MBUNGE WA CCM anayelelewa na wake zake kwa biashara ya mama ntilie

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,837
Aliyekuwa mbunge wa Songea mjini, Abdulrabi Ali Yusuph(66) akizungumzia maisha yake baada ya kufungwa jela akiwa nyumbani kwake hivi karibuni. Picha na Lauden Mwambona. .
Aliyekuwa Mbunge wa Songea mjini kuanzia Oktoba 1985 hadi Aprili 1988 alipofungwa jela miaka 11, Abdulrabi Ali Yusuph (66), amesema tangu atoke gerezani hadi sasa anaomba aonane na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ama Rais Benjamin Mkapa na hata Rais Jakaya Kikwete lakini hajafanikiwa hadi leo.
Amesema aliomba nafasi ya kumwona Rais Mwinyi akiwa madarakani ili amweleze ya moyoni, lakini hakufanikiwa na aliendelea kuomba amwone Rais Mkapa hakufanikiwa na sasa anaomba amwone Rais Kikwete bado hajajaaliwa.
Alisema hayo katika mahojiano maalumu yaliyofanyika nyumbani kwake Mtaa wa Mfaranyaki mjini Songea ambako anaishi akiwa kwenye nyumba chakavu ya urithi na wake zake wawili pamoja na watoto kadhaa.
Mahojiano ya mwandishi na mbunge huyo yalianza hivi.
Mwandishi: Mheshimiwa habari za siku nyingi. Nimefika hapa kwa niaba ya jarida la Ndani ya Habari linalochapishwa na gazeti la Mwananchi, lengo hasa ni kukujulia hali. Watu wangependa kujua unaendeleaje hasa baada ya kifungo chako. Ningependa kupata maelezo yako juu ya masuala ya maisha ya gerezani na ya sasa ukiwa huru.
Mbunge. Kwanza kabla ya yote. Wewe upo hapa ili uuze gazeti na upate fedha. Je, mimi unanieleza vipi kuhusu mapato hayo.
Mwandishi: Kazi ya mwandishi siyo biashara, bali ni ya kijamii. Kazi ya mwandishi ni kuelimisha, kufundisha, kuibua kero na kutaarifu jamii. Kazi ya mwandishi inaweza kukusaidia ama kukuharibia kwa kuibua mambo ambayo unaweza kufanya kwa kuvunja sheria na kuitisha jamii.
Mbunge: Kwa maneno yako haya ni kwamba mimi sina lolote la kufaidika leo?
Mwandishi: Ni kweli sikuja hapa kibiashara bali kukusalimu na kupata hisia zako ama kauli yako baada ya kufungwa jela kwa miaka 11 ukiwa mbunge na sasa upo nje, hivyo tunapenda kujua uliishi vipi jela na jamii inakuonaje baada ya kutoka?
Mbunge:Basi kwa kuwa umefika hapa, nitasema machache, lakini kama utakuja baada ya kujipanga, nitaeleza mengi mno. Mimi ninazo kero na mambo mengi baada ya kuishi gerezani na kwa kweli nina masikitiko mengi ambayo yananisononesha sana.
Mwandishi:Nashukuru Mheshimiwa, naomba udokeze hisia zako walau kidogo.
Mbunge: Kwanza ninayo masikitiko mpaka leo kwa viongozi wakuu wa taifa hili. Nasikitika mpaka leo kwa kunyimwa nafasi ya kuonana na walau mmoja kuanzia Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na hata awamu ya nne Jakaya Kikwete.
Mimi ninayo mambo mengi sana kwa viongozi wetu, Serikali na hata kwa taifa, lakini nasikitika kuona waliokuwa viongozi wenzangu wamenitenga kana kwamba mimi ni shetani’’ anasema.
Mimi nilibambikiwa meno ya tembo na hatimaye nilifungwa jela, nilichojifunza cha kwanza ni kwamba jamii ina tabia ya kuwanyanyapaa waliowahi kufungwa jambo ambalo hata viongozi wa taifa nao wanatekeleza kwa vitendo juu yangu. Wapo viongozi wenzangu ambao wakati ule tulicheka pamoja, tulikula pamoja na kucheza pamoja, lakini baada ya mimi kwenda jela hawaonekani.
Kufungwa kwangu kulipangwa
Mwandishi:Unasikitika kwa kufungwa kwako ama kunyanyapaliwa?
Mbunge:Mimi baada ya kufika gerezani nilijiuliza swali la kwanini nimefungwa? Maana ukweli ni kwamba meno ya tembo siyo yangu. Baadaye nilipata jibu kwamba nilifungwa ili nikaone mambo maalumu magerezani. Mambo niliyoyashuhudia yanatisha. Lakini la kwanza ni kwamba siyo wote wanaofungwa wanatenda makosa waliyoshtakiwa nayo. Pili niligundua kwamba askari magereza si wabaya wakiwa kazini, bali wabaya ni waliokupeleka kwao.
Pia nilijifunza kwamba askari magereza wanafanya kazi katika mazingira magumu kiasi kwamba wanafika hatua ya kuomba msaada kwa wafungwa. Pia niliona wazi kwamba wapo wafungwa wanaorudi gerezani kwa kupenda huku wengine wakirudishwa gerezani kwa hila za udhalimu.
Nilishuhudia kunyongwa kwa wafungwa 11 na nilishiriki kusafisha vitanzi vyao, miongoni mwao, wapo walionyongwa huku wakikana kutenda makosa waliyoshtakiwa nayo.
Mwandishi: Maisha yalikuwaje gerezani?
Mbunge:Baada ya kuhukumiwa kufungwa nilitoka gereza la Songea kwenda gereza la Lilungu Mtwara, baadaye nilipelekwa Ukonga Dar es Salaam na hatimaye Gereza la Maweni Tanga. Cha kushangaza katika magereza yote mimi nilikuwa mnyapala mkuu na pia imamu wa kuswalisha Waislam waliofungwa.
Aporwa mke baada ya kufungwa
Mwandishi:Ukiwa jela , je uliifikiriaje familia yako?
Mbunge:Kwa kweli nasema wazi kwamba suala la kufungwa kwangu lilipangwa na watu mbalimbali. Nasema hivi kwa sababu baada ya miezi mitano hivi , kiongozi wa dini ya Kilokole alinifuata nikiwa Gereza la Lulindi na kuniambia kwamba mke wangu alimbadilisha dini na kuwa mlokole na aliamua pia kumuoa.
Mpaka leo mke wangu wa kwanza ambaye nilizaa naye watoto sita hatujarudiana na amesababisha baadhi ya watoto wangu wawe walokole hadi leo
Mwandishi: Kwa hali hiyo huna mke mpaka sasa?
Mbunge. Hapana, kwa sasa nina wake wawili na watoto, watoto, eeeh nina watoto kadhaa.
Mwandishi: Ulifungwa miaka tisa nwaka 1988 , lakini ulikata rufaa ambayo ulishindwa na hatimaye kufungwa miaka mitatu zaidi, lakini ulitoka kwa msamaha wa Rais ikiwa imebaki miezi minne, je ulijisikiaje?
Mbunge: Nakumbuka nilitolewa siku ya Ijumaa. Basi nikaanza kuifikiri sana siku hiyo kuwa ina maana kubwa kwangu. Nasema hivyo kwa sababu nilizaliwa Ijumaa, nilikamatwa kwa tuhuma za meno ya tembo siku ya Ijumaa, nilihamishwa kutoka Songea kwenda Lulindi siku ya Ijumaa na hatimaye kuachiwa siku ya Ijumaa. Jambo hili lilinipa wasiwasi na kujiuliza mara kadhaa maana yake ninni. Lakini mama yangu mzazi aliyefariki mwaka juzi nakumbuka alinisihi nimshukuru sana Mungu kwa siku yake ya Ijumaa kuifanya kuwa ya matukio makuu.
Mwandishi:Ukiwa gerezani kuna mambo gani unaoyakumbuka zaidi.
Mbunge: Kwa kweli nayakumbuka yaliyokuwa yakitokea nje ya gereza juu yangu. La kwanza linalonisikitisha sana ni taarifa ya Kiongozi wa Bunge (anamtaja jina) ambaye aliwahi kulitangazia Bunge na Taifa kwa ujumla kwamba aliyekuwa mbunge na kufungwa jela Abdulrabi Ali Yusuph amefariki dunia.
Jambo hili lilinisikitisha sana. Nilimwambia Marehemu Dk Laurence Gama akiwa mbunge jambo hilo kwamba nilikerwa sana na alinihakikishia kulimaliza.
Jambo la pili lililonishtua ni kauli ya Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi alipotamka kwamba Serikali yake haina upendeleo katika masuala ya dini akitoa mfano kwamba padri Erio aliyekamatwa kwa makosa ya kuvunja sheria aliamwaachia, lakini ameamua Muislam mwenzake akitaja jina langu aendelee kusota jela. Kauli ile ilinihuzunisha kwa vile kwanza kosa lilikuwa la kubambikiwa na pili kiongozi mkuu anatangaza kuniacha nisote jela.
Mwandishi: Pamoja na kwamba unasema jamii ina mwelekeo wa kuwanyanyapaa wanaofungwa, je wapiga kura wako nao walitekeleza hayo?
Mbunge: Baada ya kutoka gerezani, wapo wana CCM waliofika na kunitaka niwe kiongozi ngazi ya wilaya, kata na hata mtaa, lakini nilisita sana ingawa baadaye nilikubali kuwa Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mfaranyaki hadi mwaka jana. Kwa ujumla utendaji wa CCM kwa sasa umebadilika sana. Hauna shukrani hata kwa waasisi wake. Mimi nina historia ndefu ya Chama hiki. Baba yangu marehemu Abdulrabi Yusuph ndiye aliyekuwa Katibu wa kwanza wa Chama cha TANU. Baba yangu ndiye aliyefanya kazi na Nyerere kwa dhati.
Mwandishi: Viongozi wa Serikali wanaweza kukusahau, je wale wa CCM nao?
Mbunge: Nakueleza baada ya kufungwa, wana CCM walinisahau kabisa , lakini siku moja dada yangu alikwenda Uwanja wa Majimaji alipotembelea Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi na kumwangukia miguuni.
Askari na vyombo vya usalama vilitaka kumfunga dada yangu, lakini Rais aliagiza mwanamke huyo afike Ikulu Songea ambako alikwenda na kuomba Serikali isaidie kuwasomesha watoto wangu wawili ambao alikuwa akiishi nao mimi nikiwa jela.

Basi nashukuru Mwinyi aliagiza CCM iwasomeshe watoto wawili ambao kweli walisomesha hadi kidato cha nne wakati mimi nikiwa jela.
 
A very touching story ila nasikitika huyo mbunge hayuko consistance and I doubt if he Ok na kama anasema ukweli!. Nahisi he is insane na ndio maana wamemkatalia kumuona rais na hata baada ya hii makala, hataweza kumuona JK!.

Mfano mdogo ni kudai ameshuhudia wafungwa 11 wakinyongwa, katika listi ya magereza aliyokaa hakuwahi kukaa gereza la Isanga Dodoma, ambalo ndilo gereza pekee la kunyongea!.

Ameeleza ana wake watatu mke mmoja aliyeporwa ana watoto 6, ila ameshindwa kueleza ana watoto wangapi!.

Uandishi jamani ni taaluma ya watu, kwa sasa fani imevamiwa kila mtu ni mwandishi!, huyo mhojaji was expected to know better mtu kudai ameshuhudia kunyongwa wafungwa 11 huku hajawahi kukaa gereza la Isanga kunashusha kabisa credibility yake na makala yake!.
Pasco
Up date
Nimekubali makosa ya upungufu wa ufahamu wangu kuhusu magereza ya kunyongea Tanzania hivyo Mbunge huyo yuko right sambamba na kuomba radhi kwa presumption ya insanity na lawama kwa mwandishi!. I apologise, nasema sorry na naomba msamaha!.
Pasco.
 
ushahidi umekutia hatiani tulia mh mbunge mstaafu ila acha kutupotosha kuwa umesingiziwa, wakmbushie wenzio wa ccm kina kinanda wawaache tembo wetu kuna siku yatawakuta kama yaliyokukuta hata kama sio leo kila uovu utalipwa
 
Mwamboma ni mwandishi mahiri. Huenda alipitiwa. Nampa pole huyo mbunge. The world is very hostile.
 
A very touching story ila nasikitika huyo mbunge hayuko consistance and I doubt if he Ok na kama anasema ukweli!. Nahisi he is insane na ndio maana wamemkatalia kumuona rais na hata baada ya hii makala, hataweza kumuona JK!.

Mfano mdogo ni kudai ameshuhudia wafungwa 11 wakinyongwa, katika listi ya magereza aliyokaa hakuwahi kukaa gereza la Isanga Dodoma, ambalo ndilo gereza pekee la kunyongea!.

Ameeleza ana wake watatu mke mmoja aliyeporwa ana watoto 6, ila ameshindwa kueleza ana watoto wangapi!.

Uandishi jamani ni taaluma ya watu, kwa sasa fani imevamiwa kila mtu ni mwandishi!, huyo mhojaji was expected to know better mtu kudai ameshuhudia kunyongwa wafungwa 11 huku hajawahi kukaa gereza la Isanga kunashusha kabisa credibility yake na makala yake!.
Pasco

Nakuheshimu sana, naamini wewe unaweza kuwa muandishi mzuri ila usimuite mtu insane kwa kuwa majibu yake hayafanani na yako. Unapoenda kufanya mahojiano na mtu na ukatanguliza dhana ya kuwa anaongopa basi hukuwa na sababu ya kwenda kumuhoji,ungeandika kile unachokiamini.
Ungekuwa umezunguka katika hayo magereza aliyoyataja pengine ungeweza kusema kitu, wewe unajua Isanga tu kuwa ndo gereza pekee linalonyonga watu ila yeye anasema alishuhudia katika magereza aliyozunguka, utakuwa ni mwandishi wa ajabu kama utaanza kubishana naye.
Suala la yeye kutotaja idadi ya watoto ni kawaida,pengine hataki kutaja idadi ya watoto aliokuwa nayo mbona Job Ndugai na hakuna aliyemlazimisha.

Mwisho,.Tusiwadharau wazee hata kama walikosea ila bado wana mambo mazuri pia ya kutuambia na kutufunza.
 
A very touching story ila nasikitika huyo mbunge hayuko consistance and I doubt if he Ok na kama anasema ukweli!. Nahisi he is insane na ndio maana wamemkatalia kumuona rais na hata baada ya hii makala, hataweza kumuona JK!.

Mfano mdogo ni kudai ameshuhudia wafungwa 11 wakinyongwa, katika listi ya magereza aliyokaa hakuwahi kukaa gereza la Isanga Dodoma, ambalo ndilo gereza pekee la kunyongea!.

Ameeleza ana wake watatu mke mmoja aliyeporwa ana watoto 6, ila ameshindwa kueleza ana watoto wangapi!.

Uandishi jamani ni taaluma ya watu, kwa sasa fani imevamiwa kila mtu ni mwandishi!, huyo mhojaji was expected to know better mtu kudai ameshuhudia kunyongwa wafungwa 11 huku hajawahi kukaa gereza la Isanga kunashusha kabisa credibility yake na makala yake!.
Pasco
inawezekana hao wafungwa walinyongwa Kimagumashi pasipo kupelekwa huko Dodoma Ndio Maana pengine alitaka aonane na Rais ili atoe Mapungufu aliyoyaona huko Gerezani ni Kweli kuna idadi kubwa ya Wafungwa wapo Magerezani kwa Makosa ya kubambikiwa huku watuhumiwa harisi wakipeta mitaani Ndio Maana Uharifu haupungui Cha Msingi huyo Mbunge Wa Zamani alipaswa kuelezea ni njia zipi zilitumika kumbambikia Kesi na ni akina nani walishiriki na kwa lengo lipi ?na baada ya kutoka amethibitisha kweli alibambikiwa nyala na ana Mpango wa kufungua kesi kudai fidia ?
 
Kinana si yuko huko kusini amwone ili amsaidie? Maana ndo mwezake ktk kumaliza Temba.
 
idadi ya Watanzania Sasa ni Milioni 45 huku Magereza yakibaki yale yale ya Zamani Hakuna Magereza Mapya kuendana na idadi ya watu Pia Maisha ya Asikari Magereza ikiwemo Sare zao na Sare za Wafungwa ni full Majanga hapa Tz Magereza si Chuo cha Mafunzo cha kurejesha Nidhamu Bali Magereza yamegeuka Kuwa Chuo cha Kujenga Usugu Mtu akitoka Jela anakuwa Sugu na mkorofi zaidi kwa kweli Kuna Haja ya Wabunge kuyatembelea Magereza yote Wazungumze na Wafungwa na Asikari Magereza Nina imani watabaini mengi ya ajabu huko magerezani
 
A very touching story ila nasikitika huyo mbunge hayuko consistance and I doubt if he Ok na kama anasema ukweli!. Nahisi he is insane na ndio maana wamemkatalia kumuona rais na hata baada ya hii makala, hataweza kumuona JK!.

Mfano mdogo ni kudai ameshuhudia wafungwa 11 wakinyongwa, katika listi ya magereza aliyokaa hakuwahi kukaa gereza la Isanga Dodoma, ambalo ndilo gereza pekee la kunyongea!.

Ameeleza ana wake watatu mke mmoja aliyeporwa ana watoto 6, ila ameshindwa kueleza ana watoto wangapi!.

Uandishi jamani ni taaluma ya watu, kwa sasa fani imevamiwa kila mtu ni mwandishi!, huyo mhojaji was expected to know better mtu kudai ameshuhudia kunyongwa wafungwa 11 huku hajawahi kukaa gereza la Isanga kunashusha kabisa credibility yake na makala yake!.
Pasco

Pasco hapa umepotoka, shutuma zako kwa mwandishi hazina mashiko. Mhojiwa akiisha kusema kuwa ameshuhudia waliohukumiwa kunyogwa 11 wakinyongwa akasisitiza kuwa baadhi ya matukio hayo ya unyongaji yeye ndiye alivisafisha vitanzi vilivyotumika kunyongea. Pasco huoni huyu xmbunge amejishuhudia ushahidi wake? sasa kulikuwa na haja ya mhojaji kuanza kubisha naye!!

pasco tatizo lipo kwa serikali yako inayoongozwa na ccm ambayo inasubiri mtu akalalamike ndio ikurupuke kutoka usingizini (precendence ya alhaji profesor juma kapuya)

Pasco inakuwaje kosa kwa mhojiwa kushindwa kutaja idadi ya watoto wake, lakini inakuwa halali kwa JOB NDUGAI kusahau si tu idadi ya watoto hata wake zake hawakumbuki idadi!!!!

Haya ma precedence wanaya set wao wenyewe serikali ya ccm. Kama vipi na wewe Pasco mpokee mwandishi mwenzio kijiti cha udadisi ili hatimaye tujue kama hata gereza la ushora kule ndago linaweza kumning'iniza convict.
 
