Mbunge wa ccm ahusishwa na ubadharifu wa mafuta:ewura waomba abadilike loh shame ewura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge wa ccm ahusishwa na ubadharifu wa mafuta:ewura waomba abadilike loh shame ewura

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BASIASI, Mar 24, 2012.

 1. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,109
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  SIKU chache baada ya kubainika kuwepo kwa upotevu wa mabilioni ya shilingi katika Mpango
  wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (BPS), madudu zaidi yanadaiwa kugundulika katika utendaji wa Kamati ya Kuratibu Uagizaji Mafuta (PIC).

  Mwenyekiti wa PIC, Mansour Shanif anadaiwa kuendesha mambo ya kamati hiyo kama ofisi binafsi, hivyo kuzusha hali ya kutolewana na wafanyabiashara wengine wa mafuta.

  PIC ilianzishwa kisheria ili kuratibu mpango wa kuagiza mafuta kwa pamoja ambao ulianza
  rasmi mapema mwaka huu.

  Katika tuhuma dhidi ya mwenyekiti huyo ambaye pia ni mbunge wa Kwimba, inaelezwa kuwa akaunti za benki za PIC hivi sasa zinaendeshwa chini ya usimamizi wa kampuni binafsi ya Mansoor ambapo Meneja wa Fedha wa kampuni yake hiyo ni miongoni mwa watia saini katika


  Wafanyabiashara hao (majina tunayo) wanamlalamikia Mansour kwa kulazimisha kuwa
  Mwenyekiti Mtendaji nafasi ambayo haipo kwenye muundo wa uongozi wa PIC.

  “Kutokana na kujipa nafasi ambayo haipo, haishangazi kuona hadi sasa PIC imeshindwa hata kuajiri karani katika kipindi cha miezi mitatu tangu ianze kazi,” alisema mmoja wa wafanyabiashara hao.

  Aliongeza kuwa: “Wakati zabuni ya tatu ya kuagiza mafuta ikitarajiwa kufunguliwa wiki
  ijayo, utaratibu mzima unaohusisha mabilioni ya shilingi unafanyika bila ya kuwepo kwa mipango inayoeleweka ya utawala na uendeshaji wa ofisi.”

  Kutokana na kukithiri kwa dosari katika mpango huo, Mwenyekiti wa PIC, Mansour, amejikuta katika malumbano na baadhi ya wanachama wa kamati hiyo na uongozi wa EWURA, ambao umemwandikia barua kutaka hali hiyo irekebishwe.

  Hata hivyo, Mansour akizungumza na gazeti hili jana alisema kuwa, ni kweli amepokea barua, huku akisema mengi yanayoenezwa juu yake ni uzushi unaosababishwa na chuki ya kibiashara.

  Katika barua ya EWURA ya Machi 16 mwaka huu kwenda kwa PIC, ambayo gazeti hili lina

  nakala yake, mamlaka hiyo inamtaka Mansour kufanya kazi na wenzake kama timu ili kuhakikisha mpango wa uagizaji mafuta kwa pamoja unafanikiwa.

  Barua hiyo iliyotiwa saini na Anastas Mbawala kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa EWURA,
  inasema mamlaka imepokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa PIC kuhusu kutoelewana na mwenyekiti wao.

  Miongoni mwa sababu za kutoelewana ni kuhusu usalama wa nishati hiyo na bei ya kununua na kuuza.

  Katika barua hiyo kutoka EWURA, PIC inaelekezwa kufanya ajira ya menejimenti yakudumu na watumishi wengine. Kutokana na hali hiyo, EWURAiliielekeza bodi ya PIC kuwa ndani ya siku saba irekebisha hali hiyo.
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  i see . . . .
   
Loading...