Mbunge wa CCM ajilipua bungeni, ataka mishahara ya watumishi iongezwe mara dufu!

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,775
18,188
Mbunge wa Gairo (CCM), Ahmed Sabiby, amemtaka Waziri wa fedha atafute pesa popote atakapozipata ili aongeze mishahara ya watumishi wa umma mara dufu, kama alivyoahidi Rais, Mh Samia Suluhu Hassan. Ametamka hayo bungeni leo wakati akichangia mapango wa maendeleo wa 2022-2025 bila kupepesa macho, kutikisa masikio wala kumuogoa mtu yeyote. Hebu msikilize wewe mwenyewe kwenye klipu hiyo hapo chini 👇
 
Du! Mkuu una roho mbaya sana aisee! Mbona wabunge wanaolipwa milioni 15 kwa mwezi lakini kila siku wanalalamika pesa hazitoshi huwaachishi kazi kwa kuwanyima kura?
Baba ako ni mbunge hebu tuekee risiti za mwisho wa mwezi huu tujue ukweli upo wapi

Kama umesimuliwa tuliaa
 
Asiyeridhika na mshahara anaolipwa aache kazi aone ilivyo kazi kupata kazi ya mshahara anaotaka. Ilisikika sauti tokea chumba cha pili cha giza cha mtumishi
 
Mbunge wa Gairo (CCM), Ahmed Sabiby, amemtaka Waziri wa fedha atafute pesa popote atakapozipata ili aongeze mishahara ya watumishi wa umma mara dufu, kama alivyoahidi Rais, Mh Samia Suluhu Hassan. Ametamka hayo bungeni leo wakati akichangia mapango wa maendeleo wa 2022-2025 bila kupepesa macho, kutikisa masikio wala kumuogoa mtu yeyote. Hebu msikilize wewe mwenyewe kwenye klipu hiyo hapo chini
Hivi kuna bunge au kikao cha Ccm??
 
Yeye wafanyakazi wake kawaongeza?

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Hivi kuna bunge au kikao cha Ccm??
Ni kikao cha kamati kuu ya CCM ijapokua kuna baadhi wanajilipua bila kujali yanayoweza kuwafika mbele ya safari. Mbunge wa CHADEMA Kasuku Bilago, alihoji mambo ya mishahara kwa watumishi akauawa. Huyu Shabib naye ajiangalie yasije yakamkuta.
 
Asiyeridhika na mshahara anaolipwa aache kazi aone ilivyo kazi kupata kazi ya mshahara anaotaka. Ilisikika sauti tokea chumba cha pili cha giza cha mtumishi
Hivi umemsikia vizuri alichosema huyo mbunge au unakurupuka tu? Nyie ndio aina ya watu ambao mnawarudisha CCM madarakani kila mwaka lakini kila siku unalalamika maisha magumu. Siwashangai, akili zenu zimebemendwa!
 
Watumishi wasiongezewe mishahara. Mishahara inawatosha ndiyo maana hawaachi kazi

Mtumishi anayeona mshahara hautoshi aache kazi. Awe mjasiriamali.
Wajasiria mali ndiyo wanamaisha mazuri hapa Tanzania? Mnachochea wizi na rushwa tu.Shabiby ni mkweli na waziri wa fedha asitafutiwe sababu za kutopandisha mishahara.
Mbona tozo ya miamala imewezekana?
 
Unapita uongozi wa ccm kwa miaka hii saba kwa kukosa utu kwa watumishi wa umma.
 
Back
Top Bottom