Last edited by a moderator:
wakati ule alipofungwa alikuwa na miaka 40 mpaka 41 tayari alikuwa na wake watatu! Huyu jamaa ni Msomali?
 
inawezekana hao wafungwa walinyongwa Kimagumashi pasipo kupelekwa huko Dodoma Ndio Maana pengine alitaka aonane na Rais ili atoe Mapungufu aliyoyaona huko Gerezani ni Kweli kuna idadi kubwa ya Wafungwa wapo Magerezani kwa Makosa ya kubambikiwa huku watuhumiwa harisi wakipeta mitaani Ndio Maana Uharifu haupungui Cha Msingi huyo Mbunge Wa Zamani alipaswa kuelezea ni njia zipi zilitumika kumbambikia Kesi na ni akina nani walishiriki na kwa lengo lipi ?na baada ya kutoka amethibitisha kweli alibambikiwa nyala na ana Mpango wa kufungua kesi kudai fidia ?

Upande wa mashitaka uliithibitishia Mahakama pasipo shaka kuwa mtuhumiwa alitenda kosa lile. ndiyo maana hata rufaa aliyokata hakushinda. kwa maneno mengine utetezi wake ulikuwa dhaifu mno kuishawishi mahakama ione ni kwa vipi alibambikiwa mashitaka.
 
A very touching story ila nasikitika huyo mbunge hayuko consistance and I doubt if he Ok na kama anasema ukweli!. Nahisi he is insane na ndio maana wamemkatalia kumuona rais na hata baada ya hii makala, hataweza kumuona JK!.

Mfano mdogo ni kudai ameshuhudia wafungwa 11 wakinyongwa, katika listi ya magereza aliyokaa hakuwahi kukaa gereza la Isanga Dodoma, ambalo ndilo gereza pekee la kunyongea!.

Ameeleza ana wake watatu mke mmoja aliyeporwa ana watoto 6, ila ameshindwa kueleza ana watoto wangapi!.

Uandishi jamani ni taaluma ya watu, kwa sasa fani imevamiwa kila mtu ni mwandishi!, huyo mhojaji was expected to know better mtu kudai ameshuhudia kunyongwa wafungwa 11 huku hajawahi kukaa gereza la Isanga kunashusha kabisa credibility yake na makala yake!.
Pasco
Mkuu ulihusika katika kufanikisha huyo mbunge mstaafu kufungwa?
Au una personnal conflict na huyo mwandishi wa makala?
 
A very touching story ila nasikitika huyo mbunge hayuko consistance and I doubt if he Ok na kama anasema ukweli!. Nahisi he is insane na ndio maana wamemkatalia kumuona rais na hata baada ya hii makala, hataweza kumuona JK!.

Mfano mdogo ni kudai ameshuhudia wafungwa 11 wakinyongwa, katika listi ya magereza aliyokaa hakuwahi kukaa gereza la Isanga Dodoma, ambalo ndilo gereza pekee la kunyongea!.

Ameeleza ana wake watatu mke mmoja aliyeporwa ana watoto 6, ila ameshindwa kueleza ana watoto wangapi!.

Uandishi jamani ni taaluma ya watu, kwa sasa fani imevamiwa kila mtu ni mwandishi!, huyo mhojaji was expected to know better mtu kudai ameshuhudia kunyongwa wafungwa 11 huku hajawahi kukaa gereza la Isanga kunashusha kabisa credibility yake na makala yake!.
Pasco

Mkuu Pasco, hujaekeweka kuwa Isanga pekee ndio inanyonga wakati hata Lilungu prison kuna wafungwa wanaosubiri kunyongwa na kitanzi kipo!!
 
#Pasco
kama huna maslahi binafsi ktk ishu hii,basi uelewa wako na uwezo wako wa kufikiri utakuwa ni mdogo saaaaaaaana.!
 
pasco nawasiwasi na uelewa wako!so kila Uzi ukosoe undo maana umefikia huku!ulishawahii fungwa?if no please shut it up!!!!!
 
Back
Top Bottom