wakipewa fedha na watuhumiwa ili waendeshe kampeni za kukivuruga chama hicho kwa malengo binafsi.

  Walibainisha kuwa uwepo wa Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, Andrew Chenge na Rostam Aziz, kamwe hauwezi kukiponya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

  Wachambuzi wa masuala ya siasa wamelidokeza Tanzania Daima Jumapili kuwa malumbano yaliyozuka hivi karibuni juu ya makada wa CCM kuhusishwa na mchakato wa kukianzisha Chama Cha Jamii (CCJ) ni miongoni mwa mambo yaliyochochea zaidi mpasuko ndani ya chama hicho.

  Wanaongeza kuwa kujitokeza kwa vijana wa CCM Mkoa wa Arusha wakitaka Mwenyekiti, James ole Millya, kujiuzulu wadhifa wake kwa madai ya kutumiwa na Lowassa kuchochea vurugu na mpasuko, waliweka wazi pia hatua ya vijana hao kumkataa Katibu Mkuu wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Marry Chatanda, kunaonyesha wazi kuwa dhana ya kujivua gamba imeongeza mpasuko na minyukano.

  Hata hivyo waliweka bayana kuwa CCM wana wakati mgumu wa kuwatosa Lowassa, Chenge na Rostam, ambao mbali na kufanikisha mpango wa kumuingiza madarakani Rais Kikwete lakini pia wana mizizi na uungwaji mkono katika ngazi za maamuzi.
  “Mwenyekiti, hali ni mbaya na ninapenda ukweli huu ufahamike, kwani sisi ndio tunakaa na watu wa matawi na vijana wengine tunajua hali halisi, hili suala la mafisadi hasa hawa mapacha watatu lisiposhughulikiwa tutaendelea kuumbuka kila siku,” alisema Matefu.


  Akichangia hoja hiyo ya hali ya kisiasa katika chama hicho, Katibu wa UVCCM Kata ya Ilala, Karim Lichela, alisema kwa kiasi kikubwa upinzani unaofikiriwa ni wa kupambana na CHADEMA, badala ya kufanya maboresho ndani ya chama kwa kuwawezesha vijana kufuata misingi thabiti ya umoja huo tofauti na ilivyo sasa kwani misingi hiyo imewekwa pembeni.

  Alisema wakati wanachama wakifikiria uchaguzi wa mwakani, ni wakati muafaka kwa baadhi ya viongozi kujivua gamba kwa kuacha nafasi zao ndani ya chama na ikibidi wajivue uanachama.
  Katika michango yao wajumbe wengi walionyesha wasiwasi wao kwa namna Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinavyoweza kuwashawishi vijana kujiunga na chama chao na kuonya kuwa hali hiyo isipodhibitiwa sasa (CCM) itakuwa na wakati mgumu katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.


  Aliongeza kusema kuwa kuendelea kujifariji kuwa kuna wanachama wapya zaidi ya 10,000 ni kujiweka gizani, kwani kwa jiji lenye watu zaidi ya milioni nne hesabu hiyo ni ndogo kwa muda wa miaka mitatu.

  “Ukweli ni kwamba kuna tatizo ndani ya umoja wetu hata ukiangalia wanaopata nafasi za kusafiri nje ya nchi wengi ni wanawake wa viongozi wa UVCCM au wale wenye ukaribu nao kwa sisi watoto wa walalahoi ni ndoto kupata nafasi hizo,” alisema Lichela.

  Aidha, vijana hao wameutaka umoja huo kuwawajibisha wale wote waliochangia kwa namna moja ama nyingine kwa chama hicho kushindwa katika baadhi ya majimbo ndani ya mkoa.
  Naye mmoja wa wajumbe hao aliyeomba jina lake lihifadhiwe alisema suala la CCM kudandia hoja za vyama vya upinzani pasipo chama hicho kuifanyia kazi imekigharimu kwa kiasi kikubwa chama hicho.

  “Tumekuwa ni wadandiaji wa hoja za wapinzani, walikuja na hoja ya Katiba, hatukujiandaa kuijua sisi, tukaivamia kwa kudhani wananchi watatuunga mkono, kwa kuwa hatukuielewa …matokeo yake tumefedheheka na tukazidi kuwapa sifa wapinzani kuwa wako makini na hoja zao,” alisema mjumbe mmoja nje ya kikao.

  Alizidi kusema kuwa hata suala la rada linahitaji umakini, kwani liliamuliwa na Baraza la Mawaziri, hivyo kitendo cha kumpeleka Chenge (Andrew) mahakamani ni kutafuta fedheha kama iliyopo sasa katika kesi ya Profesa Costa Mahalu. “Tukimpeleka Chenge mahakamani wataumbuka wengi kama ilivyo sasa kwa ushahidi wa Mahalu kumtaka Rais mstaafu Benjamin Mkapa kutoa ushahidi, hali inayomlazimu Rais Kikwete naye kutakiwa kutoa ushahidi,” alisema mjumbe huyo.
   
 11. z

  zamlock JF-Expert Member

  #11
  May 30, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  kazi kweli kweli wanalo miaka minne hii ijayi siyo nchezo
   
 12. g

  gambatoto Senior Member

  #12
  May 30, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), amesema kuwa kuna haja ya Watanzania kuungana ili kuzuia mbinu chafu za Chama cha Mapinduizi (CCM) za kugeuza nchi kuwa dola ya kipolisi.

  Lissu alisema hayo mwishoni mwa wiki kwenye mkutano wa hadhara wa CHADEMA uliofanyika kwenye viwanja vya kata ya Majengo, Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.

  Akizungumza kwenye mkutano huo, Lissu alisema yanayoendelea kutokea Tarime ni mfano mzuri kuwa lengo la CCM ni kuigeuza Tanzania dola ya kipolisi baada ya Rais Jakaya Kikwete na chama chake kushindwa kuongoza kwa hoja.

  “Watanzania tusilifumbie macho suala la Tarime kwa sababu yanayotokea yanatuhusu sisi sote na mwisho ya siku yatahamia katika mikoa mingine kutokana na mipango inayofanywa na CCM kuhakikisha kuwa majimbo ambayo CHADEMA inapendwa yanachukiwa na ikiwezekana kuwaua watu bila sababu,” alisema Lissu.

  “Tunachotaka ni kuzuia nchi hii isiweze dola ya kipolisi maana ndio agenda yao pekee iliyobaki, kuwapa polisi uhuru wa kuwaua raia,kuwatesa na kujeruhi,”alisisitiza.
  Rais Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi mkuu wa mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile, kutokana na ajali iliyosababisha vifo vya watu 13 na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa.

  Ajali hiyo ilitokea juzi baada ya basi la Kampuni ya Summry lililokuwa linatokea Arusha kwenda Mbeya kupasuka tairi la mbele lilipofika eneo la Igawa, mkoani Mbeya na kusababisha dereva kushindwa kulimudu na kupinduka.

  Taraifa kwa vyombo vya habari iliyolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, ilieleza kuwa Rais Kikwete amesikitishwa na ajali hiyo, kwani licha ya kuleta simanzi na majonzi makubwa kwa familia na ndugu za marehemu hao, taifa nalo limepata hasara kubwa kwa kupoteza nguvu kazi muhimu kwa maendeleo ya nchi.

  “Nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana na vifo hivi kwani vimeleta simanzi na majonzi makubwa kwa familia, ndugu na jamaa waliopoteza wapendwa wao kwenye ajali hiyo,” alisema Rais Kikwete.

  Kwa wale waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo, Rais Kikwete alisema anamuomba Mola awajalie wapone haraka na kurejea katika hali zao za kawaida ,ili waweze kuungana tena na familia, ndugu, jamaa na marafiki zao.

  Source: Taznaia Daima
  Rais Kikwete atuma salamu za rambirambi ajali ya Mbeya

  Mytake: Mbona sijamsikia akituma Salamu za Rambirambi za Tarime?
   
 13. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #13
  May 30, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kuna haja mwezi wa 9 Palestina wanapoenda UN kuomba kutambuliwa kama Taifa Tarime nao watume maombi hawa ndugu zetu utadhani sio raia wa nchi hii.
   
 14. t

  tambarare Senior Member

  #14
  May 30, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kikwete ni m**** sana kwa hiyo ni faraja sana kwake kutuma salamu za rambirambi badala ya kuangalia namna ya kumaliza hili tatizo........anaona raha sana hii nguvu kazi inavyopotea kila siku?????? Kwa nini asitafute njia mbadala????????
   
 15. F

  FJM JF-Expert Member

  #15
  May 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
   
 16. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #16
  May 30, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,956
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Ni kasheshe tu mtindo mmoja mpaka kieleweke.
   
 17. J

  Jiwe Member

  #17
  May 30, 2011
  Joined: Oct 17, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mytake: Mbona sijamsikia akituma Salamu za Rambirambi za Tarime?[/QUOTE]

  Usihofu subiri kesho utasikia kwenye hotuba yake ya mwisho wa mwezi. Naona hii ndiyo pointi kuu pekee imeachwa makusudi itumike kwa ajili ya kulaani UPINZANI na kuwaasa WANANCHI kuzingatia sheria. Just stay tuned!!!
   
 18. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #18
  May 30, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,261
  Likes Received: 19,387
  Trophy Points: 280
  wakome wakome kabisa tena maghembe hivi vijamaa vifupi vikaushie kabisa pumbafu kabisa hivi
   
 19. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #19
  May 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nitafanya kosa kusema Kikwete ndiye aliyesababisha mauaji ya Tarime kwa sababu hajaonyesha kushtushwa na wala hakuthubutu kuwapa pole wafiwa na other walizopata wananchi? Hata usanii wa kisiasa wa watu wa kawaida tu wangefanya hivyo, jamani sijapata kuona haya.
   
 20. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #20
  May 30, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  MIKOA ya Dodoma na Morogoro imetajwa kuwa ni mikoa inayoongoza kwa wanafunzi wa kike kukatisha masomo kutokana na kupata ujauzito.
  Hayo yalibainishwa jana na mke wa Rais, Mama Salima Kikwete alipohutubia katika sherehe za siku ya matembezi ya hisani ya chakula mashuleni yaliyofanyika kitaifa mkoani hapa.
  Alisema pamoja na juhudi za serikali na wizara mbalimbali kuhakikisha wanapambana na masuala ya utoro shuleni ikiwa ni pamoja na kutoa chakula cha mchana, bado mikoa hiyo imekuwa na ongezeko la wanafunzi wanaopata ujauzito tofauti na matarajio ya serikali. Alisema katika kipindi cha mwaka 2008 wanafunzi walioacha shule ya msingi kwa kupata ujauzito katika mkoa wa Dodoma walikuwa 216 ambapo mpaka mwaka huu wameongezeka na kufikia 225 nakuongeza kuwa mkoa wa Morogoro ulikuwa na wanafunzi walioacha shule kwa ujauzito walikuwa 296 na wameongezeka hadi 322 mwaka huu.

  MAONI YANGU: mimi nadhani kuna uhusiano mkubwa sana kati ya bunge letu na hizi mimba, maana kukiwa na Bunge viongozi wengi wa serikali wanatakiwa huko pamoja na wabunge, wengi wao hawaendi na wake zao.
  kuna mbunge mmoja nilikuwa namfahamu yeye alichukua mtoto wa shule na kuweka ndani kabisa, japo hakukuwa na mimba lakini alimualibia shule
  ndipo mimi najiuliza hayo maeneo (dodoma & morogomo) kuongoza kwa mimba za wanafunzi chanzo sio ili bunge kweli?
   
Loading...