Mbunge wa Buyungu, Kasuku Bilago Samson(CHADEMA): Serikali shule binafsi zinawahusu nini, ni wivu tu

data

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
26,149
22,723

Serikali kwanini kila siku matatizo ni yaleyale na mwashindwa yatatua.

Tunasubiri majibu ya Waziri toka kwa hoja hizo.
By the Way..huyu ni CCM!!???
 
Serikali kwanini kila siku matatizo ni yaleyale na mwashindwa yatatua.

Tunasubiri majibu ya Waziri toka kwa hoja hizo.
By the Way..huyu ni CCM!!???
Kwa kweli kwa hili la elimu blablaa zimezidi. Tena Ndaluchako ndo kavurunda kabisa. Elimu elikuwa enzi za Jackson Makweta. Tusubiri tu tutajionea mengi na bado Bomu la elimu Msingi linakuja hadi leo drs la NNE hawana vitabu.
 
Elimu itambulike kama huduma kama ilivyo hospitali na hivyo isiwe chaka la wafanyabiashara.Shule ya msingi inatoza ada kuliko University za China!!
Shule za Private zinaendeshwa kiujanja ujanja tu...

Swala la msingi serikali iboreshe shule zake hizo private zitajifia
 
Kiukweli gavana ifungwe kwenye hizi private school,itafikia hata mnaosapoti waaachwe mtaanza kulia,elimu kuigeuza biashara badala ya huduma ni kutengeneza matabaka ndani ya jamii
 
Jackson Makwetta duh umenikumbusha mbaliii
Shida matamko yamekuwa kibao hadi yanawachanganya watekelezaji wa mtaala. Mfumo wa uaandaji vitabu na usambazaji vitabu si wa kuridhisha. Enzi za Jackson Makweta. Drs la saba anayehitimu anakuwa kaiva kweli na hao drs VII waliovishwa na mfumo mzuri wa elimu enzi hizo ndo waliwafundisha akina prof Hadija. Lakini enzi hizi za Prof Hadija anayetamba yeye yuko makini form four wake unakuta ana B au C ya Hisabati au Kiingereza na amemaliza cheti cha ualimu au diploma au degree ukimwambia afundishe drs la sita au la saba anasema hawezi. Na hao ndo walimu walio wengi wapo serikalini na wana Vyeti Og wamebaki kunyang'anyana ma stadi za Kazi na Kiswahili ambacho pia bado wanafelisha wanafunzi.
 
Kiukweli gavana ifungwe kwenye hizi private school,itafikia hata mnaosapoti waaachwe mtaanza kulia,elimu kuigeuza biashara badala ya huduma ni kutengeneza matabaka ndani ya jamii

Hebu ziacheni shule binafsi zifanye kazi. Hizi shule zimekuwa kimbilio la mwisho kwa wazazi makini wasiotaka mchezo na elimu ya wanao. Na hata kama mtafanikiwa katika azma yenu ya kuziuwa, hawa wazazi makini hawatasita kuwapeleka watoto wao Kenya, Uganda au kwingine kokote kwenye elimu bora. Ni sawa na jinsi wewe unavyochukulia waganga wa kienyeji kama kimbilio lako la mwisho kwa kila kitu.
 
Blabla kama kawa!Kifuatachp ni kuua private schools, si mnaona za chama zimeanza?
Private sector inahitaji usimamizi usio na misingi ya chuki.
Za kupewa na Xi Jing Ping tuchachanganye na zetu, na mchanganyo huo tuuenzi.
 
Kiukweli gavana ifungwe kwenye hizi private school,itafikia hata mnaosapoti waaachwe mtaanza kulia,elimu kuigeuza biashara badala ya huduma ni kutengeneza matabaka ndani ya jamii
Kufunga gavana haitawezekana ikiwa serikali haitaboresha shule zake. Miaka ya 1980 shule za sekondari za serikali ndizo zilikuwa bora zaidi, matokeo ya darasa la 7 yalikuwa yanasubiriwa kwa hamu na waliochaguliwa kwenda sekondari za serikali walionekana vichwa kwelikweli na ilikuwa sifa kubwa kujiunga na shule za serikali.

Siku hizi shule za serikali ndizo zinaongoza kwa kufelisha ukiondoa zile zilizoitwa spesho ambazo ndio angalau utazikuta ndani ya 100 bora.

Dawa ni kuimarisha shule za serikali zitoe elimu bora, hizi za private zitashusha ada bila kulazimishwa.

Vv
 
Kwa maoni yangu,naona hamna shida mkuu. Iwe huria kila mtu amsomeshe mtoto wake shule anayotaka
 
Elimu itambulike kama huduma kama ilivyo hospitali na hivyo isiwe chaka la wafanyabiashara.Shule ya msingi inatoza ada kuliko University za China!!
si upeleke watoto wako shule za Kayumba wakavute bangi !
 
  • Thanks
Reactions: cai
Back
Top Bottom