Mbunge wa Buyungu, Kasuku Samson Bilago azidiwa akiwa Dodoma, Apelekwa haraka Hospitali ya Muhimbili

Status
Not open for further replies.

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
20180522_150003-620x330.jpg


MBUNGE wa Chadema katika jimbo la Buyungu, mkoani Kigoma, Mwalimu Kasulu Bilango, anayekabiliwa na maradhi ya utumbo, amesafirishwa kwa ndege maalum kutoka Dodoma kuekea Dar es Salaam, mchana huu.

Mwalimu Bilago amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa kwa wiki mzima sasa ambapo alilazwa katika hospitali moja ya Kanisa mjini hapa.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa John Pombe Magufuli, mkoani Dodoma, Mwalimu Bilago amesindikizwa na watu kadhaa wakiwamo wabunge na maofisa wa Bunge.

Miongoni mwa viongozi wa umma waliokuwapo uwanja wa ndege kumsindiza mbunge huyo, ni pamoja na mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.

Wengine, ni mbunge wa viti Maalum mkoani Dodoma, Immaculate Sware Semesi; mbunge wa Viti Maalum mkoani Geita, Upendo Peneza; Mariam Msabaha na Gimbi Masaba.

Akizungumza kwa shida wakati akitolewa kwenye gari la wagonjwa kupandishwa ndege, Mwalimu Bilago aliwataka wabunge wenzake kuendelea na mapambano.

“Nakwenda kupata matibabu Dar es Salaam. Niombeeni kwa Mungu nipone kwa haraka. Lakini ninachowaomba endelezeni mapamba haya,” alisema Bulago.

Akijibu ombi hilo la Bilago, Kubenea alimhakikishia mbunge mwenzake kuwa watafanya maombi na wataendeleza “vita ayoicha.”

*Nenda katibiwe Mwalimu. Sisi tutafanya kilichosalia. Usihofu,” alisema Kubenea kwa kujiamini.

UPDATE

Wakuu,

Mbunge wa CHADEMA, Mhe. Kasuku Samson Bilago amefariki dunia mchana huu katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili.

Marehemu alizaliwa 2 Februari 1964 alikuwa mwanachama wa cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA). Alichaguliwa kuwa mbunge wa Buyungu kuanzia mwaka 2015 hadi mauti yalipomkuta.

Pia soma >Mbunge wa Buyungu, Kasuku Samson Bilago(CHADEMA) apelekwa hospitali ya Muhimbili akitokea Dodoma

Taarifa zaidi zitafuata...[/QUOTE
 
Mkileta habari za mgonjwa, zilete vizuri watu tumpe pole.Mtu yupo hoi anapandishwa ndege awaishwe Muhimbili mnaleta story za naenda kutibiwa endelezeni Mapambano, Mapambano GANI?,haya mambo ya kuwalisha wagonjwa maneno kwa UCDM wenu na UCCM wenu sio sawa, Yale Yale ya "Mheshimiwa I Survived To Tell a Tale", mpaka Leo mgonjwa hakumbuki TALE aielezee, sijui mlimlisha maneno. Tunamuombea mbunge apone haraka aje kuendelea na jukumu la kuwakilisha wananchi wake. Huyu wa Leo wa Kigoma, yule wa Ubelgiji shauri zake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom