Mbunge wa CCM aomba arudishiwe madawati aliyotoa shuleni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge wa CCM aomba arudishiwe madawati aliyotoa shuleni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Landala, May 28, 2011.

 1. Landala

  Landala JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 938
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Mbunge wa zamani wa jimbo la Musoma mjini kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Vedasto Mathayo ameomba arudishiwe madawati yake yenye thamani ya shilingi milion 18 aliyoyatoa kwa shule mbali mbali wakati akiwa mbunge.

  Mwandishi wa Tanzania Daima alipongea naye kwa njia ya simu alilithipitisha hilo na kusema kuwa yupo mbioni kwenda mahakamani,mbunge huyo wa zamani aliangushwa kwenye uchaguzi mkuu uliopita na mbunge wa sasa kupitia Chadema mheshimiwa Vincent Nyerere.

  Habari zaidi zinasema mbunge huyo wa zamani wa Ccm bwana Mathayo ameamua kuchukua uamuzi huo kutokana na wananchi wa jimbo la Musoma mjini kutomchagua tena kuwa mbunge kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana, hivyo ameamua kuwakomoa wananchi kwa kumyima kura na kuamua kumchagua mbunge wa Chadema.

  Mbunge huyo wa zamani ambaye ni mfanyabiashara wa mafuta amesema aliyanunua madawati hayo kwa sh elfu 40,000 kwa kila dawati na jumla alitumia shilingi milioni 18. Anataka arudishiwe madawati au alipwe milioni 18.


  Source: Tanzania Daima.
   
 2. Bollo Yang

  Bollo Yang JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 440
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hiyo source sio reliable kwa habari hiyo, yani ni sawa na kutuletea source ya gazeti la Uhuru kuzungumzia habar negative ya CDM...
   
 3. i411

  i411 JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 810
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Watu wengine bwana wanapenda kutafuta umaarufu kwa kila njia, mwangalie huyu mwingine gamba limemganda mpaka halitaki kutoka sasa anaganda nalo
   
 4. kidi kudi

  kidi kudi JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 60
  hivi haya wanayoyafanya viongozi wetu mbona yanatia aibu jamani!? inashangaza kwani kuna mbunge mwingine aliyekua wa jimbo fulani Mwanza nae kama huyo mwenzake alipopigwa chini kwenye uchaguzi mkuu mwaka jana, nae alinukuliwa akitaka kuchukua vitu anavyodai ni vya kwake kwenye ofisi ya mbunge!!! Khaaa, sasa hii maana yake nini? Tutafika kweli kwenye maisha bora kwa kila mtanzania kwa hali hii?? Viongozi kama hawa wanaionyesha jamii ni kwa jinsi gani wasivyostahili hat kupewa uongozi wa Kaya!!! inshangaza sana. Anyway hilo ni fundisho kwetu wa-Tz kwamba tunachagua watu kwa kudanganywa kwa vitu vidogo pasipo kupima kwa umakini kama huyo tunayetaka kumchagua an nia ya dhati ya kuleta maendeleo.

  imeniuma sana kwa hilo analotaka kufanya huyo mheshimiwa wa zamani, kwani siasa haziko hivyo!!!!! VIONGOZI JIREKEBISHENI
   
 5. S

  Sharo hiphop JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 662
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Huyo ni tahira, kwa biashara na siasa ni wapi na wapi? Hao ndo wale wanaoweka masilahi yao mbele. Anaongea maneno kama hayo hata haya hana!
   
 6. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Daaah!
  Mathayo baba......
   
 7. k

  kibajaj Senior Member

  #7
  May 28, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hiyo kali ya mwaka alikopa anataka akayauze arudishe pesa za watu
   
 8. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #8
  May 28, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Mkuuu hii ni kweli mbona hata kweny TV walimwonyesa na alisema atawapeleka madiwani na mbunge mahakamani!
   
 9. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #9
  May 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Huyo bwana ni kilaza sana, level ya elimu yake ni form two, alikuwa ni mbunge wa jimbo letu. Amshukuru mungu kamjalia mapesa!
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  May 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kama ni kweli basi wana MUSOMA wasinunue bidhaa toka kwake (kama kuna alternative). Wagomee biashara zake zote
   
 11. T

  Twasila JF-Expert Member

  #11
  May 28, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,913
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  Wakuu, msifanye mzaha na mambo mazito kama haya. Jitahada za makusudi zifanyike haraka kumpeleka Mirembe.
   
 12. T

  Twasila JF-Expert Member

  #12
  May 28, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,913
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  Wakuu, msifanye mzaha na mambo mazito kama haya. Jitihada za makusudi zifanyike haraka kumpeleka Mirembe.
   
 13. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #13
  May 28, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,601
  Likes Received: 2,458
  Trophy Points: 280
  Huyu brother mathayo ana roho ya ubinafsi tena imemshika kweli kweli!
   
 14. R

  Radi Member

  #14
  May 28, 2011
  Joined: May 22, 2010
  Messages: 94
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kwa maana hiyo ,hiyo ilikuwa ni rushwa kwa njia mmoja ama nyingine ili apewe tena ubunge,Takukuru mko wapi kufuatilia hili swala????Unatoa Msaada/Zawadi/au huduma kwa watoto lakinini kwa masharti lazima wazazi wakuchague tena!!!!! Aibu Chama Cha Magamba.!!!CCM
   
 15. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #15
  May 28, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Asirudishiwe hela wala madawati au hata kitu chochote. Badala yake apelekwa Mirembe kwa uchungu wa akili kwani wasiwasi na uwezo wake wa kiakili au hata uwezo wa kufikiria.
   
 16. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #16
  May 28, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Duh!! hawa ndio wabunge wa ccm wavua magamba sasa sijui akili zake kazisahau kwenye droo!!!!
   
 17. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #17
  May 28, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Tanzania Daima wamempakazia Mathayo mutu ya watu, juzi juzi tu aliwapeleka wananchi wa Musoma Mjini kwa babu Loliondo.
   
 18. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #18
  May 28, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Mbunge wa zamani Jimbo la Musoma Mjini mkoani Mara, Vedasto Mathayo (CCM), ametoa kali ya mwaka baada ya kwenda kwenye vyombo vya dola, akidai arudishiwe madawati aliyotoa kwenye shule mbalimbali wakati akiwa mbunge.

  Mathayo alikuwa mbunge wa Musoma Mjini kwa muhula mmoja (2005-2010) na aliangushwa na mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Vincent Nyerere, katika Uchaguzi Mkuu mwaka jana.

  Mathayo alisema anataka arudishiwe zaidi ya madawati 460 anayodai aliyanunua wakati akiwa mbunge wa jimbo hilo, na hataki maelezo mengine juu ya hilo.

  Madai ya mbunge huyo wa zamani, yamekuja kufuatia kile kinachoelezwa kutaka 'kuwakomoa' wananchi aliokuwa akiwatumikia, kwa kushindwa kumchagua katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

  Akihutubia mkutano wa hadhara hivi karibuni katika uwanja wa Shule ya Msingi Mukendo, mbele ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilson Mukama, alisema tayari ameshalifikisha suala hilo kwenye vyombo vya dola kwa hatua zaidi za kisheria, akitaka apewe madawati yake ama arudishiwe fedha alizotumia kununua vifaa hivyo.

  "Kweli nadai madawati niliyoyanunua wakati nikiwa mbunge wa Musoma Mjini. Ninataka warudishe madawati yangu au walipe fedha nilizotumia kununulia zaidi ya madawati 460, na kila dawati lina thamani ya Sh. 40,000, ambapo kwa madawati yote yana thamani ya Sh. milioni 18.4.

  "Kwa vile nataka haki yangu, tayari suala hili nimeshalifikisha polisi kwa ajili ya kupelekwa mahakamani...warudishe mali yangu, mimi sitaki mambo mengine. Nilitumia fedha zangu binafsi kununua madawati haya ndiyo maana nazitaka," alisema Mathayo katika mkutano huo.

  Wakazi wengi wa mjini Musoma, walieleza kushangazwa na hatua hiyo ya Mathayo kuanza kudai arudishiwe madawati aliyoyanunua akiwa kiongozi, na kwamba hali hiyo inatokana na kushindwa kwake kwenye uchaguzi uliopita pamoja na kukata tamaa ya kisiasa.

  Mbali na hayo, walisema Mathayo hapaswi kurudishiwa madawati hayo bali yaendelee kutumika shuleni kwani aliyanunua kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo na hayakuwa dhamana ya uongozi wake.

  Naye Mbunge wa sasa wa jimbo hilo la Musoma Mjini, Vincent Nyerere, aliiambia NIPASHE kwa njia ya simu kuwa yuko tayari kufungwa jela na atahakikisha madawati hayo hayachukuliwi na Mathayo.

  Alisema fedha zilizotumika kununulia vifaa hivyo ni zile za maendeleo ya jimbo.

  "Haiingii akilini mtu akishindwa kwenye uchaguzi halafu anaanza kudai arudishiwe mali alizotumia, kama huo ni utaratibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wananchi wa Musoma hawako tayari kwa ubabe na dharau za namna hiyo," alisema.

  "Mimi niko tayari kufia jela kwa kupinga madawati haya yarudishwe kwa Mathayo. Tunafahamu madawati haya yalinunuliwa kwa fedha za umma zinazotokana na Mfuko wa Jimbo. Sasa nimemshinda anataka arudishiwe? Wapi na wapi?," Alihoji Vincent.

  Aliongeza: "Kama anabisha kwamba hajatumia fedha za Mfuko wa Jimbo kununua madawati haya, basi awaeleze wananchi fedha za mfuko huo zimetumikaje wakati akiwa mbunge."

  Alisema kama watu wa CCM wanataka watoto wasomee chini, wao Chadema hawataki hilo na ieleweke hivyo. Vincent kwa sasa yupo jijini Dar es Salaam kuhudhuria vikao vya Kamati za Bunge.

  Baadhi ya viongozi na makada mbalimbali wa CCM mkoani Mara, walieleza kushangazwa na kitendo cha Mathayo kuanza kudai vifaa vya maendeleo alivyonunua wakati akiwa kiongozi, na kwamba hatua hiyo inakidhalilisha chama tawala na viongozi wake.
   
 19. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #19
  May 28, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Hizo fedha alizotumia kununulia madawati ni kodi za wananchi anazolipwa kama mshahara,aanze yeye kurudisha kodi hiyo aliyokula kwa kipindi chote alichokuwa Mbunge..
   
 20. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #20
  May 28, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,951
  Likes Received: 1,275
  Trophy Points: 280
  why dont you call him and confirm? Need his number?
   
Loading...