Mbunge wa CCM aishambulia serikali, asema ahadi zake hazitekelezeki

Mpandafarasi

Member
Dec 7, 2008
57
11
UPEPO wa mashambuzi dhidi ya maamuzi mbalimbali ya serikali ambao umekuwa ukitoka katika kambi ya vyama vya upinzani na vyama mbalimbali vya kijamii, sasa umeanza kuchukua mkondo mpya baada ya Mbunge wa Jimbo la Ludewa mkoani Njombe, Deo Filikunjombe (CCM), kudai kuwa matumizi makubwa ya mamilioni ya fedha kwa ajili ya kilele cha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania ni sawa na usaliti.

Mbunge huyo amesema haoni sababu ya matumizi makubwa ya fedha katika sherehe hizo, wakati hali ya miondombinu ya barabara nchini ni mbaya.“Wizara inaandaa maonyesho ya sherehe ya miaka 50 ya uhuru huku Mtanzania wa kawaida wa kijiji anaishi maisha magumu; ni vema fedha hizi ningeletewa hata katika jimbo langu ili tuweze kutekeleza miradi ya maendeleo hasa ya barabara iliyosimama kutokana na kukosekana na fedha.

Mbunge huyo alisema hatuna haja ya kusherehekea miaka 50 ya uhuru wakati hakuna huduma muhimu za kijamii na watu wanaishi maisha duni kutokana na ahadi zisizotekelezeka.

“Hakuna utekelezaji wa ahadi. Barabara hatuna za lami, hatuna maji ya uhakika hasa katika maeneo ya vijijini. Sasa umefika wakati kwa serikali yetu isikie kilio hiki,” alisema na kuongeza kuwa wilaya ya Ludewa haina umeme wakati kuwa makaa ya mawe ya Liganga na Mchuchuma na ukelekezaji wake umesimama kutokana na kukosekana kwa fedha na ahadi zisizotekelezwa kila mwaka,” alisema Filikunjombe.

Alisema kama miradi hiyo ya makaa ya mawe na ule wa Mchuchuma ingefanikiwa kutekelezwa kwa wakati ingesaidia kukuza ajira kwa vijana hasa wilayani Ludewa pamoja na mikoa ya Nyanda za Juu Kusini. Akizungumzia uwajibikiji wa viongozi wa serikali, Filikunjombe alisema ni vema nafasi za uwaziri, ukuu wa mikoa na wilaya wapewe watu wenye moyo wa uzalendo na uchungu kwa nchi yao lakini hivi sasa imekuwa tofauti.

Alisema hatua ya baadhi ya mawaziri wanaofanya sherehe kubwa ya kujipongeza wakiteuliwa, inachangia kuporomosha misingi na maadili ya taifa na hata wakati mwingine hufikia kutumia fedha za walipa kodi kwa anasa.

Alitoa mfano wa viongozi wasiowajibika katika matukio ya mabomu ya Mbagala na maafa ya kuzama kwa meli. “Mara baada ya mabomu ya Mbagala Watanzania waliahidiwa kutotokea tena milipuko hiyo lakini baada ya muda tumeshuhudia yakilipuka Gongolamboto. Kiungwana watu wa aina hii walitakiwa kujiwajibisha wenyewe kuliko kusubiri Watanzania wakuwajibishe na hiki ni kipimo tosha cha kukosa moyo wa kizalendo.”

Aliongeza hata ajali ya meli ya Mv. Spice Islenders, ilitakiwa mawziri wenye dhamana kuwajibika. “Watu wanapoteza maisha kila siku lakini watendaji na wasimamizi wakubwa wako kimya; nini kinachowakawiza kuwajibika?” aliuliza mbunge huyo kijana. Filikunjombe, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Hesabu za Mashirika ya Umma, alisema tume zinazoundwa kwa ajili ya kuchunguza ajali hizo mara nyingi zimewaacha huru watuhumiwa.

Source: Tanzania Daima, 19 September 2011
 

Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
409
Hivi huwa hakuna source nyingine zaidi ya Tanzania Daima? Wanapomhoji huyo msemaji wanakuwa peke yao?
 

M-pesa

JF-Expert Member
Sep 4, 2011
602
151
Kama yaliyoandikwa ni ya hakika kutoka kwa Deo Filikunjombe, basi nampa jamaa big up sana. Kwani context ya kilichoandikwa kina mantiki kubwa.

Hivi huwa hakuna source nyingine zaidi ya Tanzania Daima? Wanapomhoji huyo msemaji wanakuwa peke yao?
<br />
<br />
 

Luiz

JF-Expert Member
May 23, 2011
342
36
Mbopo wewe unaiamini source ya Gazeti la uhuru tu? Kwa taarifa yako uhuru hawawezi kutoa taarifa yenye ant-ccm.
 

Ludewa

JF-Expert Member
Mar 9, 2009
215
36
Hivi huwa hakuna source nyingine zaidi ya Tanzania Daima? Wanapomhoji huyo msemaji wanakuwa peke yao?

Tanzania daima ni gazeti makini. Haya mahojiano Filikunjombe kayafanya Jumapili asubuhi kwenye kipindi cha Star TV. Nilimsikiliza kwa makini. Nilimwelewa, alichokisema Filikunjombe kwa ujumla ni alisisitiza dhana ya uwajibikaji toka kwa viongozi wetu tulowapa dhamana ya kututumikia ili kuwansuru watanzania kutoka kwenye wimbi hili la umaskini.
 

Tundapori

JF-Expert Member
Aug 12, 2007
563
151
Huyu naye asituzengue wadanganyika. Yaani leo hii 19/9/2011 ndiyo anajua kuwa serikali ya Danganyika ina ahadi nyingi zisizo tekerezeka. Maajabu kweli haya kazi kupiga makofi tu.
 

Tetere Enjiwa

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
217
65
Hili la maandalizi ya sherehe za miaka 50 ya tanganyika, na matukio yanayofanywa kuelekea kilele cha sherehe zenyewe is another EPA on making tusubiri tutataona kiasi kitachokuwa kimetumiwa hii ndio TZ yetu.
 

Ave Ave Maria

JF-Expert Member
Apr 22, 2011
10,735
5,613
Hivi huwa hakuna source nyingine zaidi ya Tanzania Daima? Wanapomhoji huyo msemaji wanakuwa peke yao?

wewe, macho yako, masikio yako, miguu na mikono yako, pua yako, pamoja na ubongo wako ni source tosha kabisa! Licha ya kuwa ameongea mtu mwingine lakini hata wewe mwenyewe ni shahidi tosha kabisa wa hizo ahadi zisizotekelezeka hata kama hautasema lakini akilini mwako unalitambua hilo! Mabomu ya mbagala na gongo la mboto nayo yanahitaji kujaza source ya magazeti hapa??, au kuna mtu ama kiongozi husika yeyote ambae amewajibishwa kuhisiana na hayo majanga ambae wewe mwenzetu unamfahamu utuambie na hizo source zako unazozitaka?? Miundo mbinu duni inaonekana waziwazi kabisa wala haihitaji kusontewa ndo utambue na hata kama wewe ni kipofu lazima ujikwae tu na uteguke miguu kwa mabonde ya barabarani, na kama wangetekeleza ahadi zao haya yote yasingetokea! Au wewe unayafurahia haya?? Wangekuwa wawajibikaji katika ahadi zao ile meli ingerundika abiria kiasi kile mpaka ikazama? Embu kuwa muungwana na ukubali iliyo kweli na sio ulazimishe kuletewa sources mia mbili hapa ilihali halisi yenyewe inaonekana wazi!
 

gmosha48

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
2,399
1,468
Huyu jamaa kwa upepo unavyoelekea 2015 out...

Huyu mheshimiwa si ndio yule alikoswa koswa kichapo kutoka kwa wabunge wa CDM?? Inaonekana kule kusutwa kwake na wabunge wa CDM ( siku ile wenje alipotolewa mjengoni) kumemfungua macho na akili zake. Sasa ameamua kutetetea watu wake badala ya kushabikia chama. Good job!
 

Ave Ave Maria

JF-Expert Member
Apr 22, 2011
10,735
5,613
Hili la maandalizi ya sherehe za miaka 50 ya tanganyika, na matukio yanayofanywa kuelekea kilele cha sherehe zenyewe is another EPA on making tusubiri tutataona kiasi kitachokuwa kimetumiwa hii ndio TZ yetu.

yap! Tena huu utakuwa ni ufisadi na unyama kuzidi hata ule wa EPA nakwambia! Wanasherekea miaka 50 ya ccm na ufisadi waloufanya pamoja na kuuza roho za watanzania wasiokuwa na hatia! Unafiki mtupu, kuna uhuru gani anaoupata mwananchi wa Tanzania wakati ananyang'anywa ardhi ktk nchi yake na serikali inafurahia?? Ana uhuru gani wakati wazungu, waarabu, wachina wahindi na makabacholi mengine ndo yanayothaminiwa na kuishi kwa raha hapa kwenye ardhi ya mtz kuliko mtanzania mwenyewe? Mkulima na mfanyabiashara wa kitz hana uhuru na soko, wageni ndo wameliteka na sasa hivi wanauza hadi vyakula, je wanasherekea jinsi chakula halisi cha mtanzania kilivyododeshwa na wavamizi? Alafu eti wanajidai kufanya maandalizi ya gharama kuuubwaaa wakati hata yule mhanga wa ajari ya meli pale Nungwi hawajamsaidia?? Tuwaeleweje hawa watu zaidi ya kuwa ni wafujaji na mafisadi wanaojilipa jasho la mtanzania kwa kumnyonya?? Serikali iache unafki kwa kuugharamia uhuru hewa!
 

Duble Chris

JF-Expert Member
May 28, 2011
3,482
564
sasa ataitwa haraka sana aeleze kwa nini anakiuka kanuni za chama ambazo zinamtaka mwenye malalamiko ayapeleke kwenye vikao halali vya chama " moto anao utasikia tu "
 

Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,870
3,262
Wabunge wa CDM eg Regia, Zitto, Mnyika etc ninaomba muulize hili swali kwenye kikao kijacho cha Bunge la JMT. Je ni shilingi ngapi serikali imetumia kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika kuanzia, ngazi ya wilaya, mikoa, Taifa na kilelele chake December 9? Je, pesa hizo zilitengwa kwenye bajeti ya 2011/12? Je ni faida zipi (value of money) ambazo mwananchi wa kawaida amepata kutokana na sherehe hizo?Mimi mbunge wangu ni wa Magamba, ingawa tayari swali hili nimeshampatia katibu wake, lakini nina imani hataliuliza. Ninaomba kuwakilisha.
 

Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
409
Mbopo wewe unaiamini source ya Gazeti la uhuru tu? Kwa taarifa yako uhuru hawawezi kutoa taarifa yenye ant-ccm.

Conversely, hata Tanzania Daima haiwezi kutoa habari ambayo ni pro-CCM. Ndiyo maana magazeti haya yana hadhi sawa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom